Gazaniga
JF-Expert Member
- Apr 12, 2015
- 1,051
- 360
Ha ha haaaa!! umenikumbusha tulikuwa tunaenda moshi mjini na brother wangu sasa tulikuwa tuko watatu, mimi ,brother pamoja na mke wake, ila mke wake alikuwa amekaa siti ya nyuma alafu amenyamazaaaa kimya muda mrefu sisi ndio tunapiga story!
tukasimamishwa na trafiki wa kike pale KIA kwakweli alikuwa mzuri yule dada masikini nadhani ndio alikuwa anaanza kazi maana hata kuuliza maswali alikuwa anaogopa! alipoturuhusu tuondoke tukaanza kumsifia yule dada,
ghafla broo akasema 'NAKWAMBIA MOSHI KUNA WATOTO ASIKWAMBIE MTU" ghafla tukashtulia na sauti ya shemeji ikisema "NDIO MAANA MLIKUWA MNANILAZIMISHA MNISHUSHE KWETU NISALIMIE NA NYIE MUENDE KWENYE MIHANGAIKO,
KUMBE NDIO MIPANGO YENU KUJA HUKU MOSHI LEO KWA WATOTO" kimya kikatawala kidogo ila brother alirudi na topic mpya tena kwa ukali, "sasa unachokasirika ni nini!!? si nikweli kila kona MOSHI utaona watoto wanaenda shule!!? kila kona hebu ona wale kule eenhh ona wee ona tu mwenyewe kila mahali ni watoto wako busy na kwenda shule"
Mkuu hukuchukua namba ya huyo traffic unirushie?