...unajua mpaka watu wanaamua kuachana kaa ufahamukuwa wamejitahidi kila wawezavyo ila imeshindikana. Kuna sababu nyingi sana zinazopelekea haya, moja ni changamoto za maisha, pia mda mwingine ni pressure toka kwa wazazi. Utakuta binti kajifungua na mshkaji amemchukua wanaishi wote ila bado wazazi wana-force wafunge ndoa bila kujua hayo ni mambo yao binafsi na ni vema waachwe waamue wenyewe. Sasa kinachotokea ni wazazi kutompa raha mwanaume, unatoka kwenye miangaiko unarudi home mwenzako analeta topics za ndoa hadi unachoka, ndo unakuwa wimbo wa taifa. Sasa kinachokuja kutokea ni mwanaume kuchoka sabu unajaribu kumweleza mwenzako ila hakuelewi so unaamua mpeane time kila mtu afanye mambo yake binti anarudi kwake na wewe unaendelea na maisha. Mambo haya nimeyaona na yamemtokea mtu wangu wa karibu sana ila naweza sema kwa asilimia kubwa wazazi walipoingilia walisababisha watu watengane. Wadada mnaweza kuja kunishambulia na kusema kwani angemuoa tu hivyo hivyo si wangeishi tu na kupanga mambo yao slowly? Na mimi nauliza mbona hampendi kutupa nafasi, mbn mnapenda kutuburuza na kufanya mambo haraka kwa speed muipendayo. Maana mara nyingi ndoa za dizain hii hazidumu. Hivyo dada gfsonwin, hatuwatelekezaji wake zetu wala watoto wetu wazuri ila mda mwingine mambo haya yakitokea ni vigumu sana kueleza na kueleweka.