afrodenzi
Platinum Member
- Nov 1, 2010
- 18,150
- 9,255
Hahahahaaa mi mzima bukheri wa afya na hivi mvua zimeanza basi kilimo mtindo mmoja,
Ama baada ya salam lengo na dhumuni ni kutaka kukujulia hali na pia kukwambia kwamba ulimisiwa sana nami......
M'Jr
Nashukuru kusikia kilimo na mvua kwa wingi....
Je ulipata ile barua yangu niliyotuma tarahe 3.2.1985?
niliiweka kwenye bahasha ya bluu na nyekundu?
Dhumuni la barua hii na ile ni kuku julisha jinsi nilivyo kukumbuka
na ninasubiria sana kwa hamu kurudi nyumbani tukajifiche tena katanini..
karatasi limeisha, wino umegoma kilochobakia ni mapigo yangu ya moyo.
sidhani kama yataendelea kupiga kama sintakuona muda wa karibuni...
PS. hakikisha unachoma barua hii baada ya kusoma
akupendae kwa dhati
Afrodenzi
PS......moyo wangu utajawa nafuraha ntakapo pata majibu yako...








