Wanaume tupambane kwa nguvu zote tufungue biashara ili wake zetu waweze kuzisimamia.
Hii hali ya kuoa mwanamke aliye ajiriwa kuna changamoto zake kama ifuatavyo:-
Kazi ndio mme wake
Mumewe ni chaguo la pili baada ya kazi
Anaiheshimu ile kazi na anaitii kuliko anavyomtii mme wake
Kazi inamfanya alale nje au wakati mwingine awe mbali na mumewe (safari za kikazi)
Anamtii bosi wake kuliko mume wake
Bosi akiwa kipanga atatembea na mkeo kwa kumuwekea mazingira ya posho posho n.k
Ikitokea kazi inamhitaji nawe unamhitaji, atasikiliza kazi kwanza na wewe unawekwa pending
Ikitokea amehamishwa mkoa au nchi,inabidi uwe mpole tu sababu kazi ndio iliyomuoa
Mfano mdogo tu; mkeo akipigiwa simu na bosi wake ataanza kutetemeka zaidi kuliko anavyopigiwa simu na mumewe.
Swali, Je wake wa matajiri wameajiriwa?
Amka mwanaume, mfungulie mkeo biashara ajiajiri, kuajiriwa sio sifa.