Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, mkoani Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Debora Magiligimba, amewataka wanaume wanaonyimwa unyumba kuripoti katika madawati ya jinsia yaliyopo katika vituo vya polisi kwani huo ni ukatili.
ACP Debora ametoa wito huo Desemba 1,2021 wakati wa maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili yaliyofanyika katika viwanja vya Tabata shule ambapo pia alikabidhi vitambulisho maalumu kwa madereva bodaboda na bajaji ili iwe rahisi kutambulika.
"Kunyimwa unyumba husababisha kupata ukatili wa kisaikolojia yanapotokea hayo nendeni dawati la jinsia mripoti...nasikia mnauliza mnaanzaje wewe njoo tutakusikiliza," amesema Kamanda Debora.
Chanzo: Mtanzaniadigital
#edwinmoshiupdates