Wanaume, unatumia gharama gani ku-shave kwa mwezi?

Wanaume, unatumia gharama gani ku-shave kwa mwezi?

Mwanaume kunyoa kwa elfu 12 kwa mwezi huko ni kujiremba fata ushauri anaokupa jamaa
Haya ni kujiremba basi ila niwajuze tu asili ya mwanaume sio kutengeneza magomvi yasiyo na misingi tumieni hekima kutoa maoni kama uzi unavyoeleza mtakuja kutoa maoni mabovu kwa popobawa alafu mshindwe kusimulia yatakayojiri.
 
Habari wakuu,

Kama heading inavyoeleza hapo juu, nataka kufanya research binafsi ili nione kama kuna kipya katika matumizi na gharama zetu katika maisha yetu ya kila siku, Nikisema kipya ni kujua kama kuna uwezekano wa watu wanaotumia gharama sana, gharama za kawaida (kati) au kuna za chini kabisa n.k

Nitaanza na mimi, binafsi napenda sana kuwa smart all the time hivyo napenda kuwa on point kila mara so nimekuwa mtu wa kuchagua sana vinyozi na ubaya ninapoishi hamna saloon zile za high level (Barber Shop) hivyo kutokana na hilo huwa kuna kinyozi wangu natokaga mitaa mitatu kumfuata kwaajili ya kazi hiyo, Kutokana na suala hilo la umbali imebidi nijipe ratiba ya kunyoa na full head mara mbili tu kwa mwezi ambapo huwa nalipia 10,000 huku beards na ndevu nikiwa nashave kila baada ya siku 5 hapahapa mtaani ambapo nalipia Tsh. 500 tu.

Kwa hesabu hiyo hapo juu mimi hujikuta natumia Tsh.11,500 - 12,000 kwaajili ya kushave kila mwezi.

Wewe je?
3,000 zinanitosha mwezi mzima,Wembe wa Laser II wenye nyembe 5,nanyoa ndevu mara 3 kwa wiki,nywele mara 2 kwa wiki....
 
3,000 zinanitosha mwezi mzima,Wembe wa Laser II wenye nyembe 5,nanyoa ndevu mara 3 kwa wiki,nywele mara 2 kwa wiki....
mkuu ndevu nikinyoa na nyembe naona zinaleta mapele
 
Haya ni kujiremba basi ila niwajuze tu asili ya mwanaume sio kutengeneza magomvi yasiyo na misingi tumieni hekima kutoa maoni kama uzi unavyoeleza mtakuja kutoa maoni mabovu kwa popobawa alafu mshindwe kusimulia yatakayojiri.
Yani we uwe popo bawa? Popo bawa gani ananyoa kwa tsh 12,000/=? Popo bawa ni sisi tunaonyoa kwa buku kwahiyo kuwa makini
 
Back
Top Bottom