Wanawake 500 wapata mimba kwa upandikizaji Arusha

Wanawake 500 wapata mimba kwa upandikizaji Arusha

Huyo mtoto ubini wake ni nani..??
Je mwanamke bikra anaweza pandikizwa na akazaa wakati ametunza bikra yake..??
Alafu huu ujinga utasababisha wanawake wawe na kibri sana, kwamba anaweza kupata mtoto hata bila kupigwa miti...😎
Tayari ipo mkuu, wengi km siyo baadhi wanapandikizwa na kuoigwa wembe kisa hawataki kukutana na nyie pia kuoata uchungu as they called usumbufu.

Tatizo baba mtoto ndiye hafahamiki so akikua na kuja kugundua I'ven't Dad sijui inakuwaje 🥲!
 
Wanaotaka huduma ya kubebewa mimba jamani (surrogacy) , kizazi kipo available. Inbox me. [emoji51] No seriously, isn't surrogacy a thing yet in Tz??

Kwa Tanzania bado haijaanza mpaka ianzishwe sheria,

Ni muhimu wananchi tukaanza kupaza sauti ili iwepo.
 
Mwanamke mmoja (50), amefanikiwa kupata watoto mapacha kwa njia ya upandikizaji mimba jijini Arusha.

Mwanamama huyo ni mmoja kati ya wanawake 500 waliofanikiwa kupata watoto kwa huduma hiyo inayotolewa na kituo cha Huduma ya Uzazi na Upandikizaji Mimba cha Avinta Care Medical kilichopo jijini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha mapema wikii hii, Daktari bingwa wa magonjwa ya kinamama na uzazi wa kituo hicho, Nicholaus Mazuguni amesema kwa sasa wanafanya huduma hiyo wakishirikiana na wataalamu kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Amesema waliamua kutoa huduma hiyo ili kutatua changamoto ya uzazi iliyokuwa ikisumbua familia nyingi na kufuata huduma hiyo nje ya nchi, ambapo kwa sasa wanahudumia wagonjwa 100 kwa wiki.

"Tumeanza kutoa huduma hii 2017, tumeshapandikiza wanawake zaidi ya 500 na kufanikiwa kupata watoto zaidi ya 250. Mwitikio ni mkubwa kwa sababu watu walikuwa wanatumia gharama kubwa kwenda nje ya nchi”

"Mara ya mwisho tumempandikiza mapacha mwanamke mwenye miaka 50 na amefanikiwa kupata watoto wake vizuri bila shida yoyote. Wengi wanafurahi kwani wameteseka na kukutana na changamoto nyingi katika kutafuta watoto. Gharama zetu za utoaji wa huduma ni kuanzia Sh7 milioni na kuendelea kulingana na umri wa mgonjwa," amesema.

Kwa upande wake Daktari wa akinamama kutokana Muhimbili, Hildegarda Aloyce amesema wamekuwa wakishirikiana na kituo hicho cha Avinta katika kutatua changamoto za uzazi kwani tatizo hilo bado ni kubwa katika jamii ambapo kati ya wagonjwa 10 ambao wamekuwa wakipokelewa wagonjwa 4 hadi 6 wana tatizo la uzazi .

Mganga Mkuu wa Mkoa, Dokta Sylvia Mamkwe amepongeza juhudi hizo zilizofanywa na kituo hicho kwa kushirikiana na hospitali nyingine,na Kama serikali wapo tayari kutoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha huduma hiyo ili kuwahudumia wagonjwa wengi zaidi.

Mmoja wa wanufaika kutokaa wilayani Simanjiro, Martha Sangwa amesema kuwa amefurahishwa sana kwa huduma hiyo iliyomfanikisha kupata watoto mapacha kwani ameteseka kwa miaka 16 bila msaada wowote, hivyo uwepo wa kituo hicho ni faraja kubwa sana kwao na kuwataka wanawake kujitokeza kwa wingi kupata huduma hiyo.

Source: Mwananchi
Bichwa la habari watoto 500 utumbo wa habari watoto 250 toka 2017, kwa maana hiyo ni uwiano wa watoto 50 tu kwa mwaka au 4 tu kwa mwezi.

Hivi kwanini mnapenda kuandika uongo?
 
Hii inshu ya IVF, huwa ni msaada kwa yupi... Ni mwanaume ndiyo hana uwezo wa kutia mimba? ama ni mwanamke ndiyo hana uwezo wa kunasa mimba?

-Kaveli-
 
Hilo tatizo limekaeje kwa wale wanawake waliotolewa mfuko wa uzazi kutokana na matatizo mbalimbali wanaweza pata mimba au?
 
Alafadhali maana kukosa mtoto kibongo bongo utajuta hasa ukiwa kwenye ndoa.
 
Huyo mtoto ubini wake ni nani..??
Je mwanamke bikra anaweza pandikizwa na akazaa wakati ametunza bikra yake..??
Alafu huu ujinga utasababisha wanawake wawe na kibri sana, kwamba anaweza kupata mtoto hata bila kupigwa miti...[emoji41]
Ushimeeeeen. Unaitwa huku mkuu[emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji23]
 
Mwanamke mmoja (50), amefanikiwa kupata watoto mapacha kwa njia ya upandikizaji mimba jijini Arusha.

Mwanamama huyo ni mmoja kati ya wanawake 500 waliofanikiwa kupata watoto kwa huduma hiyo inayotolewa na kituo cha Huduma ya Uzazi na Upandikizaji Mimba cha Avinta Care Medical kilichopo jijini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha mapema wikii hii, Daktari bingwa wa magonjwa ya kinamama na uzazi wa kituo hicho, Nicholaus Mazuguni amesema kwa sasa wanafanya huduma hiyo wakishirikiana na wataalamu kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Amesema waliamua kutoa huduma hiyo ili kutatua changamoto ya uzazi iliyokuwa ikisumbua familia nyingi na kufuata huduma hiyo nje ya nchi, ambapo kwa sasa wanahudumia wagonjwa 100 kwa wiki.

"Tumeanza kutoa huduma hii 2017, tumeshapandikiza wanawake zaidi ya 500 na kufanikiwa kupata watoto zaidi ya 250. Mwitikio ni mkubwa kwa sababu watu walikuwa wanatumia gharama kubwa kwenda nje ya nchi”

"Mara ya mwisho tumempandikiza mapacha mwanamke mwenye miaka 50 na amefanikiwa kupata watoto wake vizuri bila shida yoyote. Wengi wanafurahi kwani wameteseka na kukutana na changamoto nyingi katika kutafuta watoto. Gharama zetu za utoaji wa huduma ni kuanzia Sh7 milioni na kuendelea kulingana na umri wa mgonjwa," amesema.

Kwa upande wake Daktari wa akinamama kutokana Muhimbili, Hildegarda Aloyce amesema wamekuwa wakishirikiana na kituo hicho cha Avinta katika kutatua changamoto za uzazi kwani tatizo hilo bado ni kubwa katika jamii ambapo kati ya wagonjwa 10 ambao wamekuwa wakipokelewa wagonjwa 4 hadi 6 wana tatizo la uzazi .

Mganga Mkuu wa Mkoa, Dokta Sylvia Mamkwe amepongeza juhudi hizo zilizofanywa na kituo hicho kwa kushirikiana na hospitali nyingine,na Kama serikali wapo tayari kutoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha huduma hiyo ili kuwahudumia wagonjwa wengi zaidi.

Mmoja wa wanufaika kutokaa wilayani Simanjiro, Martha Sangwa amesema kuwa amefurahishwa sana kwa huduma hiyo iliyomfanikisha kupata watoto mapacha kwani ameteseka kwa miaka 16 bila msaada wowote, hivyo uwepo wa kituo hicho ni faraja kubwa sana kwao na kuwataka wanawake kujitokeza kwa wingi kupata huduma hiyo.

Source: Mwananchi
namshukuru Mungu amenipa watoto naturally kupitia mke wangu. hata hivyo, nilishaapa, sitahitaji mtoto wa kupandikiza, simtaki, na nisingempenda., kwasababu nisingeona kama ni mtoto au mwanadamu halisi kama wanadamu wengine. samahani kwa nitakayemuudhi.
 
Hata miaka ya zamani kuzaa kwa procedure ya operation ilikuwa inaonekana ni kitu cha ajabu kwenye jamii lakini kadiri miaka ilivyokuwa inaenda jamii ikaanza kuona ni jambo la kawaida.

Vivyo hivyo kuhusu IVF itafika wakati kuonekana ni jambo la kawaida .

Wenzetu nchi zilizo endelea walishaanza kufanya hizo IVF kwa miaka mingi ilopita.

Sema usilolijua litakusumbua!
 
Bichwa la habari watoo 500 utumbo wa habari no watoto 250 toka 2017, kwa maana hiyo ni uwiano wa watoto 50 tu kwa mwaka au 4 tu kwa mwezi.

Hivi kwanini mnapenda kuandika uongo?
Umezingua maza..ebu tuliza akili soma tena bila kuwa na mrengo fulani

Kwakukusaidia:

500 ni idadi ya waliofanyiwa hiyo procedure

250 ni idadi ya waliozaliwa

IVF haimaanishi inafanikiwa saa zote , wakati mwingine mimba hutoka nk.(kumbuka huu utaratibu hufanyika zaidi kwa wenye changamoto za uzazi.)

Mara chache kwa wale wenye kuhitaji kuchagua jinsia za watoto na wenye kuhitaji mapacha
 
Mwenyezi Mungu amewapa Wanadamu maarifa zaidi na ujuzi katika kuleta suluhisho la changamoto za uzazi Kwa namna moja ama nyingine.

Kwa hiyo ni Mungu anahusika moja kwa moja kwenye hili pia.

Utukufu apewe Mwenyezi Mungu wote.
 
Bure???Kama Ni bure niende wanipandikize mapacha nipumzike😂
 
Kituo kinatoa huduma hiyo kwa watu 100 kwa wiki na toka 2017 wamepandikizwa wanawake 500 tu kwahiyo tuseme kituo kimefanya kazi kwa wiki 5 tu toka kuanza kutoa huduma hiyo mwaka 2017??
 
Back
Top Bottom