Wanaume wa Kijaluo wakimbeba David Livingstone mwaka 1885 kumuonesha ziwa Victoria ili aweze kuligundua

Wanaume wa Kijaluo wakimbeba David Livingstone mwaka 1885 kumuonesha ziwa Victoria ili aweze kuligundua

John speke nae alikuwa wa kwanza kuona mlima Kilimanjaro 😂 sijui Niko sawa
 
Aneyoona kwanza ndio anagundua au anayepelekwa?
Na tulidanganywa sana kwamba mtu wa kwanza kuona Mlima Kilimanjaro ni mzungu fulani. Mbaya zaidi tukafundishwa hivyo mashuleni. Je, wachaga si watu?! Kuna haja ya kuandika upya historia yetu ya kweli na ya staha. Si hiyo ya kukejeliwa na kudharauliwa.
 
Livingstone hakufika ziwa Victoria na alifariki 1873 kule Chitembo mpakani mwa Zambia na Tanzania.Kuna ujumbe kiasi kwnye bandiko lako ingawa ni andiko ahistorical
Ni sahihi kabisa, hakuwahi kufika ziwa Nyanza. Hata milima inayoitwa kwa jina lake huku Nyanda za Juu Kusini Magharibi (milima ya Ukinga), iliyosambaa kuanzia mkoani Mbeya, Njombe hadi Ruvuma, hakuifikia. Aliiona kwa mbali akiwa nchini Malawi.

Tunawaenzi wazungu kijinga na kujidhalilisha sana, badala ya kuuenzi utamaduni wetu mzuri.
 
Aneyoona kwanza ndio anagundua au anayepelekwa?
That time Waafrika ilikuwa hawajaanza kuhesabiwa kama binadamu, definition ya enzi hizo ya black Africans was "animals very organized like human beings but slow in thinking".
Hapo walikuwa sahihi kabisa japo according to them back then mvumbuzi wa lake Victoria alikuwa ni John Hanning Speke.
 
Waarabu walikua wameisha fika na kuyaona yote hayo na ilikua tayari maziwa na milima na vinginevyo yalikua yanajulukana Zanzibar na ndipo hawa 'wavumbuzi' walikua wanapata habari zote za kuwepo hayo huko ndani kwenye bars la giza (dark continent).
Pia safari zao na Mandalizi yao ya vifaa, vyakula, wapagazi na kiongozi wa msafara viliandaliwa Zanzibar
Zanzibar ilikua tayari mbali kimaendeleo na mtandao wa kibiashara kwenda ndani mpaka Kongo.
Kitu ambacho Hawa wavumbuzi walikuja nacho kipya ni uchoraji wa ramani na kuandika maelezo kwa wanayo yavumbua au kuyaona wakiwa katika msafara.
Kwa hiyo uvumbuzi ni mjumuiko wa juhudi kutoka kwa wenyeji waafrika , waarabu na hao wazungu
 
Back
Top Bottom