Usiseme hivyo mkuu, halijakukuta tu. Kuna watu ni mastermind kwenye hili eneo la uchakataji.
Nina mshkaji wangu yumo humuhumu JF, kila wakati alikuwa anasema kuna ID flani anaipenda sana, nikadhani mwana kachanganyikiwa! Nikamuuliza anaipendaje ID bila kujua uhalisia wa 'bearer' wa hiyo ID kama ni KE kweli? Au kama ni mzuri kama anavyodhani? Akawa anajichekelesha.
Kimyakimya akazama PM. Akakuta mkuu kafunga PM. Akawa kwenye kila uzi ambao huyo bidada yupo ana-comment au ku-like. Wakazoeana. Kulekule kwenye nyuzi tena kiutani utani akawa anamuomba bidada afungue PM. Kuna siku bidada akakubali kuifungua, ila akampa sharti kwamba akimwambia tu upuuzi anaifunga tena.
Wakawa wanachatishana PM, jamaa kila akiomba namba bidada anachomoa. Baada kama ya mwezi hivi jamaa alikuwa anamchatisha kule PM na akaghairi kabisa kuomba namba. Siku isiyo na jina dada akamtumia jamaa namba (landline). Jamaa akawa anampigia kama kwa wiki 2 hivi mfululizo. Ghafla kuna siku jamaa akamuaga bidada, akamwambia kwamba hatompigia tena kwenye ile landline; kama bidada ameshindwa kumuamini kwa kipindi chote hicho basi ni afadhali wabaki marafiki wa JF tu, ila akamshukuru kwa kufahamiana nae walau kwa uchache (jamaa hakumaanisha, hii ilikuwa ni technic tu kwasababu jamaa aligundua kwamba bidada kashamzoea [emoji1]).
Khe! Dada upesiupesi akatuma namba yake ya simu ya mkononi na kumuomba mshkaji msamaha kwa kuwa stubborn. Nadhani kilichoendelea unakijua [emoji28].
Kuna watu wakiamua lao hakuna kinachoshindikana mkuu. Ulale salama [emoji23]
Sent using
Jamii Forums mobile app