Wanaume mnaocheza vikoba mnatia aibu

Bora umeelewa Hilo Kuna vicoba wanacheza had million 20 had 30 na vipo wapo wanacheza upatu wengine wananunuliana magari kifupi ni Level ya maisha ulonayo tu sio ishu ya kusema hakina maana
Kwakweli, kuna watu wanaweka hisa kila week laki 5,

Na kuna sisi tunaosema wanaume wanaocheza vicoba hawana hela[emoji23][emoji23]
 
Upo vizuri,.nina ushahidi kwa hili ulisemalo.
Upo wazi popote alipo mwanamke mpambanaji. Siku hizi vijana wa kiume wanalelewa na kuwekwa ndani na wanawake sababu wanawake wanapambana. Usishangae kukutana na kijana mponda vicoba akiendesha gari la mwanamke wake lililonunuliwa kwa pesa ya kicoba ila yeye hawezi hata kuweka mafuta.
 
Umeelezea kitu kingine, hio sio vikoba. Huo ni upatu
 
[emoji419][emoji419]
 
Watu nendeni shule mpate elim. Nch zilizoendelea kina kitu inaitwa welfare. Hulu kwetu nchi maskin inaitwa community welfare tunajifariji na kujikimu wananch wenyewe, familia, majirani, graduates, wanaume au wanawake, bodaboda, madereva nk nk ukifika kwenye vikundi mbalimbali utakita wanacheza 1000 Kila siku, niliona bodaboda wanafanya hivyo, madereva daladala, wanafanya umoja wao na wananunua usafiri wao.

Nirejee nchi tajiri zenye uchumi mkubwa, jobless analipwa, mfanyalazi ukiwa hunakaz utapewa fedha Hadi pale utalapopata mshahara.

Waafrika,tRNA watanzania wastaarabu unatoa wapi ujinga was kuona upatu,vikona na namnambalimbali za kuweka hisa kama gender problem?

Mtachelewa aana kufika,Tena waname unawarudisha sana nyuma wanawake kimaendeleo. Wengi hivi vikoba vinalipa ada, Kodi ,matibabu hiyo nidhamu ya kuweka pesa mwenyewe unaipata wapi. Sijawahi kusikia kijumbe wakiume! Inatia aibu, oneni aibu mnatia aibu. Mmebaki nyuma nyuma. Wengi wenu mmejaa unapiga bodaboda hivi bodaboda ndio kazi yamaana Sana? Hata konda wa daladala inaafadhali, Acheni upuuz wenu.

DeepPond rekebisha kauli yako
 
Si ununue ya blue?Huoni kama unachochea dhambi ya usengenyaji?[emoji28][emoji28]
Nilipanga ninue rangi tofauti mshahara wa mwezi wa nane ulipotoka , sasa kichekesho ni kuwa ulitoka mshahara ila nilienda mpaka sokoni wanakouza suruali ili walau ninue moja rangi tofauti.

Shida kuna jamaa akasema nisubiri jioni zinakuwepo nyingi nzuri na bei ni ndogo kwa hela yangu naweza kupata hata mbili maana bajeti yangu ilikuwa elfu tano .

Mpka inafika jioni hela yote nilikuwa nimeshampa barmed nilikuwa na elfu mbili hela ya daladala kunifikisha stand ya basi lilipo basi la kwenda kituoni kwangu kulitumikia taifa .

Dada Joannah hili namuomba Mungu nilifanyie kazi bila kuzubaa

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Anyway, nilipokuwepo au ambako bado nipo upatu umebaki upatu. Idea ya vicoba ni idea tofauti na upatu. Halafu umeniita wa 2010 hahaaa inshu ni kuwa wewe umeona vicoba mapema labda ulikuwa village Mimi cooperative unions/ devlommt and the like nimechelewa labda kuziona kulingana na mazingira nimeona sana sana upatu wa akina mama ndiyo maana nasema idea yao ni tofauti na upatu.

Halafu sidhani kama vicoba vimeanzia ktk idea ya upatu. Nafkiri vicoba vimeanzia ktk nchi za kibepari kwa kuwa mfumo wake uko bank oriented lakini mchezo au upatu uko ktk kusaidiana kutimiza mbo ya kijamii zaidi na siyo kiuchumi zaidi. Nachelea kusema Round Table, Rotary, Freemasonry, Federal Reserve, Skull and Bones na nyinginezo ziko ktk idea za vicoba zaidi ya upatu zaidi.
 
Waanzirishi = waanzilishi, zinazowakabiri = zinazowakabili. Wewe jamaa utadhani ni bilionea kumbe ni kenge mmoja anayemiliki smartphone
 
Vicoba ni nini?

Vicoba ni Village community bank.

Kwahiyo ukielewa maana ya Vicoba hakuna tatizo lolote kwa mwanaume kushiriki.
Kabisa mkuu. Umesema kila kitu.

Kuna Madaktari wastaafu wa Bugando Hospital (wanaume) wana Kikoba chao, and they are proud kukiita Kikoba.

Uncle wangu ni daktari bingwa mstaafu, kuna siku nilienda kumsalimia, ilikuwa j2, jioni akaniaga anaenda kwenye Kikoba.

Aliporudi tukawa tunastorisha kuhusu hicho Kikoba chao. Aisee kiko vizuri. Wanafanya mambo makubwa sana beyond maswala ya kiuchumi. Kuna nyakati wanatoa hadi huduma za kiafya kwa wahitaji.

Wote wako vizuri sana kiuchumi kupitia Kikoba chao. Sasa nashangaa mtu anayepotosha maana halisi ya Kikoba!

[emoji28][emoji28]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…