Wanaume wa JF muwe mnatuma nauli mkitaka kuonana na warembo mwenzenu kanitia hasara!

Wanaume wa JF muwe mnatuma nauli mkitaka kuonana na warembo mwenzenu kanitia hasara!

Kwani wanajf waingiao dodoma lazima wajiandikishe kwenye daftari lako? Au mi ndio sijaelewa[emoji1][emoji1][emoji1]
Huyu pesa yako tu...

Its cold out there? Basi kwa demiss ni joto muda wote ukiwa dom
 
Eti wanasema huwa wanafurahia comment zangu wanifananishe na mimi
Maskini wangejua mweeee D mwenyewe kasichana kadogo tu hakana mbele wala nyumaa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Saivi wataogopa mambo ya kufunguliana uzi nani anayataka
 
Vitu vingine ni kuvichukulia simple, pengine anayeongea yupo mbali na tabia hizo, ameamua tu kuchemsha vichwa vya watu.
Kuna picha naijenga kuhusu huyu mleta maada inaweza kuwa inaakisi jinsi alivyo kwa asilimia kubwa
1. Yawezekana anajiuza
2. Anaishi kwa kudanga
Haiwezekani mtu utoke hombolo umfate mtu mjini kwa gharama hiyo halafu utegemee urudishiwe, Ina maana moja kwa moja ulitegemea zaidi ya hiyo kwake.
Na kingine mwanamke mwenye staha asingeleta upuuzi huo hapa lazma angeona haya, sisi wanaume tunajuana na nadhani huyo jamaa hakuwa na nia ya kukugegeda kwa vyovyote vile maana unaonekana wewe ni mweupe na mrahisi Sana.

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
 
Mzee mama mjini hpa huyo alifika hpo akakuchora kakuona haulipi..kasepa
 
Kuna mtu anajiquote mwenyewe humu[emoji23][emoji23]hatari sana[emoji23][emoji23]anatumia ID tatu ndani ya uzi huu huu mmoja[emoji57][emoji57]
Na bila shaka yeye ndie mlengwa kwenye hii thread. Anatumia uongo wake wa darasa la saba,.mara ooh naishi nje, mara nina pesa[emoji16][emoji28]kumbe likapukuu la kufa mtu!

Sasa bisha na hapa[emoji41](unajijua)
Nasema hivi....bisha na saivi nikuumbue[emoji57][emoji57][emoji57]

Hahahahahahahah uwiiii nako.....
 
Pale mdangaji ANAPOKOPWA! Pole sana kama nakuona vile hasira zako za kutoboa kipochi chako.

Bora tu niseme ukweli kuliko kudanganyanaa.

Kwanini nimesema mwanaume yeyote anaye hitaji kuonana na mimi lazima atume nauli.


MKASA
Kuna mkaka mmoja wa Jf ana I'd yake inaanzia kama ya kike alinifata pm anahitaji kuonana na mimi.
Mimi wala sikuwa na shobo naye akaniganda kama rubaa nakwambia ooh mara natoka Canada nitashuka kenyata airport mara sjui wapi nakuja Dodoma kikazi lazima nikuone Demiss.

Mimi kusikia hivyo nikaona huyu mtu wa maana bwanaa weee kumbe hamsini zangu zimefika chiii

Huyu mkaka baada ya kufika Dom tukawasiliana akasema niende town alafu si mnajua mm naishi huku Hombolo jamani.

Eeeh nikachukua bodaboda mpaka mjini gharama elf 20 nikalipa.
Kichwani nilivaa wigi limeshachambuka na upepo limekuwa kama vuzi la Escober.
Nikapitia saloon kwa Jesca mcharuko akanipaka make up mimi akanichana na wigi kwa sh elf 5. Jumla nimetumia elf 25 mpaka hapo.

Nikakaa hapo saloon nasubiria kuonana na Mwanajf asije akanikimbia nimeshajipodoa na kuupara mtoto nanukia marashi weee balaaa.

Wewe si akaingiza sababu kibaoo jaman nilikereka hapo alisema atarudisha nauli yangu ikabidi niende kulala kwenye geto la Jesca Maili mbili.

Kesho nikaamka nikaenda nane nane nikapanda Super baraka mpaka hombolo nikiwa na mawazo debee.
Jaman nilipata hasara yani hela yangu bado inaniuma mpaka leo.
Alafu huyo member alisema atanirudishia lakini wapi mpaka leo sijaona muamala ukisoma kiufupi hela yangu inaniuma yani ningenunua mchele si ningepata hata kilo kumi.

Kuanzia leo naomba mjue mimi naishi HOMBOLO village.

Mchanganuo wa nauli
Hombolo-Town Elfu 40,000 kwenda na kurudi.
Saloon - Elf10,000

Kama huna nauli basi uwe na gari ya kunifata nilipo sitaki usumbufu.

Onyo:
Sijalazimisha kuonana na mtu ila mkae mkijua habari ndo hiyooo.
Alafu mm sina kifua ukinifanyia kitu lazima niseme saivi kiufupi siwezi kuweka mambo rohoni nisije kufa na pressure.

Location: Ihumwa Machimboni.
 
Back
Top Bottom