Sasa uweke akiba ya maneno!
Maana isije ikaja tokea kwa wanao ikija kuwa mtihani mkubwa!
Mwenyezi Mungu atuhurumie na kutuepusha na magumu!
watoto wangu nimewakabidhi kwa Mungu, na Mungu wetu hatakuja kutuacha. Mungu hadhihakiwi, apandacho mtu ndicho atakachovuna. kuwa ukweli ambao ni mgumu kuuongea, nao ni huu. ukiona una tatizo la kupata watoto, jua kuna mambo mawili
(1) ni jaribu Mungu amekupatia ili akutumie kupata utukufu na kuwa fundisho kwa wengine, mwisho wa jaribu la aina hii huwa ni furaha na kicheko milele.
(2) aidha umechezea kizazi, ulishawahi kuugua magonjwa ya zinaa, una mashetani au kuna mikataba wewe mwenyewe au wazazi wako waliingia na mashetani. dawa hapa ni moja tu, kutubu na kumwomba Mungu peke yake atatue tatizo. ukiwa persistent, Mungu huwa anajibu. Yesu alitoa mfano mmoja wa kuomba bila kukoma akasema kulikuwa na kadhi/hakimu mmoja ambaye kulikuwa na mjane alikuwa akimsumbua muda wote akimtaka apate haki yake, yule hakimu akaamua kumpa tu ili aachane na usumbufu. akatuasa tuombe bila kukoma. kama hakimu aliye dhalimu anaweza kuwapa vitu watu, je si zaidi Mungu wetu anayetupenda kupita upeo?
ajabu pia ni kwamba, Mungu wetu ni Mungu wa Rehema, huwa anasamehe na kusahau kama mtu akija kwake kwa kutubu akimaanisha kuacha dhambi kwa kweli. hivyo hata kama ulitoa sana mimba ukaharibu kizazi, atakusamehe na atakuponya. zaburi 119 inasema "akusamehe maovu yako yote, akuponya magonjwa yako yote". hata kama umeingia mikataba ya mashetani kwa kujua au kwa kutokujua, atakusamehe na kukukomboa. watu wanaingia sana mikataba na mashetani kwa njia ya madawa ya kibiashara, madawa ya kujilinda, madawa ya kazi n.k, shetani hajawahi kumpa mtu kitu bure, lazima ulipie. ndio maana wote wanaokabidhi maisha yao kwa shetani/waganga n.k lazima huwa kuna siku yao ya majuto inakuja mbeleni, kwasababu wameamua kumkataa Mungu wakachagua shetani, wameamua kumtii wakiona shetani anaweza kuliko Mungu, wakamdharau yule aliyewaumbe anayejua kila kona ya miili yao. ndio maana wamebaki kutegemea sayansi badala ya Mungu. katika maisha yangu niliapa sitakuja kuhitaji mtoto wa kupandikiza, kwasababu huyo sio asili, nilihitaji mtoto asili na Mungu akanipa, na Mungu atawapa wengine wote wanaomwomba hata leo. yeye sio dhalimu, ila sisi wanadamu huwa tunaondoka mikononi mwake na shetani akitupiga ndio tunaanza kuona kama Mungu yupo mbali kwanini hatusaidii kumbe ni sisi wenyewe tumeondoka kwenye mikono yake ya ulinzi.
katika maisha yangu, nilishawahi kukosa watoto kwa miaka kadhaa, sikujua kumbe Mungu alikuwa ametaka kujitwalia utukufu. Mungu alifunga tumbo la mke wangu kama alivyofanya kwa sara, alipoanza kuzaa, hadi tumesema Mungu sasa basi, na watoto ni copyright na mimi. shetani hana mkataba na mimi, hana haki yeyote kwangu wala kwa watoto wangu, kwasababu Yesu Kristo alininunua kwa Damu yake, alimaliza deni lote. ningekuwa nadaiwa na shetani angefanya chochote lakini kwasasa hana haki yeyote kwangu kwa sheria za kiroho.
katika nyakati zangu za kukosa watoto, nilishaapa kwamba kwamwe sitokuja kwenda kwa mganga wa kienyeji wala kunywa madawa ya mitishamba n.k, na kweli mimi na mke wangu hatukwenda, pia tuliapa kwamba hatutahitaji kupandikiza wala kutafuta mtoto wa kuasili. sisemi watu wasiasili lakini kwa upande wetu tuliamua kwamba tutaishi hivihivi kama Mungu ndivyo alivyoamua, na baada ya kumwangalia Mungu tu, alitutokea siku moja kwa maono, watoto wangu wote tuliozaa tuliwaona katika maono kabla hata hawajazaliwa. Mungu ni Mkuu sana.
kama kuna mtu yeyote humu ambaye hana watoto, nakuasa, Mtazame huyo aliyeangikwa juu ya msalaba ili upate kuishi, kama vile Musa alivyomwinua nyoka wa shaba jangwani ndivyo Mwana wa Adamu alivyoinuliwa kwenye mti wa msalaba ili kila amwaminiye awe na uzima. hoja hapa ni kwamba, hakuna aliyeweka macho yake kwa Yesu tu akaaibika. shida watu wanakuwa wanamwomba Mungu na wakati huohuo akili zao zipo kwa wanadamu na kwa waganga wa kienyeji. michanganyo kwa michanganyo, Mungu hachanganywi, sasa hata ukipata unachokitafuta kwasababu ulichanganya sana itajulikana ni Mungu amekupa au na wanadamu au waganga au mashetani?ndio maana Mungu akiona unafanya michanganyo huwa anaamua kukaa pembeni anakuacha. mwangalie yeye tu, mwamini yeye tu, weka tumaini lako looote kwake tu, atakusaidia. Hakuna aliyemtumaini Mungu akaaibika, hii ndio siri na tabia ya Mungu, wote wanaomkimbilia ameahidi hawatatahayarika/hawataaibika. na kama amesema kwenye Neno lake, lazima atatenda. ni Mungu wa principles.
Mungu awabariki sana.