Wanawake 500 wapata mimba kwa upandikizaji Arusha

Wanawake 500 wapata mimba kwa upandikizaji Arusha

Tayari ipo mkuu, wengi km siyo baadhi wanapandikizwa na kuoigwa wembe kisa hawataki kukutana na nyie pia kuoata uchungu as they called usumbufu.

Tatizo baba mtoto ndiye hafahamiki so akikua na kuja kugundua I'ven't Dad sijui inakuwaje 🄲!
Nafikiri wanachukua sperm za waume zao halafu wanaziingiza kwa wenza wao
 
Hii inshu ya IVF, huwa ni msaada kwa yupi... Ni mwanaume ndiyo hana uwezo wa kutia mimba? ama ni mwanamke ndiyo hana uwezo wa kunasa mimba?

-Kaveli-
Unaweza kuwasaidia wote,kwa mfano mwanaume anaweza kushindwa kusababisha nimba kwa sababu ya uchache wa manii.hii njia inamfaa
 
Huyo mtoto ubini wake ni nani..??
Je mwanamke bikra anaweza pandikizwa na akazaa wakati ametunza bikra yake..??
Alafu huu ujinga utasababisha wanawake wawe na kibri sana, kwamba anaweza kupata mtoto hata bila kupigwa miti...[emoji41]
Kwan shida ipo wapi?! Wao wapate watoto walee wenyewe nani anataka kuhangaika na watu wenye kiburi. Matatizo ya malezi ya watoto, matabia mambovu watapambana nayo wao wenyewe na viburi vyao.
 
Hilo tatizo limekaeje kwa wale wanawake waliotolewa mfuko wa uzazi kutokana na matatizo mbalimbali wanaweza pata mimba au?
Ukitolewa mji wa uzazi huo ujauzito unaenda kutungia wapi kwenye kibofu au?!
 
Hilo tatizo limekaeje kwa wale wanawake waliotolewa mfuko wa uzazi kutokana na matatizo mbalimbali wanaweza pata mimba au?
Hawawez maana ukuaji wa mtoto unaanzia kwenye mfuko wa uzazi.
 
Mwanamke mmoja (50), amefanikiwa kupata watoto mapacha kwa njia ya upandikizaji mimba jijini Arusha.

Mwanamama huyo ni mmoja kati ya wanawake 500 waliofanikiwa kupata watoto kwa huduma hiyo inayotolewa na kituo cha Huduma ya Uzazi na Upandikizaji Mimba cha Avinta Care Medical kilichopo jijini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha mapema wikii hii, Daktari bingwa wa magonjwa ya kinamama na uzazi wa kituo hicho, Nicholaus Mazuguni amesema kwa sasa wanafanya huduma hiyo wakishirikiana na wataalamu kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Amesema waliamua kutoa huduma hiyo ili kutatua changamoto ya uzazi iliyokuwa ikisumbua familia nyingi na kufuata huduma hiyo nje ya nchi, ambapo kwa sasa wanahudumia wagonjwa 100 kwa wiki.

"Tumeanza kutoa huduma hii 2017, tumeshapandikiza wanawake zaidi ya 500 na kufanikiwa kupata watoto zaidi ya 250. Mwitikio ni mkubwa kwa sababu watu walikuwa wanatumia gharama kubwa kwenda nje ya nchiā€

"Mara ya mwisho tumempandikiza mapacha mwanamke mwenye miaka 50 na amefanikiwa kupata watoto wake vizuri bila shida yoyote. Wengi wanafurahi kwani wameteseka na kukutana na changamoto nyingi katika kutafuta watoto. Gharama zetu za utoaji wa huduma ni kuanzia Sh7 milioni na kuendelea kulingana na umri wa mgonjwa," amesema.

Kwa upande wake Daktari wa akinamama kutokana Muhimbili, Hildegarda Aloyce amesema wamekuwa wakishirikiana na kituo hicho cha Avinta katika kutatua changamoto za uzazi kwani tatizo hilo bado ni kubwa katika jamii ambapo kati ya wagonjwa 10 ambao wamekuwa wakipokelewa wagonjwa 4 hadi 6 wana tatizo la uzazi .

Mganga Mkuu wa Mkoa, Dokta Sylvia Mamkwe amepongeza juhudi hizo zilizofanywa na kituo hicho kwa kushirikiana na hospitali nyingine,na Kama serikali wapo tayari kutoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha huduma hiyo ili kuwahudumia wagonjwa wengi zaidi.

Mmoja wa wanufaika kutokaa wilayani Simanjiro, Martha Sangwa amesema kuwa amefurahishwa sana kwa huduma hiyo iliyomfanikisha kupata watoto mapacha kwani ameteseka kwa miaka 16 bila msaada wowote, hivyo uwepo wa kituo hicho ni faraja kubwa sana kwao na kuwataka wanawake kujitokeza kwa wingi kupata huduma hiyo.

Source: Mwananchi
baba wa mtoto nani? Na ikiwa mwanamke anamume inahitaji makubaliano.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] buree ni wee na shem kugalagazana tyuuh.
Kugalagazana Tena..!!!..kwenye kupandikiza??au Mimi sijaelewašŸ¤”
 
Milioni 7 mara 100 kwa wiki ni 700mil. , kwa mwezi ni kama bilioni 3. Sasa kwanini tusiwalipishe hili tangazo la biashara?

Pia huyo wa miaka 50, alipandikizwa mayai yake au ya mwanamke mwingine? Kama ni ya mwanamke mwingine basi ni bora uka-adopt tu, maana hata ukipima DNA itaonyesha kwamba wewe sie mzazi wake
 
Nini kimefanya wenyewe washindwe kupandikiza na Arusha ni baridi? Au nao wameambukizwa udhaifu toka Namanga na Taveta
Kwa sababu kuna matatizo ya uzazi wanawake, ambapo mayai inabidi kwanza yavunwe, halafu yarubishwe kwenye test tube kisha zygote ndio ipandikizwe tumboni.
 
Tunawatakia mafanikio makubwa.
Mwanamke mmoja (50), amefanikiwa kupata watoto mapacha kwa njia ya upandikizaji mimba jijini Arusha.

Mwanamama huyo ni mmoja kati ya wanawake 500 waliofanikiwa kupata watoto kwa huduma hiyo inayotolewa na kituo cha Huduma ya Uzazi na Upandikizaji Mimba cha Avinta Care Medical kilichopo jijini humo

Amesema waliamua kutoa huduma hiyo ili kutatua changamoto ya uzazi iliyokuwa ikisumbua familia nyingi na kufuata huduma hiyo nje ya nchi, ambapo kwa sasa wanahudumia wagonjwa 100 kwa wiki.

"Tumeanza kutoa huduma hii 2017, tumeshapandikiza wanawake zaidi ya 500 na kufanikiwa kupata watoto zaidi ya 250. Mwitikio ni mkubwa kwa sababu watu walikuwa wanatumia gharama kubwa kwenda nje ya nchiā€

"Mara ya mwisho tumempandikiza mapacha mwanamke mwenye miaka 50 na amefanikiwa kupata watoto wake vizuri bila shida yoyote. Wengi wanafurahi kwani wameteseka na kukutana na changamoto nyingi katika kutafuta watoto. Gharama zetu za utoaji wa huduma ni kuanzia Sh7 milioni na kuendelea kulingana na umri wa mgonjwa," amesema.

Kwa upande wake Daktari wa akinamama kutokana Muhimbili, Hildegarda Aloyce amesema wamekuwa wakishirikiana na kituo hicho cha Avinta katika kutatua changamoto za uzazi kwani tatizo hilo bado ni kubwa katika jamii ambapo kati ya wagonjwa 10 ambao wamekuwa wakipokelewa wagonjwa 4 hadi 6 wana tatizo la uzazi .

Mganga Mkuu wa Mkoa, Dokta Sylvia Mamkwe amepongeza juhudi hizo zilizofanywa na kituo hicho kwa kushirikiana na hospitali nyingine,na Kama serikali wapo tayari kutoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha huduma hiyo ili kuwahudumia wagonjwa wengi zaidi.
 
namshukuru Mungu amenipa watoto naturally kupitia mke wangu. hata hivyo, nilishaapa, sitahitaji mtoto wa kupandikiza, simtaki, na nisingempenda., kwasababu nisingeona kama ni mtoto au mwanadamu halisi kama wanadamu wengine. samahani kwa nitakayemuudhi.
Mkuu; Atakayeudhika kwa maamuzi yako ww binafsi atakuwa ana lake jambo.
Hoja yangu kwako ni hii: Je, hao watoto wako uliopata naturally kupitia mke wako unauhakika 100% ni wewe uliyepandikiza?? Wahenga wanatutanabahisha kwamba anayemjua baba wa mtoto kwa uhakika ni Mama. Ndiyo maana Wahenga waliweka msemo "kitanda hakizai haramu" kwa lengo la kuepusha udadisi-dadisi kwa Wake zetu na kuepusha Migogoro mingi katika ndoa zetu na watoto watakaozaliwa baina yenu wanandoa wapate matunzo.
Samahani lakini kama nitakuwa nimekuudhi.
 
Tayari ipo mkuu, wengi km siyo baadhi wanapandikizwa na kuoigwa wembe kisa hawataki kukutana na nyie pia kuoata uchungu as they called usumbufu.

Tatizo baba mtoto ndiye hafahamiki so akikua na kuja kugundua I'ven't Dad sijui inakuwaje 🄲!
Mkuu; Baba wa mtoto atafahamika kwani katika mfumo wa uchukuaji mbegu(Sperm-donor) na Upandikizaji kumbukumbu hutunzwa. Mtindo huu kwa upande wa wanyama/mifugo unaitwa Uhimilishaji (Artificial Insemination).
Tatizo ninaloliona kwa binadamu ni kwa Wanaume Inferior watakuwa eliminated i.e. hawatapata fursa ya kuzaa au kuendeleza kizazi chao kwani vinasaba visivyotakiwa (inferior Traits) hazitakiwi.
 
Back
Top Bottom