Siwezi kukataa ila iko too general. Unajua kila rika lina namna ya kuliishi. Ukiwa kijana na una kanafasi kiasi jitahidi kupendeza na kuvutia.
Mimi ni kijana, na nakwenda gym. Kwanza, nimeichagua kuwa starehe yangu yaani nikishatoka mihangaikoni sina pa kwenda so naenda gym kupoteza muda.
Pili, nafanya mazoezi kwa ajili ya afya.
Tatu, mimi nina mwili mdogo kiasi kwahiyo naongeza vinyama kimtindo ili tisheti isinipwaye.
Ukitazama malengo yangu yote hakuna napolenga kumvutia mwanaume wala mwanamke.
Accidentally, wanawake wanavutiwa nasi, hata wasipojilengesha ila tukiwataka hawasumbui. Humo wakiwemo wake zenu ninyi wenye miili isiyo na mpangilio, mwili wa mviringo kama puto ama mwembamba ukivaa nguo yoyote haikai.
Bahati mbaya zaidi, mnajua wake zenu wanatupenda. Huo ndio msingi wa hasira zenu kwetu.
Nikushauri kama ni kijana, jitahidi kuishi kama kijana. Ujana ukikoma na gym inakoma, sasa kijana gani mwili mbaya, sura mbaya, kuvaa hujui upo upo tu kama mzee.
Wanawake wenu wakitupenda mnavimba.
Sent using
Jamii Forums mobile app