Mokaze
JF-Expert Member
- Aug 3, 2018
- 14,370
- 14,929
Yani sina mpango wa kumgombanisha na nduguze kwaio hawawezi kujua
Mimi lengo langu ni utulivu tu sio kumbully hapana
Nampenda sana siwezi kumtesa kwa style hio
Binadamu hususan mtu mzima anao uhuru bafsi wa kujitambua na kujua anafanya nini, hicho ulichomfanyia, ninaweza kusema, ni ukiukaji wa haki za binadamu ili ujipatie furaha ndani ya nafsi yako, kama huyo mumeo alikuwa hawezi kubadilika ungetumia njia za kawaida kutafuta suluhu vinginevyo hicho ulichomfanyia ni kama mateso kwake na furaha kwako na hivyo ni wewe unachuma dhambi kwa kumfanya ndondocha/msukule mumeo.
Kwa lugha nyingine kama yeye alikuwa ni mkosefu kwako basi wewe umefanya makosa makubwa zaidi kumfanya ndondocha na kadiri atakavyokuwa hivyo ndio kadiri nawe utachuma dhambi.
Hiyo hatua uliyoichukuwa haina tofauti sana na utajiri wa kafara.