Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Wanaume, mpo? Nawauliza kwa upole kabisa, lakini kwa uzito wa moyo: Hivi nyie mnaokasirika kasirika hapa JF, mnaishije na wake zenu majumbani?
Naongea na wewe mwanaume, ambaye kila unapoandika mada, unapojibu maswali, unapochangia hoja, maneno yako hayakosi ukali, kejeli, hasira na wakati mwingine hata matusi. Sasa najiuliza, kama unaongea maneno ya namna hiyo mbele ya watu usiowaona humu, je ukiwa mbele ya mke wako hali ikoje?
Mke wako akipika chakula akakitia chumvi zaidi, kunakuwa na amani nyumbani au mvua ya maneno makali ndo inaanza kunyesha? Je, akichoka na kukosa nguvu, na siku hiyo akashindwa kukupa haki yako ya ndoa, unamwelewa kweli, au ndo hasira zinapopanda kama moto?
Hasira isiyodhibitiwa haijengi, inabomoa. Haiponyi, inaumiza. Na mara nyingi, huanza kidogo tu, lakini huishia kuvunja ndoa, kuharibu watoto, na kuondoa amani kabisa nyumbani.
Mwanaume uliumbwa kuwa kiongozi wa nyumba, lakini sio kwa kelele wala ukali, bali kwa hekima, upendo, na uvumilivu. Ukali sio uanaume. Matusi sio mamlaka. Hasira sio nguvu.
Kuna roho ya hasira ambayo imewakamata baadhi yenu wanaume. Hii roho inawasukuma kusema maneno ambayo hata mioyo yenu haikusudii kuyasema. Inawafanya muonekane wakali hata pale ambapo hapahitaji ukali.
Hasira ya mara kwa mara sio tu inaharibu mahusiano, bali pia inapunguza siku zako za kuishi. Moyo unachoka, mwili unachoka, akili inachoka. Unajiumiza mwenyewe bila kujua.
Leo nakutia moyo, wewe unayesumbuliwa na hali hiyo, inaweza kukutoka!
Yesu Kristo anaweza kukupumzisha. Anaweza kukutoa katika minyororo ya hasira. Anaweza kukupa moyo mpya wa upole, subira na unyenyekevu.
Njoo kwa Yesu sasa kwa imani, mwambie ukweli katika sala hii fupi. Omba hivi:
“Ee Mungu, nina tatizo la hasira, niondolee hali hii, niokoe, nifanye upya, katika Jina la Yesu, amen.”
Ukiomba hivyo kwa dhati, hakika Yesu hatakuacha, atakusaidia kuwa mpole na mwenye kiasi.
Mungu aibariki ndoa yako, na nyumba yako idumu kuwa mahali panapotiririka maziwa na asali.
Amen!