hahahaaa umenikumbusha jamaa yangu alikuwa na kapikipiki kake akitoke kati ya mji, akaona sio kesi ngoja apitie pale kwa macheni, alipofika pale akaagiza bia zake mbili, akazikata fasta, ghafla akaja muhudumu na bia mbili zingine, akamwambia jamaa yako amekuagizia, mwana bila kujiuliza akapiga, ataka kumaliza, zikaja tena mbili, mmh, jamaa akauliza ni nani anakutuma akaambiwa jamaa yule pale, kidogo ukaja mchemsho, jamaa kichwa ikaanza kuchaji, akaona hapa lazma nimuone anayeniagizia, wakati anamaliza mchemsho sasa ndio likaja pandikizi la dume, na yeye ndio anainuka, kwanza akashikwa tako, dah jamaa akahamaki, akaambiwa tulia kijana, mambo madogo tu haya, usijali utazoea unaonekana we ni mpya mambo haya bado huna uzoefu nayo, usijali hata wenzako walikuwa wakali kama wewe, akashikwa tena tako, janaa ilimchomoka ngumi moja matata sana, yule bazazi chali, damu kibao, cha ajabu alipoinuka akamuagizia aletewe bia tatu, kwani kijana anaonekana sildi, mshikaji alivyosikia hivyo akaanza kukimbia huku akipiga kelele, na pikipiki akaisahau, alipofika maskani ndio akaja kuomba msaada turudi nae afuate pikipiki...