Wanaume tukumbushane tu mambo machache tunapochagua mke wa ndoa

Wanaume tukumbushane tu mambo machache tunapochagua mke wa ndoa

Kikubwa kuwa na misingi bora ya maisha, mke ana reflect vile ulivyo
Hili ndilo kosa kubwa wanalofanya vijana. Utawasikia nitambadilisha ndani ya ndoa

Usipuuze hata kidogo red flags wakati wa uchumba na urafiki la sivyo utajuta mbeleni

Mahaba yasikufanye uwe kipofu kuona uhalisi
 
Asante kwa maoni yako.

Ila kwa mwanaume makini anakuwa na standards za mwanamke wa kumfanya mke wake wa ndoa


Ivi ndugu hujawai kusikia wahenga wanasema,
Oooh mapenzi ni upofu
Oooh mapenzi ni ukilema
Oooh mapenzi ni..........sio wajinga wameyaona yakawashinda...but sio wote
 
Haya Mambo Hayana Ushauri Babuuu
Yana ushauri ndio maana hata Muumba kwenye vitabu vyake vitakatifu alitoa mashauri kuhusu kumtambua mke mwema na jinsi mume na mke wanavyopaswa kuishi maisha ya ndoa na kulea watoto.

Kama hayana ushauri vipi naye tuyapuuze mahusia yake?
 
Huo Ushauri Alifanya Kwa Kizazi Kilichopita Sio Kizazi Hiki Cha Karne Ya 21. Kuishi Na Mke Hakuhitaji Ushauri. Ushauri Wa NDOA Ni Kichwa Chako Mwenyewe
 
Mkiingia kwenye ndoa ndipo utajua uhalisia wa huyo mwanamke.

Huku nje kwenye uchumba kumejaa maigizo.
Ukweli ni kwamba licha ya maigizo wengi huona changamoto kubwa za wachumba wao. Tatizo la wengi:

● Uoga wa kufanya maamuzi magumu ya kusitisha uchumba

●Tatizo lingine ni mahaba na vile mahusiamo ni mapya yanawafanya wachumba (KE/ME) kupuuza madhaifu makubwa ya watu wao.


 
I think cha muhimu ni kuhakikisha kwanza kama mwanaume una qualities zote za mume bora na baba bora na sio tu kuwa na uwezo wa kudindisha.
Hawa wanawake tutawalaumu sana but birds of the same feather fly together.
Kama mwanaume ni wa kiwaki tegemea the same energy kwa mwanamke utakaemuoa maana wao pia ni binadamu.
Tujifunze kujirekebisha sisi kwanza na kuwa na qualities bora before hatujaanza kuchagua chagua
 
Mke mwema hutoka kwa Mungu! Mshirikishe Mungu katika kuchagua,mwambie akuchagulie Yeye mwenyewe! Yeye mwenyewe atakuongoza kwa mke sahihi!
SIsi wanadamu hata tufanyeje tunaangalia sura,chura,Mweupe,nk
Wanaume wengi wanajuta kuoa kwa sababu walitumia macho yao kuoa!
 
Huo Ushauri Alifanya Kwa Kizazi Kilichopita Sio Kizazi Hiki Cha Karne Ya 21. Kuishi Na Mke Hakuhitaji Ushauri. Ushauri Wa NDOA Ni Kichwa Chako Mwenyewe
Ninachojua hakuna ushauri wa ndoa na familia aliotoa Sir God umewahi kupitwa na wakati

Alisema mke amheshimu sana mume wake, mume ampende mke wake, watoto wawaheshimu wazazi wao, mume aitunze familia yake na mwanaume kabla ya kuoa awe na kitu cha kumwingizia ridhiki

Unafikiri hayo mashauri hayafai wakati wetu mkuu au yamepitwa na wakati?
 
Back
Top Bottom