Maisha sio fair ila hakuna namna tuvumiliane.
Mwaka huu nilikuwa introduced kwa binti fulani, nikapenda character yake. Mwanzo akawa ananipotezea, siku moja kakubali nikamtoa, basi toka siku hiyo si akawa kama kapagawa nami.
Kumbe ana bwana yake wamedumu toka chuo wamepitia mengi, ila msela ndo hajajipata. Aliniambia ana mahusiano, but kila mtu ana mahusiano so sikujali sana maana sikujua kama jamaa anamwelewa sana binti.
Siku zilivyozidi kwenda jamaa akanotsi binti anamuignore, kisa tu nikija nambeba kwa gari, nampeleka nice places.
Jamaa kumbana binti si akasema hamtaki tena amepata new guy ambaye ni mimi. Sina hili wala lile namba mpya inanipigia usiku. Kusikia ni jamaa anaanza jitambulisha, anauliza kama namfahamu binti fulani. Anyway niliona jamaa kafanya jambo la kidwanzi sana, mimi siwezi kumpgia msela anayepita na mpenzi wangu for what, labda angekuwa mke.
Ila alikuwa mstaarabu so na mimi ni ka act cool. Jamaa akaanza nieleza walikotoka, jinsi anavyompenda sijui nini. Mimi mwisho nikamwambia, ni kweli alichokwambia, ila mimi sikujua kama mko serious kihivyo. Ila kama vipi flesh, mimi nampotezea manzi wako. Ila mwanangu jitafute, acha kulialia na mabinti, mimi ntampotezea, ila atakuja mwingine atambeba. Wewe badala ya kujitafuta uko unalialia haikusaidii.
Kumbe boya linanirekodi si likaenda msikilizisha.
To cut the story short... Demu nilimpotezea na demu akampotezea jamaa pia.
So mwanangu, wanawake ni opportunist, akiona fadhali kwa mtu wengi wako radhi kukuacha solemba waende wanakoona ahueni.