Wanaume tupeni majibu sahihi kwanini mnapenda kuwachumisha wengine dhambi?

Wanaume tupeni majibu sahihi kwanini mnapenda kuwachumisha wengine dhambi?

kumbuka wakati unataka nifanye maamuzi ya busara nipo kwa mwanamke napewa vitu vitamu.hapo ni muumba aingilie kati kunusuru.

ivi ivyo vitu vitamu vinaharibu akili sio??
Sasa kwann unaporudi kuja kutafuta huruma/msaada usiende kwa huyo anokupa vitu vitamu?
 
Asante mamii gfsonwin

Yani tunarudi pale pale kwenye ubinafsi. Anakuwa anataka shida zake ziwe za wengine, hisia zake za kulia lia ziwahusu hiyo familia yake alotelekeza bila kujali wao wanajisikiaje.

Watu wabinafsi ndivyo walivyo..hawajali wengine.Everything has to be about them and no one else.
Lizzy karibu
ivi usipmuonea huruma mtu kama huyu ni dhambi?
well leo nimekutana na kisa hiki, mama tena baba kijana alitelekeza familia for 8 yrs leo hii eti mkewe wa ndoa anapigiwa simu mumeo kapata ajali mbaya sana iringa na kalazwa hosp ya rufaa iringa, huyu mdada kwao ni dodoma na hivyo alipotelekezwa akarudi dom kwa ndg zake kisha kaka yake akamchukua kuja mjin na wanae akabaingaiza maisha ndo akaweza kujenga huku uswen kwetu.
sasa huyu dada anasema jaman ivi mie naenda kupitia wapi? je niseme naenda kwa wakwe ama? na je nikimsusa inakuwaje?
mbaya zaid wifi yake anampigia simu jaman wifi njoo yaan hata mtu w akumuogesha hatujapata?? uwiii nimeshindwa kumwambia aende ama asiende
 
Last edited by a moderator:
Yaani ni kero na tena usiniambie maana kwangu majanga tupu.... Kwa kifupi kabisa wanawake wenzenu wasio na fadhila na wasioheshimu ndoa na muundo wake ndio wanaowapoteza hawa wababa mafedhuli na wasio na heshima... Kwa sasa wanasema michepuko...Hivi kama kila mwanamke angejaribu kuubeba mzigo wa mwenzie na kuwakimbia hawa wababa watia nuksi unafikiri kuna ndoa au familia ingekuwa njia panda???????? Wanawake hampendani ila pia kwa aina hii ya wababa mimi naona bora wasingezaliwa au wangeishia mateja na machizi ili wasiharibu dunia zaidi.
mweeeh!! iyo like nimekupa kwasabb tu umetoa maoni yako ila kwakweli umekuwa mkali sana teh teh teh
mie nasema ivi huyu baba anaye kwapuliwa akili yeye anakuwa amempa nani izo akili amshkie? ivi huwa mchepuko unaweza kununua akili ya mtu kwa kiasi hicho? mie nadhani ni utash wao wa ndani kwakweli
 
Chanzo cha hili tatizo ni wanawake wenyewe wala usiwalaumu wanaume. Mfano mimi mwenyewe nina mtoto nimezaa na dada mmoja hivi. Nimemuhudumia toka mimba hadi mtoto na nilikua nina mpango wa kuoa, lakini yaliyotokea sina hamu nayo. Tukafika point tukakubaliana kuangalia kweli nikawa nahudumia lakini mtoto akawa hali yake hainiridhishi. Mtoto akiwa na mwaka na nusu akapata kazi akasema hawezi enda na mtoto anamucha nikasema mlete kwangu. Akamleta nikampeleka humo akawa analelewa huko. Mtoto alibadilika akachangamka akanenepa akawa na afya kulingana na umri wake. Akaja mchukua likizo akaenda nae lakini nasikitika kagoma kumrudisha ili aanze shule zile za watoto. Inaniuma sana maana yule mwanamke atamtesa mtoto hana mapenzi na mtoto hata kidogo. Hasira zake zote anazipeleka kumkoromea mtoto. Yaani kanikatisha tamaa nikasema basi waendelee na maisha yao. Lengo langu ni kumjenga mtoto kielimu kipindi hichi nina uwezo lakini umimwambia hivyo anadai ukimchukua najiua
 
Baba huwa hamwachi mwanae,anamwache pale mtoto akikaidi ushauri wa baba,unakuta mababa wengine wa kizamani,sasa mtoto anakuja kutoboa baba anakuwa piriton maana alimshauri mtoto asingefanikiwa kwa njia hizo,mfano,baba wa diamond usikute aliwahi kumshauri diamond asivae cheni,hereni,asiimbe mziki ni uhuni,leo mtoto katoboa baba mdomo wazi na amekumbwa na matatizo no option wakati diamond ana choo cha gold iliyogarimu million 70 sawa na kombe la timu zote Tanzania bara inayogombaniwa...........cha msingi usimpotezee baba,anaweza ongea pumba ila kuna point lazima inakuhusu.
Viol ivi unajua kuwa kuna akina baba wanatelekezaga watoto kabisa na kuwaacha na mama?
tena akiwa na iman kwamba sitaki tena kuwa karibu na hawa watu?
 
Last edited by a moderator:
Wala usiwaze!
Mara nyingi maswali magumu majibu yake ni mafupi sana japo sio rahisi kuyaelewa bila kufafanuliwa. Sababu ni:

Inatokea hivyo kwa sababu ya incompatibility ya changamoto za maisha ya mume na mke!
 
Chanzo cha hili tatizo ni wanawake wenyewe wala usiwalaumu wanaume. Mfano mimi mwenyewe nina mtoto nimezaa na dada mmoja hivi. Nimemuhudumia toka mimba hadi mtoto na nilikua nina mpango wa kuoa, lakini yaliyotokea sina hamu nayo. Tukafika point tukakubaliana kuangalia kweli nikawa nahudumia lakini mtoto akawa hali yake hainiridhishi. Mtoto akiwa na mwaka na nusu akapata kazi akasema hawezi enda na mtoto anamucha nikasema mlete kwangu. Akamleta nikampeleka humo akawa analelewa huko. Mtoto alibadilika akachangamka akanenepa akawa na afya kulingana na umri wake. Akaja mchukua likizo akaenda nae lakini nasikitika kagoma kumrudisha ili aanze shule zile za watoto. Inaniuma sana maana yule mwanamke atamtesa mtoto hana mapenzi na mtoto hata kidogo. Hasira zake zote anazipeleka kumkoromea mtoto. Yaani kanikatisha tamaa nikasema basi waendelee na maisha yao. Lengo langu ni kumjenga mtoto kielimu kipindi hichi nina uwezo lakini umimwambia hivyo anadai ukimchukua najiua
pole kwa masaibu yako , lkn huoni kwamba ungemuoa huyu mama wa mwanao angekupunguzia hizi karaha?
manake wewe ni iko ivi ama ulikosea kutafuta mtu sahihi ama ulikurupuka kuzaa lkn kama kakuzalia mtoto damu yako inatosha kusahau kila kitu na muanze kuyajenga upya kuliko kuwa mbinafsi kwa kuwaza yakupendezayo ukasahau mtoto wako ambaye yeye ni innocent sana wala hausiki na hilo saga lenu
 
Compatibility - exist/occur together without problems or conflict, so the opposite is incompatibility, that means their life challenges cause problems/conflicts to their relationship instead solving their problems/conflicts!
 
Viol ivi unajua kuwa kuna akina baba wanatelekezaga watoto kabisa na kuwaacha na mama?
tena akiwa na iman kwamba sitaki tena kuwa karibu na hawa watu?

Wapo kabisa hata mtaani kwetu,baba anawaachia watoto mama jambo lolote asihusishwe,ila jamii kama hizo zipo vijijini,baba wa mjini mbona mjanja na akizingua itakula kwake,vijijini wanawake hawajui majukumu ya mme wakiolewa kama wapo jela,mwanamke wa mjini hawezi kuachiwa watoto itakula kwako
 
Last edited by a moderator:
hivi hekimamali, huo ugumu wa maisha yeye tu ndo anaokumbana nao?na je nani antegemewa aje awe msaada kwa watoto wake/familia yake/ivi anaporudi kuomba msamaha wewe kama mama ama mtoto ulotelekezwa utasamehe kweli? nimejikuta namkumbuka Kongosho na King'asti kwenye hii hoja
dada gfsonwin maisha magumu huchangia kwa mtu ambaye uvumilivu hana unakuta mtu pesa shida,ajira ndo hivyo inapiga chenga ,kodi unadaiwa na familia ndo hivyo inakutegemea wewe sasa hali kama hii familia inashinda njaa mtu anaona asepe bila kujali hali aliyoiacha na vijana wengi hufanya hivi wakiwa na matumaini kuwa ndugu au wazazi wa mwanamke kwa lolote ile watatoa msaada
 
Last edited by a moderator:
Wala usiwaze!
Mara nyingi maswali magumu majibu yake ni mafupi sana japo sio rahisi kuyaelewa bila kufafanuliwa. Sababu ni:

Inatokea hivyo kwa sababu ya incompatibility ya changamoto za maisha ya mume na mke!

sasa kama mko incompatible ina maana umekuja mkulijua hilo baada ya kuwa na watoto 3,4,5,6,7,8,
kwann usingeiona iyo kabla ya kuzaa? na je hiyo compatibility haiwez kutengenezwa mtu ukishajua ilo ndo tatizo?

manake hata kwenye kemia muda mwingine unatafuta njia ya ku optimize ili upate farmula kamili
 
mweeeh!! iyo like nimekupa kwasabb tu umetoa maoni yako ila kwakweli umekuwa mkali sana teh teh teh
mie nasema ivi huyu baba anaye kwapuliwa akili yeye anakuwa amempa nani izo akili amshkie? ivi huwa mchepuko unaweza kununua akili ya mtu kwa kiasi hicho? mie nadhani ni utash wao wa ndani kwakweli
Nakuambia usicheze na nguvu ya Limbwata dada yangu maana mwanzo ni mzuri ila baada ya kukolezewa madawa huyo siyo binadamu tena ila ni nusu pepo, sasa kama mbaba ameshageuka pepo mtu, ataweza kuishi na binadamu.... Nina hasira sana maana kama siyo mipango ya mungu na uvumilivu wa mama yangu labla ningekuwa teja au chokora huku mdingi anakula vya laana. Biblia inasema "Enyi wanawake waombeeni waume zenu" Kuna kitu mungu aligundua hadi kuweka hili agizo.... Ila kwa niliyoyaona tangu nakua, baadhi ya wanaume hawakustaili kuuona utukufu wa binadamu.. real bora wangeumbwa kuku ili warukie kila uchapo.
 
ivi ivyo vitu vitamu vinaharibu akili sio??
Sasa kwann unaporudi kuja kutafuta huruma/msaada usiende kwa huyo anokupa vitu vitamu?

unajuwa Mimi naamini mapenzi ya dhati yapo kwa mwanamke mmoja tu yule ambae ulianza nae mkapata na familia.ukifanya mambo ya ajabu huko nje ukirudi asilimia nyingi atakukubali tu na kuendelea na maisha. Kuhusu suala la vitu vitamu kuharibu akili ama la ungekuwa mwanaume ungenielewa gfsonwin.
 
dada gfsonwin maisha magumu huchangia kwa mtu ambaye uvumilivu hana unakuta mtu pesa shida,ajira ndo hivyo inapiga chenga ,kodi unadaiwa na familia ndo hivyo inakutegemea wewe sasa hali kama hii familia inashinda njaa mtu anaona asepe bila kujali hali aliyoiacha na vijana wengi hufanya hivi wakiwa na matumaini kuwa ndugu au wazazi wa mwanamke kwa lolote ile watatoa msaada
ivi mdogo mdogo hawa unaowaacha nyuma wao ni vyuma? Kwamba hizi shida hazitawagusa?
 
pole kwa masaibu yako , lkn huoni kwamba ungemuoa huyu mama wa mwanao angekupunguzia hizi karaha?
manake wewe ni iko ivi ama ulikosea kutafuta mtu sahihi ama ulikurupuka kuzaa lkn kama kakuzalia mtoto damu yako inatosha kusahau kila kitu na muanze kuyajenga upya kuliko kuwa mbinafsi kwa kuwaza yakupendezayo ukasahau mtoto wako ambaye yeye ni innocent sana wala hausiki na hilo saga lenu

Unaambiwa ni bora ukakosea kujenga nyumba kuliko mke. Hii ni story nyingine ambayo inahitaji muda wake kuijadili. Lakini kwa kifupi niliishi nae na ninajua kuipenda familia yangu lakini mambo yake yalinishinda hasa hawa wadada wa siku ambao wanapenda ndoa lakini majukumu ya ndoa hawayawezi ni shida tupu. Wacha waishi tu maana nishaanza kusahau ila roho inaniuma hasa yule mtoto. Maana mama mtu hana future hata kidogo
 
unajuwa Mimi naamini mapenzi ya dhati yapo kwa mwanamke mmoja tu yule ambae ulianza nae mkapata na familia.ukifanya mambo ya ajabu huko nje ukirudi asilimia nyingi atakukubali tu na kuendelea na maisha. Kuhusu suala la vitu vitamu kuharibu akili ama la ungekuwa mwanaume ungenielewa gfsonwin.
mmh mie nisiseme sana kuhusu ilo la vitamu kuharibu akili ila nije kwenye kuhurumiwa, ivi kweli unataka huruma kwa mtu uliyemtenda?
 
Chanzo kiubwa cha wakina baba kutelekeza familia ni hao hao wanawake. Kwani anapotelekeza sehemu moja ujue kuna sehemu nyingine anahudumia.
 
Unaambiwa ni bora ukakosea kujenga nyumba kuliko mke. Hii ni story nyingine ambayo inahitaji muda wake kuijadili. Lakini kwa kifupi niliishi nae na ninajua kuipenda familia yangu lakini mambo yake yalinishinda hasa hawa wadada wa siku ambao wanapenda ndoa lakini majukumu ya ndoa hawayawezi ni shida tupu. Wacha waishi tu maana nishaanza kusahau ila roho inaniuma hasa yule mtoto. Maana mama mtu hana future hata kidogo
ivi wewe una muadhibu mwanao kwa kosa la mama yake?
imagine akija kukosa bright future utajilaumu kwa kiasi gani?
ivi umewaza waweza kumkuta siku mwano uliyempenda ni msukuma mikokoteni njian (sina maana nawadharau) afu unamuona wa rafiki yako ni afisa fulan ana maisha mazuri na wewe ulikuwa na uwezo wa kumpa maisha mazuri ili awe na future nzuri kama huyo wa rafiki yako utajiskiaje?

acha kuwa mcheleweshaj wa neema zamwanao kuna wazazi nenda kwa kufuata taratibu chukua mwanao mlee vizuri aje ajifae maishani.
 
Chanzo kiubwa cha wakina baba kutelekeza familia ni hao hao wanawake. Kwani anapotelekeza sehemu moja ujue kuna sehemu nyingine anahudumia.

sawa kunapo anapohudumia lkn je hivi akili inakuwa imeshikiliwa ama?
 
Hakuna dhambi wala laana kuacha kuwasaidia watu kama hao ...ila wao huwa wanapata laana kwa waliyoyafanya ndo maana huwa wanarudi na hali MBAYA
 
Back
Top Bottom