Wanaume tunaopenda kuwa smart tusikose package hii

Wanaume tunaopenda kuwa smart tusikose package hii

Kukinga ngozi dhidi ya nini Mkuu?

Kama ngozi yako imeathirika na unatumia kama tiba sioni tatizo.

Ila kama inatumika kwa shabaha ya kuifanya ngozi iwe nyororo, ipendeze, inukie, imeremete. Hapa ndio naweza kushangaa
Kukinga ngozi dhidi ya changamoto za afya ya ngozi. Ngozi yangu ni nyepesi kushambuliwa na mba. Hii sabuni na lotion imekuwa kinga
 
Ready to go
17373613979816881405734584256617.jpg
 
Pengine asili ya ngozi yako. Lakini wengine ngozi zina shida. Kuna mtu ngozi kavu anapauka, angefanyaje? Mwingine mweusi tii anatoka ukoko, angefanyaje?
Heeeeh!!!! kumbe hili nalo ni tatizo??

Matatizo ya ngozi mi najua ni muwasho, fangasi, kutoka ukurutu, kutoka mapele, mzio nk.

Kumbe hadi kupauka kwa ngozi nako ni tatizo??
 
Kukinga ngozi dhidi ya nini Mkuu?

Kama ngozi yako imeathirika na unatumia kama tiba sioni tatizo.

Ila kama inatumika kwa shabaha ya kuifanya ngozi iwe nyororo, ipendeze, inukie, imeremete. Hapa ndio naweza kushangaa
Hapana, hayo mafuta ni ya kiume. Hayafanyi mtu kung'aa na kuwa nyororo kama ya wanawake. Bali yanamuweka smart. Labda kwa vile huyajui.
 
hamna, kwanza kiasilia ngozi ya ME haihitaji matunzo kama ya KE

halafu asilimia kubwa ya matunzo ya ngozi ni kwenye mlo

ni katika kujiepusha na ngozi kavu na makunyanzi, pia chunusi, na makovu kovu
 
Hapana, hayo mafuta ni ya kiume. Hayafanyi mtu kung'aa na kuwa nyororo kama ya wanawake. Bali yanamuweka smart. Labda kwa vile huyajui.
Mkuu wanaandika yakiume ku-target soko.

Kwenye chupi tu ndio naweza kukubaliana kuwa zipo za kiume na za kike lakini sio kwenye hizi lotion ambazo zimetengenezwa kwa makemikali

Binafsi siamini kama kuna chemical ya kike au ya kiume.
 
Noma sana aisee....
Nilikuwa nadhani huwa ni wanawake tu wenye mafuta ya uso, mafuta ya kiwiliwili, mafuta ya mikono kumbe yapo kwa ajili ya wanaume pia.
Ngoja nizidi kujifunza maana nilidhani ninajua yote kuhusiana na mafuta nikaja kusikia kuwa kuna mafuta hata ya Pdiddy.
Vipi unataka upakwe?
 
hamna, kwanza kiasilia ngozi ya ME haihitaji matunzo kama ya KE

halafu asilimia kubwa ya matunzo ya ngozi ni kwenye mlo

ni katika kujiepusha na ngozi kavu na makunyanzi, pia chunusi, na makovu kovu
Kabisa mkuu ndio maana hata katika puberty stage kati ya mwanaume na mwanamke utaona asili inayojidhihirisha.

Mwanaume akifikia stage ya puberty lazima awe na ngozi yenye machunusi hovyo hovyo na sauti kuwa nzito.

Wakati mwanamke hicho kipindi mwili wake huzalisha homoni ya sebum kwa wingi ambayo husaidia kufanya ngozi yake iwe nyororo na laini.
 
WaTanzania wengi wanahitaji elimu juu ya afya ya ngozi zao, utunzaji wa ngozi hakuingiliani na mwanaume kuwa soft au mlaini, ni afya kwa ujumla.
Kwenda sauna, kwenda barbashop n.k kwa ujumla ni kujitunza...

Ndio maana ukitembea sehemu nyingi Tanzania, vijana wengi ni kama wakimbizi kimuonekano, mtu kajichokea, hawajali kuhusu ulaji na afya... ukitokea na muonekano wa tofauti wanaanza kukutizama wanajua kabisa huyu si mbongo mwenzetu...
Ama huyu ni tajiri... tubadilike...
 
Back
Top Bottom