Wanaume wa ki-Tanzania wengi wao wanajua majukumu yao nyumbani

Wanaume wa ki-Tanzania wengi wao wanajua majukumu yao nyumbani

Mmh tunawashukuru kwa wale ambao familia zao ndo priority zao za kwanza, ila kiukweli sio wote. Naona lundo la wanaume wabinafsi linavyozidi kushamiri. Naziona familia nyingi sana ambazo mama ndo amegeuka baba kimajukumu kwa sababu baba ameamua kuinvest kwa vimada na bar. Mungu anawaona


hata sina la kusema ! nisije haribu uzi wa watu!
 
Wa hivyo wapo tunawaona ila huwa wanasikitisha sana,
Yaan mtu anasubiria mafao ndiyo akajenge hii ni aibu sana kwa mwanaume 45years upo nyumba ya kupanga!
Kama mtu anaishi nyumba ya kupanga ila still anaitunza familia yake kadri ya uwezo wake, huyu anaweza kueleweka. Maybe maisha hayajawa smooth kwake kihivyo kwake au maybe kipato kikubwa anakitumia kwenye kuinvest kwenye elimu ya watoto wake na welfare nyingine, bado utegemezi wa wazazi, ndugu jamaa na marafiki.... Angalau he is responsible, inaeleweka japo ndo hivyo tena

Hapa tunamsemea mtu mwenye kipato lakini hajali familia. Nyumbani watoto hawapati lishe bora ila baba kajaza fridge kwa mchepuko. Nyumba inapokaa familia imechokaaa ila baba kashusha mjengo kwa kimada, kama sio kuweka heshima bar. Wababa wengine wanajijali tu wao mmh, watoto wanaishi maisha as if baba hayupo kabisa khaa. Aliyezishika fahamu za watu hawa, Mungu anawaona.
 
We angalia hata mada zao humu siku hizi, mara wafundishane namna ya kumchuna mwanamke, mwingine alisema wanawake tujiongeze tulipie mahari!!
Sijui ni malezi ndio tunakosea au shida ni nini!!!
Yani nashindwa kuelewa tunakosea wapi honestly. Idadi ya wanaume irresponsible inazidi kuenea jamani mmh
 
Afu mtu awe na mawazo kama haya asipendwe we ni mwanamke wa pekee sana aisee nimekupenda mara 366

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Kutokana na uzoefu wangu hapa duniani nimegundua kuwa wanaume wa ki-Tanzania wana jua majukumu yao. Wanahakikisha mambo ya nyumbani yametulia kabla hawajaanza kujifikiria wenyewe.

Si ajabu kumkuta mwanaume ana suruali moja au mbili tu lakini anajenga nyumba na watoto wanakwenda shule.

Nchi hizi za jirani zetu zenye kuiga uzungu mwingi, mwisho wa mwezini mwanaume anakwambia weka sehemu mchango wako wa budget mezani kabla hujaenda saloon. Nimeshuhudia mume akitembea na remote control kwenye brief case kisa mke hakuchangia LUKU.

Wanaume wengine wanaokaribiana na wanongo kwa kutunza wanawake ni wa Ghana. Hawa mshahara wako hutaukizwa unakwenda wapi lakini siku mkitoka usimtie aibu mbele ya rafiki zake eti umevaa dera la elfu tano.
Asanteee, nikweli kabisa, huwezi piga pamba za maana mke wako anashinda na kuzurula na madela, watoto wanavaaa mitumba grade ya mwisho, ni uenda wazimu wa kiwango cha juu.

Nini kweli, wanaume wengi wa kibongo hawataki familia zao zi-aibike, wanajitahidi.

"Do not compete with any one, do the best to become the best"
 
Ni hali ya maisha tu lakini nyumba ya kupanga siyo ya kukaa kwa muda mrefu mkuu. Ninakumbuka mshkaji wa karibu alifia na mama yake mwenye nyumba alikataza matanga ilibidi tulilie hospitali
Inatia aibu Sana basi tu!
 
Kama mtu anaishi nyumba ya kupanga ila still anaitunza familia yake kadri ya uwezo wake, huyu anaweza kueleweka. Maybe maisha hayajawa smooth kwake kihivyo kwake au maybe kipato kikubwa anakitumia kwenye kuinvest kwenye elimu ya watoto wake na welfare nyingine, bado utegemezi wa wazazi, ndugu jamaa na marafiki.... Angalau he is responsible

Hapa tunamsemea mtu mwenye kipato lakini hajali familia. Nyumbani watoto hawapati lishe bora ila baba kajaza fridge kwa mchepuko. Nyumba inapokaa familia imechokaaa ila baba kashusha mjengo kwa kimada, kama sio kuweka heshima bar. Watoto wanaishi maisha as if baba hayupo kabisa khaa. Aliyezishika fahamu za watu hawa, Mungu anawaona.
Na wa hivyo kwa maisha ya sasa ni mmoja mmoja sana.
 
Leo mmetutetea duh Mara ya kwanza nasikia JF hzo compliments
 
Kabisa tunateseka sana hata mi ua nikiangalia kibegi changu afu nilicheka Wife kujaza begi kubwa na kabati

Post sent using JamiiForums mobile app
 
SAFI SANA MKUU SKY ECLAT KWA KULIONA HILI.

UBARIKIWE SANA. NA WANAWAKE WENZIO WAELEWE PIA.
 
Mtoa mada sijui ana waume wangapi. Si kwa utafiti huo[emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom