Wanaume tuko desperate sana kupata ngono, ifike mahali wanaume tuwe na akili

Wanaume tuko desperate sana kupata ngono, ifike mahali wanaume tuwe na akili

Balqior

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2021
Posts
2,406
Reaction score
8,039
Nimefanya uchunguzi binafsi, ukitaka kujua ukweli ingia kwenye dm za wadada kwenye mitandao ya kijamii kama facebook, insta, humu jf, uone wanaume tunavojichoresha na kujidhalilisha na kujipendekeza Kwa kuwatumia wadada sms 20 za kimapenzi kwa mpigo, yoote hiyo ili upate attention ya mdada ambaye in real life humjui hakujui, Utakuta dm ya mdada imejaa sms toka kwa wanaume 9 tofauti, na hajawajibu hata mmoja bcoz Wote hawafahamu, sisemi its wrong kumtongoza mdada, ila tunatumia platform mbovu inayotufanya wanaume Tuonekane tuna njaa sana na ngono, ndio maana wanaume tunadharaulika.

Mtu unatumia laki 6 kumuhonga mdada uliekutana nae juzi Ili akupe penzi wakati huyo mdada hata hakujali, ukute hata hajakuomba io hela, hakuthamini, hajawahi kukupa Papuchi na hatokaa aje kukupa papuchi, wakati mdogo wako wa kike Kule kijijini hana hata sketi mbili na amekosa tshs elfu 80 ya ada..ila kijana mdogo wa kiume unawekeza hela kwenye ujinga, nilisoma mtandaoni kwa nchi kama Marekani kuna baadhi ya wanaume huwapa wanawake ambao wamekutana nao cku mbili zilizopita hadi usd 5000 (Tshs million 11) ili tu wapate mzigo mara nyingi hao wanaume hawapati hata busu toka kwa hao wanawake achilia mbali papa yenyewe.

Kwenye sekta ya mahusiano naona kwa kiasi fulani wanawake wametuzidi akili, huwezi kuta mdada amekaa anaanza kutuma sms Za kimapenzi kwa wanaume asiowajua mtandaoni, huwezi kuta mwanamke anatumia asilimia 60 ya mshahara wake kuwapa wanaume wanne tofauti ili afanye nao mapenzi.

Wanaume tuache wenge na tupunguze njaa ya ngono, tu-focus kwenye kujijenga kiroho (Tumtafte Mungu) tujijenge kiuchumi kwa manufaa yetu, ya ndugu zetu, Wake na watoto, watu jirani wanaotuzunguka na taifa kwa ujumla.

Kulala na wanawake wengi au kulala na kila mwanamke unaemuona sio sifa wala ujanja.
 
Back
Top Bottom