Wanaume tupambane kwa nguvu zote tuwafungulie wake zetu biashara wajiajiri

Wanaume tupambane kwa nguvu zote tuwafungulie wake zetu biashara wajiajiri

Umesahau na watoto kwa kiasi kikubwa kulelewa na mahausigel,mtoto anayelelewa na mtu baki asiyekuwa mzazi wake ni hatari sana hana kitu kinachoitwa maadili.

Hao house maids mabwana zao ni bodaboda drivers na wauza magenge hawa wakati ninyi wazazi mmeenda kazini mchana wanaingizwa kwenye nyumba zenu wanawapiga pipe hadharani mbele ya watoto wenu wadogo nao watoto wanaona sawa wakikua unashangaa unaletewa kesi mwanao aged 17 anainamishwa uchochoroni mzazi unaenda kulaumu shule anakosoma unasahau hukumpa malezi mazuri nyumbani.
 
Wanaume tupambane kwa nguvu zote tufungue biashara ili wake zetu waweze kuzisimamia.

Hii hali ya kuoa mwanamke aliye ajiriwa kuna changamoto zake kama ifuatavyo:-​
  • Kazi ndio mme wake​
  • Mumewe ni chaguo la pili baada ya kazi​
  • Anaiheshimu ile kazi na anaitii kuliko anavyomtii mme wake​
  • Kazi inamfanya alale nje au wakati mwingine awe mbali na mumewe (safari za kikazi)​
  • Anamtii bosi wake kuliko mume wake​
  • Bosi akiwa kipanga atatembea na mkeo kwa kumuwekea mazingira ya posho posho n.k​
  • Ikitokea kazi inamhitaji nawe unamhitaji, atasikiliza kazi kwanza na wewe unawekwa pending​
  • Ikitokea amehamishwa mkoa au nchi,inabidi uwe mpole tu sababu kazi ndio iliyomuoa​
Mfano mdogo tu; mkeo akipigiwa simu na bosi wake ataanza kutetemeka zaidi kuliko anavyopigiwa simu na mumewe.

Swali, Je wake wa matajiri wameajiriwa?
Amka mwanaume, mfungulie mkeo biashara ajiajiri, kuajiriwa sio sifa.​
Naunga mkono hoja 100%. Nimekuwa mwajiriwa na mfanyabiashara kwa nyakati tofauti. Unachozungumza Ni halisi.
 
Back
Top Bottom