Wanaume na dhana ya kutopenda mboga ya kabichi

Kwahiyo wewe ni nafaka tuu kwa kwenda mbele???
 
Wanawake wengi wanahisi kuweka miviungo mingi na mafuta ndo kujua kupika.

Kabisa yaani wangejua kwamba hatuyapendi ma spices kibao kwenye vyakula wasingefanya!! Mimi mivyakula yenye mifuta na spices siyapendi....Mimi weka nazi+chumvi basi lakini kuweka sijui miihiriki,sijui mipilipili manga,mara mi binzari mara miroyco,mara wamemix micurry podwer ,mara sijui nini masala siipendi.
 
Kwahiyo wewe ni nafaka tuu kwa kwenda mbele???
Hapana, nakula hata hivyo nisivyopenda nakula sichagui, ila wakati naishi peke yangu nilikuwa siwezi kula vitu hivyo. Ila nakula mihogo, ndizi, ugali (japo uambatane na nyama choma ndo unanoga), makande, viazi, n.k. ikiwemo fast foods, ila technically nakula hata nisivyopenda uzuri uwa zina kinyaa, ndiyo maana hata nyama ya mamba nakula
 
Unakula hata hupati taste ya unachokula, yani haieleweki unakula kitu gani hadi unaweza kuuliza hivi haya ni maharage kweli πŸ˜…
 
Yaan mtazamo wa Wageni watatu wa Kiume Nyumban kwangu ndio wa Wanaume wote?
 
Itakuwa umekula sana utotoni kama waliosoma boarding schools wanavyochukia maharage na Makande
Bilinganya sijui bamia sijui kisamvu mamamae pelekea mbuzi wakale nitazikuta kwenye nyama yao tu!
 
Mboga za majani ninazokula bila kulalamika ni mchicha, kabichi na matembele.

Nyingine nakula kwakua nasikia ni muhimu kwa kujenga mwili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…