Wana MMU
herini ya mei mosi.........
Leo naomba nije na hoja hapa tuijadili sote kuhusu akina baba...........
mie nawauliza hivi kwanini wanapenda kuwachumisha wengine dhambi? Yaani akina baba kuwachumisha watoto wao dhambi hawaoni tabu. Hivi mnapotelekezaga wake zenu an watoto ama wazazi wenzenu na watoto afu mama ana hustle na watoto hadi wanatoboa huwaga nini kinawapata kwenye akili zenu?
mwishoni sasa watoto wakitoboa mnaaza kulalamika, kuacha malaana ya ajabu ajabu, mnalazimisha kusaidiwa mbaya zaid huwaga hamjui mbele mnachokaga vibaya mkirudi masukari ndo mnayo achilia mbali, magauti na ma kansa.
Kinachowashika akili ni kitu gani? na kwann kwenu nyie moyo wa kusamehe basi hamnaga lakin ikitokea mnahitaj msaada mnataka msamehewe??
Yaani nimekuwa nikichunguza familia nyingi zilitolekezwa na akina baba yaani wengi niliowaona huwaga wanarudi wakiwa na hali mbaya sasa najiuliza ivi walipokuwa wanaaacha hizi familia walikuywa wanawaza nini?
Hivi hamuoni kwamba mnawachumisha dhambi wake/wazazi wenzenu na watoto wenu?? manake wasipokuhudumia ni dhambi afu akikuhudumia kwa shingo upande na penyewe tena ni dhambi, yaani mnatesa wenzenu bila sababu kabisa.
sipendi kutoa mifano ya watu mnaowajua manake sitak kuhukumu lkn nataka nijue kwaninin huwa mnafanya haya kama akina baba/wanaume
Sehemu kubwa,Tatizo ni nyie nyie wanawake.
Unajua jamaa anamke na watoto.unamteka.
Unamfanya asahau familia yake.
Unamfanya achukie familia yake.
Unamuahidi mazuri.
KUMBE UNACHOTAKA NI PESA ZAKE,
AU NGUVU ZAKE.
unamchuna weeeee/unamchosha weeeee.
Akitepweta unamtimua.
Aende wapi?
Hakujua kama anakosea pengine!
Hakujua watoto wanakula nini?
Ila hakua yeye MOYO WAKE ULIDANGANYIKA.
anarudi kwa mkewe kwa watotowe.
Na ndipo mahali sahihi!
Aende wapi?
Wanawake nyie mna jukumu la kuwachunga wanaume.
Na wanaume wanajukumu la kuwalea(mahabatically)
Si jambo zuri. Ila
Mapungufu kaumbiwa binadamu.
Muhimu kusameheana.
Kuelezana,kuelewana.
Dunia Maiuto/dunia njia.
Ya mini ufe umenuna!
Samehe bure,mpokee mwenzio.
Yaliyo pita si ndwele,mgange yawajiayo mbele.na maisha yaendelee.
Kitu kizuri zaidi kwa mtoto kulelewa na baba na mama kwa pamoja.
Ila wanaume tubadilike,tuinamishe macho chini.
Ili familia zetu ziwe na furaha,amani,upendo na utulivu.
KATIKA MUNGU YOTE YANAWEZEKANA.