Wanawake 500 wapata mimba kwa upandikizaji Arusha

Wanawake 500 wapata mimba kwa upandikizaji Arusha

Yeah Kweli kabisa, Mwenye Uhakika 100% ni mama! Mara nyingi sie tumekuwa tunaenda kwa Imani tu kwamba mtoto ni wako ila in real sense hata tukisema Mke wako amseti mtu then upewe taarifa kuhusu kuwa kuna uwezekano kwamba Huyo dogo sio wako/ AM shure utaanza kuamini hata kama si kweli.
Naam; Kwa imani ni bora zaidi. 🙏
 
wote wa kwangu, tunafanana copyright. though kuna mmoja wa nje ambaye tunafanana nusu, nina mpango wa kupiga DNA. na hata akitokea kuwa sio wangu, nimeshampenda, nitamtunza hadi atakapokuja kuamua yeye mwenyewe niendelee kuwa babake au la, kwasababu upendo wake kwangu ni mkuuu na ananiita baba.
Hilo ndio la msingi sana.🙏na busara kuliko kuanzisha malumbano yasiyo na Tija.
Excellent mkuu.
 
Kwa wasiyo na mume, ina maana wanaponunua sperm madaktari wanaeleza 'haya mayai mwenyewe anaitwa 1234Y anaishi Y4321 na namba yake ya simu hii hapa 12Y34?.'
Sio kivile haswa ila mwanamke anachagua kati ya wanaume waliodonate sperms wanaubora gani ambao yy anautaka e.g. maumbile kimwili(muonekano wa nje mathalani massive,slim, tall, moderate, hana kilema cha Asili,nk ...), ustahimilivu wa magonjwa na hali ngumu ya mazingira etc. Hapo ndio chaguo lake linazingatiwa na mchakato wa Urutubishaji yai la mwanamke hufanyika kwa sperms kuingizwa katika mfumo wa kizazi cha mwanamke pindi yai (Ovum) linapokuwa limepevuka. Ni mchakato complicated kidogo ila ni rahisi sana.
 
Hao sasa ndio Watoto wa kisasa OG

After miaka 10 tukutane tena hapa jukwaani tujadili
 
Baba si ndie anayetoa mbegu (shahawa/manii)?
Ndiyo lakini katika scenario hii; Watakuwepo Baba wa aina 2:-
(a) Baba mlezi/mtunzaji mimba na mtoto atakayezaliwa (b) Baba mzazi(Biological father). Huyo Biological father anaweza akawa ni huyohuyo (a) na (b) au akawa ni mtu mwanaume mwingine Mfadhili wa sperms. Ni kweli aliyetoa shahawa iwe ni kwa Ufadhili au vinginevyo ndiye Baba ki-Ukweli. Huyo mlezi cjui nin nini huyo ni Mhudumu na sio wa lazima kuwepo kwani wapo single mothers na wanajimudu vyema utunzaji.
 
Bichwa la habari watoo 500 utumbo wa habari no watoto 250 toka 2017, kwa maana hiyo ni uwiano wa watoto 50 tu kwa mwaka au 4 tu kwa mwezi.

Hivi kwanini mnapenda kuandika uongo?

bora umejileta nikupige swali...

Hivi Uislamu unaruhusu upandikizaji wa mimba.?
 
Hao sasa ndio Watoto wa kisasa OG

After miaka 10 tukutane tena hapa jukwaani tujadili
Human breeding! Unazalisha aina(breed/koo) ya mtu mwenye sifa unazotaka wewe.
Hii kitu ni Hatari sana (hebu fikiria kuku wa kisasa na ukuaji wake ulivyo wa fasta n.k) na ikiendelezwa Itaanza kufanyika "Human Cloning"😢😭 miaka 10 ni mingi mno bro.
 
bora umejileta nikupige swali...

Hivi Uislamu unaruhusu upandikizaji wa mimba.?
Swali lako zuri sana:

Jibu...

Kutafuta tiba ya utasa sio tu inajuzu, bali pia kunahimizwa katika Uislam. Katika sheria za Kiislam, teknolojia zote za usaidizi za uzazi (ARTs) zinaruhusiwa, mradi tu chanzo cha mbegu ya kiume, yai la uzazi, na uterasi kinatokana na wanandoa waliooana kihalali katika kipindi cha ndoa yao. Hakuna mtu wa tatu anayepaswa kuingilia kazi za ndoa za ngono na uzazi. Ubaguzi haukubaliwi katika Uislamu. Idadi ya ziada ya viinitete vilivyorutubishwa inaweza kuhifadhiwa kwa kuhifadhiwa na inaweza kuhamishiwa kwa mke yuleyule katika mzunguko unaofuatana, huku ndoa ikiwa thabiti. Kutumia manii iliyogandishwa baada ya kifo cha mume hairuhusiwi.

Nahisi wewe unadhani kuwa hii tekolojia ndiyo kwanza umeisikia ikifika na kushamiri Tanzania basi na wengine hawaifahamu! Ulikuwa huelewi kuwa, katika nchi nyingi zenye Waislam wengi teknolojia za uzazi zipo kwa miaka mingi sasa. Hapa kwetu ndiyo kwanza tunayaona ambayo wenzetu wanayo zamani...

Utafiti wa kianthropolojia wa kimatibabu kuhusu sayansi, teknolojia ya kibayoteknolojia, na dini umezingatia “ulimwengu wa kimaadili wa mahali hapo” wa wanaume na wanawake wanapofanya maamuzi magumu kuhusu afya zao na mwanzo na mwisho wa maisha ya binadamu. Mada hii inaangazia ulimwengu wa kimaadili wa Waislamu wasio na uwezo wa kuzaa wanapojaribu kutengeneza, kwa mtindo sahihi wa kidini, watoto wa Kiislamu katika kliniki za urutubishaji katika mfumo wa uzazi (IVF) nchini Misri na Lebanon. Mapema kama 1980, fatwa zenye mamlaka zilizotolewa kutoka Chuo Kikuu cha Al-Azhar maarufu nchini Misri zilipendekeza kwamba IVF na teknolojia kama hizo zinaruhusiwa mradi hazihusishi aina yoyote ya mchango wa mtu wa tatu (wa manii, mayai, viinitete, au uterasi). Tangu mwishoni mwa miaka ya 1990, hata hivyo, tofauti za maoni kuhusu mchango wa gamete wa wahusika wengine zimetokea kati ya Waislamu wa Sunni na Shi’ite, huku Ayatollah anayeongoza wa Iran akiruhusu mchango wa gamete chini ya masharti fulani. Fatwa hii ya Irani imekuwa na athari kubwa kwa nchi ya Lebanon, ambapo Washia walio wengi pia wanatafuta huduma za IVF. Kulingana na vipindi vitatu vya utafiti wa ethnografia katika kliniki za IVF za Misri na Lebanon, karatasi hii inachunguza mijadala rasmi na isiyo rasmi ya kidini inayozunguka mazoezi ya IVF na michango ya watu wengine katika ulimwengu wa Kiislamu, pamoja na athari za kijinsia za mchango wa gamete kwa ndoa za Kiislamu.
 
Human breeding! Unazalisha aina(breed/koo) ya mtu mwenye sifa unazotaka wewe.
Hii kitu ni Hatari sana (hebu fikiria kuku wa kisasa na ukuaji wake ulivyo wa fasta n.k) na ikiendelezwa Itaanza kufanyika "Human Cloning"😢😭 miaka 10 ni mingi mno bro.

Acha tujipe muda coz hatuna la kufanya kuzuia haya yanayoendelea,, tunaona kama hayatuhusu hivi
 
Acha tujipe muda coz hatuna la kufanya kuzuia haya yanayoendelea,, tunaona kama hayatuhusu hivi
Tunalo la kufanya hata kama hatutaweza kuzuia moja kwa moja yanayoendelea. Kwanza ni kupaza sauti na kuweka wazi (create awareness) kwa Jamii ili ijue mustakabali na hatima ya yanayoendelea na Athari zake.(Mbona wameweza hoja ya Ukeketaji?)
Cha Pili ni kuijengea uwezo (capacity building) jamii ili iweze kubaini Mapungufu yaliyopo/yatokanayo na kwa Hiari isijiingize au kuruhusu jambo hilo miongoni mwao.
Hapa ndipo elimu itolewe na kutumia Mifano Hai iliyopo hata kama ikibidi itumike kutoka uzoefu uliopatikana kwenye Mifugo(Ikumbukwe na kuzingatiwa kwamba Binadamu nao ni mojawapo ya Wanyama - hatuna tofauti kubwa).Mbona hata wazee wetu zamani walikuwa makini sana inapokuwa ni hoja ya Ndoa kwa vijana wao?
Cha Tatu ni Kupanua wigo kwa kuhusisha Watu/Jamii/Mashirika na Taasisi/Wafadhili mbalimbali wenye mapenzi mema kwa jamii yetu ili kusimama kinyume na jambo hilo. Mbona Serikali/Viongozi wameweza kutunga Sheria kuhusu Ushoga?
La Mwisho (au la Nne) ni kujiwekea Mkakati wa Makusudi wa kuhafifisha na kusambaratisha juhudi zozote zinazolenga kuliendeleza Jambo hilo.
 
namshukuru Mungu amenipa watoto naturally kupitia mke wangu. hata hivyo, nilishaapa, sitahitaji mtoto wa kupandikiza, simtaki, na nisingempenda., kwasababu nisingeona kama ni mtoto au mwanadamu halisi kama wanadamu wengine. samahani kwa nitakayemuudhi.
Umetanguliza kushukuru Mungu
Kama unaamini kuna mungu maana yake unaamini kama wewe umepewa bado una generations zako mbele. What if mwanao umezaa anepata hilo tatizo au mjukuu nk

Kama unakula broilers au mayai ya layers na unapandikiza mbegu za mahindi za ASA shambani kwako, amini sayansi ni matokeo chanya ya changamoto anazokumbana nazo mwanadamu
 
Sasa uweke akiba ya maneno!

Maana isije ikaja tokea kwa wanao ikija kuwa mtihani mkubwa!

Mwenyezi Mungu atuhurumie na kutuepusha na magumu!
watoto wangu nimewakabidhi kwa Mungu, na Mungu wetu hatakuja kutuacha. Mungu hadhihakiwi, apandacho mtu ndicho atakachovuna. kuwa ukweli ambao ni mgumu kuuongea, nao ni huu. ukiona una tatizo la kupata watoto, jua kuna mambo mawili

(1) ni jaribu Mungu amekupatia ili akutumie kupata utukufu na kuwa fundisho kwa wengine, mwisho wa jaribu la aina hii huwa ni furaha na kicheko milele.

(2) aidha umechezea kizazi, ulishawahi kuugua magonjwa ya zinaa, una mashetani au kuna mikataba wewe mwenyewe au wazazi wako waliingia na mashetani. dawa hapa ni moja tu, kutubu na kumwomba Mungu peke yake atatue tatizo. ukiwa persistent, Mungu huwa anajibu. Yesu alitoa mfano mmoja wa kuomba bila kukoma akasema kulikuwa na kadhi/hakimu mmoja ambaye kulikuwa na mjane alikuwa akimsumbua muda wote akimtaka apate haki yake, yule hakimu akaamua kumpa tu ili aachane na usumbufu. akatuasa tuombe bila kukoma. kama hakimu aliye dhalimu anaweza kuwapa vitu watu, je si zaidi Mungu wetu anayetupenda kupita upeo?

ajabu pia ni kwamba, Mungu wetu ni Mungu wa Rehema, huwa anasamehe na kusahau kama mtu akija kwake kwa kutubu akimaanisha kuacha dhambi kwa kweli. hivyo hata kama ulitoa sana mimba ukaharibu kizazi, atakusamehe na atakuponya. zaburi 119 inasema "akusamehe maovu yako yote, akuponya magonjwa yako yote". hata kama umeingia mikataba ya mashetani kwa kujua au kwa kutokujua, atakusamehe na kukukomboa. watu wanaingia sana mikataba na mashetani kwa njia ya madawa ya kibiashara, madawa ya kujilinda, madawa ya kazi n.k, shetani hajawahi kumpa mtu kitu bure, lazima ulipie. ndio maana wote wanaokabidhi maisha yao kwa shetani/waganga n.k lazima huwa kuna siku yao ya majuto inakuja mbeleni, kwasababu wameamua kumkataa Mungu wakachagua shetani, wameamua kumtii wakiona shetani anaweza kuliko Mungu, wakamdharau yule aliyewaumbe anayejua kila kona ya miili yao. ndio maana wamebaki kutegemea sayansi badala ya Mungu. katika maisha yangu niliapa sitakuja kuhitaji mtoto wa kupandikiza, kwasababu huyo sio asili, nilihitaji mtoto asili na Mungu akanipa, na Mungu atawapa wengine wote wanaomwomba hata leo. yeye sio dhalimu, ila sisi wanadamu huwa tunaondoka mikononi mwake na shetani akitupiga ndio tunaanza kuona kama Mungu yupo mbali kwanini hatusaidii kumbe ni sisi wenyewe tumeondoka kwenye mikono yake ya ulinzi.

katika maisha yangu, nilishawahi kukosa watoto kwa miaka kadhaa, sikujua kumbe Mungu alikuwa ametaka kujitwalia utukufu. Mungu alifunga tumbo la mke wangu kama alivyofanya kwa sara, alipoanza kuzaa, hadi tumesema Mungu sasa basi, na watoto ni copyright na mimi. shetani hana mkataba na mimi, hana haki yeyote kwangu wala kwa watoto wangu, kwasababu Yesu Kristo alininunua kwa Damu yake, alimaliza deni lote. ningekuwa nadaiwa na shetani angefanya chochote lakini kwasasa hana haki yeyote kwangu kwa sheria za kiroho.

katika nyakati zangu za kukosa watoto, nilishaapa kwamba kwamwe sitokuja kwenda kwa mganga wa kienyeji wala kunywa madawa ya mitishamba n.k, na kweli mimi na mke wangu hatukwenda, pia tuliapa kwamba hatutahitaji kupandikiza wala kutafuta mtoto wa kuasili. sisemi watu wasiasili lakini kwa upande wetu tuliamua kwamba tutaishi hivihivi kama Mungu ndivyo alivyoamua, na baada ya kumwangalia Mungu tu, alitutokea siku moja kwa maono, watoto wangu wote tuliozaa tuliwaona katika maono kabla hata hawajazaliwa. Mungu ni Mkuu sana.

kama kuna mtu yeyote humu ambaye hana watoto, nakuasa, Mtazame huyo aliyeangikwa juu ya msalaba ili upate kuishi, kama vile Musa alivyomwinua nyoka wa shaba jangwani ndivyo Mwana wa Adamu alivyoinuliwa kwenye mti wa msalaba ili kila amwaminiye awe na uzima. hoja hapa ni kwamba, hakuna aliyeweka macho yake kwa Yesu tu akaaibika. shida watu wanakuwa wanamwomba Mungu na wakati huohuo akili zao zipo kwa wanadamu na kwa waganga wa kienyeji. michanganyo kwa michanganyo, Mungu hachanganywi, sasa hata ukipata unachokitafuta kwasababu ulichanganya sana itajulikana ni Mungu amekupa au na wanadamu au waganga au mashetani?ndio maana Mungu akiona unafanya michanganyo huwa anaamua kukaa pembeni anakuacha. mwangalie yeye tu, mwamini yeye tu, weka tumaini lako looote kwake tu, atakusaidia. Hakuna aliyemtumaini Mungu akaaibika, hii ndio siri na tabia ya Mungu, wote wanaomkimbilia ameahidi hawatatahayarika/hawataaibika. na kama amesema kwenye Neno lake, lazima atatenda. ni Mungu wa principles.

Mungu awabariki sana.
 
Umetanguliza kushukuru Mungu
Kama unaamini kuna mungu maana yake unaamini kama wewe umepewa bado una generations zako mbele. What if mwanao umezaa anepata hilo tatizo au mjukuu nk

Kama unakula broilers au mayai ya layers na unapandikiza mbegu za mahindi za ASA shambani kwako, amini sayansi ni matokeo chanya ya changamoto anazokumbana nazo mwanadamu
hilo tatizo haliwezi kunipata mimi wala watoto wangu wala kizazi changu kwa Jina la Yesu Kristo. tunalindwa na Mungu and I refuse matatizo hayo kabisa,sio fungu langu wala la kizazi changu. hayana haki kwenye maisha yetu kwasababu tumekombolewa kwa Damu ya Yesu Kristo. tule broiler au chochote, hata tukila vitu vya kufisha havitatudhuru kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
 
Mkuu Wife wako akiamua atest mitambo tu kwa kutumia hata rafiki yako wa karibu, labda kuonyesha mawasiliano fake kuhusu Watoto sio wako; Uwe na hakika kuna namna utaanza kufuatilia kujua whats Happen ili upate taarifa,Sidhani kama utakaa tu uendelee kujiaminisha kwamba ni wako kisa mnafanana. Tena unaweza kuanza kuona kasoro fulani kwenye kufanana kwenu hiyo yote ni kwa sababu umepata taarifa inayokinzana na unavyoamini. Hiyo inaonyesha haukuwa sure kiviile.
unajua unavyoongea, ni sawa na mtu aje leo hii aseme baba yangu mimi sio baba yangu, wakati hata nikiangalia kwenye picha tumepishana umri tu, ila sura kila kitu nafanana na babangu. nikipita sehemu zingine watu huwa wanashika vichwa wanashangaa imekuwaje dingi kanizaa nafanana naye namna hii. ndivyo ilivyo kwa watoto wangu ambao Mungu amenipa (atawapatia pia wote wanaomwamini, ni maombi yangu na hata nisipoomba Mungu atawapatia tu), nafanana mno na watoto wangu, nina damu kali mno. hata sihitaji DNA..
 
Hii kitu ni balaa kwa mwanaume asiezaa 😁 u M/ke anaweza akawekewa sperm za M/me mwingine bila kujua
 
Huduma hii itawafikiaje wananchi masikini wasio na uwezo bali wangehitaji?
Maskini hajawai kukosa nguvu za kiume wewe!
Au hujawaiskia msemo.....maskin na wanae, tajir na mali zake!
 
namshukuru Mungu amenipa watoto naturally kupitia mke wangu. hata hivyo, nilishaapa, sitahitaji mtoto wa kupandikiza, simtaki, na nisingempenda., kwasababu nisingeona kama ni mtoto au mwanadamu halisi kama wanadamu wengine. samahani kwa nitakayemuudhi.
Binafsi umeniuudhi ila nishakusamehe kama ulivyoomba
 
Back
Top Bottom