Wanaume tupeni majibu sahihi kwanini mnapenda kuwachumisha wengine dhambi?

Wanaume tupeni majibu sahihi kwanini mnapenda kuwachumisha wengine dhambi?

dada mkubwa hata kama kosa ni kubwa kiasi cha kutosameheka sidhani kama ni sahihi kuacha familia. Mimi huwa nasema hata iweje sitaruhusu mwanangu aumie kwa sababu ya mwanamke. Nifanya kila kilicho katika uwezo wangu kuhakikisha wanangu wanakuwa katika hali nzuri. Na hii wapo wanaume wengi tu wanafanya.
hongera sana kama wewe u baba bora
mie namuombea sana mume wangu ili asibadilike kutoka apa alipo as ni mume bora sanaaaa
ila hawa wanaume baadhi wanachumisha dhambi wenzao hasa watoto na wake zao
 
Ni dhambi kubwa sana ukishindwa kumfanyia wema ndugu wa damu kuanzia mume/mke,dada/kaka,mama/baba,wifi/shemegi,bamkwe/mamkwe ,shangazi/mjomba n mtoto, hata km awe amekuudhi kiasi gn,basi ww mfanyie wema n ihsani,mwisho mwenyewe ataona aibu kwa alokutendea baada ya ww kumfanyia wema

dah lakin muda mwingine inabidi watu wafundishwe hata kama ni kwa njia ngumu
ivi mtu amekutelekeza for 16 yrs anakuacha na matatizo, dhiki, shida, na mateso adi unakatiwa majina mtaan mara mama shida huyo, mara mama mtalikiwa, mara sijui mama makusanya afu anakuja kurudi wewe ukiwa ndo umepata neema na wanao mnapojionea mlepo raha ivi kweli huo moyo wa wema kiasi hiko utakuwepo?
 
Mkuu Manuu nasoma baadhi ya post juu ya wadau naona wanabase juu ya hisia flani ama wanalibeba kihisia tuu. Maana mtu hawezi kurupuka na kufanya huo upuuzi bila kuwa na sababu, wanawake wamekuwa ni zaidi sumu sasa katika ndoa zilizo nyingi. Mimi nasem mpaka mwanaume afanye ivyo kuna side B yenye iffect sana imagne amegombana na mwanamke then mwanamke anamropokea we nawe mwanaume unajiaminishaje kwanza flani ni mwanao?. Japo swali kama hilo atalisema akiwa na hasira je unafikir kwa mwanaume linachukua nafasi gan? Akikusanya na tabia nyingine za kutokuwa mwaminifu hapo nyuma labda kufaham mwenzake anachepuka unafikiri nn kinaenda kutokea? Jaman kila kitu kinatokea kukiwa na sababu za msingi za kukifanya kitokee.

sawa kabisa ulinikimbia kisa nina tabia mbaya na matusi nk.............umeniachia watoto nikalea ata kama papo mahali niliuza mwili niwalee wee ilo halikuhusu. Haya leo hii unaporudi nyumban baada ya kututelekeza ina maana zile tabia zangu mbaya hazipo? ama zimefutika? kinachokurudisha wewe nyumban ni kitu gani hasa? mbaya zaid unarudi ukiwa tyari afya mgogoro, na tena ukiwa na bahati nzuri ukute una klinik vinginevyo nakuja kukukutia kitanda cha hosp ivi wee ni mzima kweli ama?
 
ilo limbwata muda mwingine tunalisingizia,
ivi wanawake wao hawapewagi ilo limbwata?
Yapo pande zote.... Wewe hujawahi shughudia mwanamke ananyanyaswa na mmewe hadi majirani mnamwonea huruma ila ukidhubutu kumshauri anaenda kukuistaki kwa mmewe, hivi unafikiri huyu atakuwa na akili zake au zakutegeshewa??? Hope unaamini upo uchawi japo hauwezi kukudhuru kwa kuwa tu umeamua kuwa moto au baridi na siyo vuguvugu.
 
mizani huwa inalinganishwa ndo unakuwa na kipimo sahihi,,, mwanamke kaumbwa kuongea -(kuchonga sana), kitu ambacho hamkubali ni kwamba huwa mnakuwa chanzo cha rabsha, sasa sbb mnachonga sana, ndio mnakuwa wa kwanza kwenda kuyasema huko nje, ilhali wewe ndo mtuhumiwa, hakuna mwanaume anaekimbia bila sababu, wanawake ndo waanzilishi wa matukio, na ndio wa kwanza kuwahi polisi.
 
jamani situnataka haki sawa kwa kila jambo ? sasa tukiachwa na wenza wetu na tukajitunza na kutunza watoto wetu bila msaada wao kunatatizo gani?
 
gfsonwin kwanza hongera kwa kulileta hili umegusa hisia za wengi ambao wamepitia katika kadhia hii.
Kuna msemo wa kipya kinyemi umewaangusha wanaume wengi toka baba zetu mpaka sisi vijana kuhusu limbwata kwangu mimi siipi nafasi kubwa ila ninachojua MBUNYE au PAPUCHI ukiiwekea sikio ukasikilizia ndo matokeo yake unatelekeza familia na michepuko inavyojua kujituma na ku care mh!unakuta umeenda mkoani anakupigia simu baby umekula?hili swali huwa linanikera hivi kweli mimi mtu mzima na timamu niwe sijala mpaka unikumbushe?nasema wizi mtupu unajifanya kunipenda kuliko bimkubwa wangu.
 
mmmh akya nnai tena hawa wababa wanajuaga kuchumisha dhambi wenzao
imagine eti anakuacha unatesema afu mwishon anakuijia eti kutafuta huruma yako

na ukimkataa unaambiwa una roho mbaya na hapo hapo wakiwa wenyewe wanajisifu ati wanaume huwa hawarudii matapishi kweli usilolijua ni kama usiku wa kiza.
 
unajua hata kama ni upendo lkn kuna muda inabidi basi akili ikuamulie kwa busara
ivi brodah mtu unapotelekeza familia afu baada ya muda unarudi tena humo humo kuomba msaada tena kwa lazima unakuwa hukumbuki ama?
je usiposaidiwa huwa unalaumu nini?

Yaani umeogea kitu ambacho kimetokea sasa hivi hapa ofisini, kuna mzee mmoja kaja kuomba msaada kwa mwanae, huyo mwanae tunafanya naye kazi aliwatelekeza miaka ya 70 sasa kaisha , hana kitu , kuumwa ndiyo kama sala kwake na huyu kijana hapa ndiyo kasoma na anapata mshahara mzuri,baba ndiyo huyo, kijana wa watu hana budi kumuhudumia , ingawa yeye aliwatelekeza kiasi ambacho hakielezeki.
NB: Ukifanyacho leo kinarudi kesho kama malipizo au malipo yako.
 
tuache kupayuka payuka hapa, hivi huyu baba anaetelekeza familia, anaitelekeza na kuishi peke yake? tumeshajiuliza huwa anaenda wapi?
wengi huanzisha familia nyingine na kuzihudumia, mbona hatujadili uzuri wa upande huu? tuache kuwa bias na tuone both positive and negative aspects za hawa wababa.
 
ubinafsi na tamaa
wababa kukimbia majukumu na kuona kwamba kwa wakati huo hawawezi kushiriki kwa lolote.
 
tuache kupayuka payuka hapa, hivi huyu baba anaetelekeza familia, anaitelekeza na kuishi peke yake? tumeshajiuliza huwa anaenda wapi?
wengi huanzisha familia nyingine na kuzihudumia, mbona hatujadili uzuri wa upande huu? tuache kuwa bias na tuone both positive and negative aspects za hawa wababa.

umeshajiuliza familia ile iliyoachwa inaishije?
 
Bestito nashukuru kwa mada nzuri hii ya kuwakumbusha wajibu wanaume wazembe ni kama umegusa mboni ya jicho langu mm mwenyewe huwaga wananishangaza sana hawa wababa/wanaume ambao wanatelekeza familia yao na kufanya mambo ya kihuni sana

wanaona fahari sana kufanya uhuni kuliko kuwalea watooto wao hawako radhi kuwashughulikia wale wtoto waliowaleta duniani wao wanatelekeza hawajui kuwa ipo siku ambayo hiyo familia mungu ataionekania na kuwa bora baadaye

na wanapopata shida wanarudi kwa familia yao sasa hapo kama ndo mm asinijue kila mtu aishi kwa mpango wake mwenyewe na wala asinifuate tena kwani ni kwazo kwakngu pia
 
mizani huwa inalinganishwa ndo unakuwa na kipimo sahihi,,, mwanamke kaumbwa kuongea -(kuchonga sana), kitu ambacho hamkubali ni kwamba huwa mnakuwa chanzo cha rabsha, sasa sbb mnachonga sana, ndio mnakuwa wa kwanza kwenda kuyasema huko nje, ilhali wewe ndo mtuhumiwa, hakuna mwanaume anaekimbia bila sababu, wanawake ndo waanzilishi wa matukio, na ndio wa kwanza kuwahi polisi.
sawa ni kelele za mwanamke zimekutoa ndani
sasa je unaporudi kuja kutaka huruma/msaada wake hizo kelele anakuwa kasheziacha ama?
 
jamani situnataka haki sawa kwa kila jambo ? sasa tukiachwa na wenza wetu na tukajitunza na kutunza watoto wetu bila msaada wao kunatatizo gani?
hakuna tatizo kabisa wala mie ilo sio tatizo kwa mwanamke yyte yule
tatizo ni je kwann hawa wanaoacha /telekeza familia hurudi kuja kutaka msaada wa hawa aliowatekeza?
kama umeamua kusepa si usepe for good??
saa kinachokurudisha ukiwa na hali mbaya, kisukari mara mapresha mara sijui magaut mata ma athritis ni kitu gani?
jambo zuri ni ivi ukijua kutelekeza basi usirudi tena nyuma
 
na ukimkataa unaambiwa una roho mbaya na hapo hapo wakiwa wenyewe wanajisifu ati wanaume huwa hawarudii matapishi kweli usilolijua ni kama usiku wa kiza.

ishu ni kwamba ukijua kuondoka ondoka milele usirudi nyuma
kwann kurudi nyuma afu unakuta mwingine akigundua aliye mwacha ana mapoozeo anaaza kumsakama na kumpiga wakati yy huko anaish na mtu ivi sijui hawa wanaume wakoje.

kuna mama mmoja nilikuwa naongea nae akanisimulia mkasa wa maisha yake yaani alitelekezwa afu bado mume akawa na wivu nae bado jaman mie niliishia kushangaa tu..........sijui huyu baba alikuwa na akili gani
 
Bestito nashukuru kwa mada nzuri hii ya kuwakumbusha wajibu wanaume wazembe ni kama umegusa mboni ya jicho langu mm mwenyewe huwaga wananishangaza sana hawa wababa/wanaume ambao wanatelekeza familia yao na kufanya mambo ya kihuni sana

wanaona fahari sana kufanya uhuni kuliko kuwalea watooto wao hawako radhi kuwashughulikia wale wtoto waliowaleta duniani wao wanatelekeza hawajui kuwa ipo siku ambayo hiyo familia mungu ataionekania na kuwa bora baadaye

na wanapopata shida wanarudi kwa familia yao sasa hapo kama ndo mm asinijue kila mtu aishi kwa mpango wake mwenyewe na wala asinifuate tena kwani ni kwazo kwakngu pia

yaani swala ni akiondoka aondoke milele na asirudi tena
 
tuache kupayuka payuka hapa, hivi huyu baba anaetelekeza familia, anaitelekeza na kuishi peke yake? tumeshajiuliza huwa anaenda wapi?
wengi huanzisha familia nyingine na kuzihudumia, mbona hatujadili uzuri wa upande huu? tuache kuwa bias na tuone both positive and negative aspects za hawa wababa.

na mie ugomvi wangu hauko kwenye iyop familia nyingine iliyo anzishwa.
mie nasema kwann hurudi tena kwa bi mkubwa kutafuta huruma na msaada??
si ukae huko huko ulikoanzisha familia ufie huko huko?
kurudi ukiwa mgonjwa na hali mbaya unamletea nani mzoga??
 
tatizo ni kwamba anaye achwa hujikaza kisabuni hadi wanae watoboe afu mwoshon anarudisha kichwa nyumban eti amerudi kuja kupata msaada....
gfsonwin

katika dunia kuna mambo mengi sana ya kuumiza japo yapo mazuri pia

usipotoa msaada inakuwa lawama hadi ukoo kama vile wanajua ulifikaje hapo ulipo........labda ikitokea kwa huruma ya mtu na mtu basi inabidi kusaidia kwa shingo upande maana wakati mwingine kuna kale ka damu kakuchangia kanakusukuma.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom