Mkuu, kondomu zimeanza kutumika miaka ya 2000, hatuongelei mambo ya kabla ya hapo, mambo yamebadilika hatupaswi kuishi kikale kale. Sijasema mambo yataisha au hayatoisha, nachosema MIMBA SIO AJALI, mwanamke au mwanaume anapoenda kufanya tendo la ndoa bila kinga anafahamu kabisa mojawapo ya matokeo ya hicho kitendo ni MIMBA, neno ajali halifai hapa maana mtu hanywi maji akajikuta ana mimba, MIMBA INATAFUTWA, mtu anawekeza muda,nguvu na hata pesa ndo mimba inatokea. Matokeo ya uwekezaji wako hayapaswi kuitwa ajali. Hilo ndo nalokataa. Mtu yoyote anayefanya tendo la ndoa hapaswi kushtuliwa na matokeo ya tendo hilo iwe mimba, UKIMWI, kisonono etc, matokeo ya tendo yanajulikana kabla ya tendo kufanyika. Sisi sio ng'ombe au mbwa, sisi ni binadamu. Hata wanawake wanaowasakazia watoto wanaume zao mi siwaungi mkono, hao ndo wanasababishaga mtu anakuja kuwa na mahusiano na kaka yake wa damu au dada yake kisa mama alimficha baba halisi wa mtoto. Uwajibikaji ni kwa jinsia zote mbili sio mwanaume pekee.
Tunapaswa kujenga utamaduni wa uwajibikaji katika kila eneo ikiwemo eneo la mahusiano na tendo la ndoa ambapo takwimu zinaonesha jamii zetu ndo zinaongoza kwa matokeo ya kukosa nidhamu kwenye eneo hilo na madhara yanaenda zaidi kwa watoto.