Wanaume walalamikia uchafu wa wake zao

Wanaume walalamikia uchafu wa wake zao

GIRITA

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2016
Posts
4,432
Reaction score
5,864
Kutoka Kijiji cha Kagumoini, eneo bunge la Gatundu Kusini, kaunti ya Kiambu nchini Kenya wamelalamikia wakidai kuwa wake zao ni wachafu kupindukia.

Wanaume hao wanalalamika kuwa wake zao wanashindwa hata kubadilisha nguo kwa zaidi ya wiki moja, hali ambayo inachochea ndoa nyingi kuvunjika.

Hali hiyo wanadai kuwa imechangiwa na uhaba wa maji katika kijiji hicho kutokana na mtoa huduma ya maji wa eneo hilo kuacha kuvuta maji hadi majumbani mwao.

“Wake zetu ndio wanateseka zaidi kwani wanaishi na nguo moja kwa wiki nzima bila kubadilisha. Harufu inayotoka katika nyumba mbalimbali haiwezi kuvumilika tena,” Elijah Mungai Mumu, mkazi wa eneo hilo alisema.

Kutokana na changamoto hiyo ya zaidi ya miaka miwili, wanawake wa kijiji hicho wanalazimika kusafiri zaidi ya kilomita mbili kutafuta maji katika mto Rwabura.

Katika kujibu malalamiko ya waume zao, wanawake hao walimuomba Rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati suala hilo kabla ya hajaondoka madarakani wakidai wametishiwa kuachwa na waume zao.

“Hakika tunapaswa kusikilizwa ikiwa familia zetu zitasimama. Tumeachana na ufugaji kwani hatuwezi kulisha mifugo kwa maji ya kutosha. Tunamwomba Rais Uhuru Kenyatta aingilie kati kabla hajastaafu,” Hellen Mwangi, mkazi mwingine alisema

chanzo: Millard ayo

1645943134675.png
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji24][emoji24][emoji24]

Inasikitisha na kufurahisha
 
Raha ya JF, haya yanatokea Kijiji cha Kagumoini, eneo bunge la Gatundu Kusini, kaunti ya Kiambu nchini Kenya ghafla uzi huu utageuka uwanja wa vita kati yetu humu jukwaani😊
 
Afrika tuna safari ndefu sana, kama kodi mnalipa ku pump maji yafike majumbani ilipaswa kuwa kipaumbele.
Kweli kabisa,Tungemaliza kwanza changamoto za upatikanaji wa maji...ni tatizo kubwa.
 
Raha ya JF, haya yanatokea Kijiji cha Kagumoini, eneo bunge la Gatundu Kusini, kaunti ya Kiambu nchini Kenya ghafla uzi huu utageuka uwanja wa vita kati yetu humu jukwaani😊
Tuombe vita isitokee mkuu
 
Back
Top Bottom