Wanawake hawanitaki, nahisi nina mkosi mkubwa

Wanawake hawanitaki, nahisi nina mkosi mkubwa

Salam za wakati huu jamvini, naimani hamjambo na wazima wa afya kabisa na mnaendelea kulijenga taifa la mpate japo kitu kiende kinywani.

Bila kupoteza muda na kuifupisha makala hii, naweza kusema kuwa napitia wakati mgumu sana pale ambapo naona binadamu wenzangu wakidekezana wao kwa kao (male + female).

Mie nchi hii wanawake ndio wameamua kunikataa kabisa najaribu ku approkiach wanawake l ambao wanaonekana kabisa wako tayari kunidate lakini wapi, aisee huu ni mkosi!

Inafikia hadi natumia pesa kuwapata lakini tutadate siku mbili tu halafu haijulikani tumeachanaje.

Ahsanteni, naomba kuwasiliana uzi huu niendelee na Mfungo wa Ramadan.
Pole ndugu Baharia,mabaharia hawakati tamaa na mabaharia hawatumii pesa kwenye hizo mambo,hujenga tu mazingira na akili mingi bila papara.Jua aina ya mtu/binadamu anayekufaa acha haraka wala mihemko,tenga muda wa kumjifunza,anza kupiga kasia mdogo mdogo,kasia ikishika kasi sasa unaweza kushusha nanga😁
 
Ingekuwa ni m'moja au wawili then tungesema hao uliokutana nao wana tatizo. Lakini so far unasema hiyo hali imejirudia mara kadhaa then ni salama kuamini wewe ndie tatizo.

Kaa chini kujitathimini wapi una pwaya. Inawezekana ni muonekano wako sio wa kuvutia, au haiba yako inakera au haivutii kwa mwanamke kuwa na imani ya kuwa na wewe.

Wanawake wanavutiwa na mwanaume yoyote ambaye anaeleweka na anajitambua. Hata kama hana pesa.

Mimi kuna kipindi sikuwa hata na mia mfukoni ila crush za wanawake nilikuwa napata kama kawaida na nilikuwa nafanya kuwakwepa na kuzuia mahusiano maana nilijua sina cha kuwapa ndani ya mahusiano sababu sina uwezo wa kifedha but i was nice and kind to them ili wasishtukie kuwa nawakwepa.

Sasa wewe ukiona wanakimbia jua una shida kubwa sana. Aidha sio msafi wa mwili na kimuonekano so inawapa picha ya aina ya Maisha uliyonayo, au unaongea pumba sana kwasababu haujiamini, au upo aggressive hadi unakera kukuzoea, au upo arrogant sana, kuna sababu inakufanya ukose mvuto.

Kutatua haya acha kutunga majibu nenda kwenye uhalisia ujikague uone wapi unakosea. Kama haupati majibu then anza kujipanga upya.

1. Kuwa msafi wa mwili hadi wewe mwenyewe ukiri kuwa sasa umekuwa msafi wa mwili. Na usiishie tu kwenye mavazi bali hata mazingira yako unayoishi yawe nadhifu.

2. Jiweke karibu sana na imani yako kwa kusoma vitabu vya dini (Bible or Quran) vina mafunzo ya kujenga na vitakusaidia kujenga nguvu ya character yako mpya na kujipa new life goals and purpose.

Unaonekana hauna maisha ndio maana wanawake wanakukwepa. Hata wewe usingekubali kukutana na mtu kasha asie na maisha ndani yake akikuvuta uingie gizani kwenye Maisha yake yasiyo na uelekeo wowote.

3. Tazama matumizi yako ya pesa yaelekeze kwenye vitu muhimu ambavyo vinakupa amani na furaha wewe binafsi sio ununue vitu ili kuwaonyesha watu wakusifie.

4. Improve communication skills zako unaonekana haupo vizuri hilo eneo maana shida ya kwanza kwa wanawake ni kuwasiliana na mtu ambaye skills nzuri za mawasiliano.

5. Tazama ratiba yako kwa siku ina vitu gani hapa ndipo shida kubwa ilipo. Ukitaka kujua mtu ni interesting ama vipi tazama ratiba yake. Ratiba yako inatakiwa iwe interesting hadi mtu atamani kuspend muda na wewe aweze tumia ratiba yako na wewe.

6. Usisahau kula, enjoy chakula sababu ni sehemu muhimu ya maisha. Sasa wewe unaacha kula unawaza mademu. Kula na ikibidi alika mademu mle bila kuwataka kingono uone kama hautawavutia.

7. Usifanye wanawake wawe sababu yako ya kufanya maisha utafeli maana utakuwa ni sawa na mpishi ambaye ana kila kitu jikoni halafu ana vitazama anasubiria vijipike vyenyewe, maana atakesha na hakuna kitakachotokea.

Usisubiri upate mwanamke ndipo uanze maisha tafasiri yake ni kuwa hauna maisha. Na wanawake wa siku hizi hawapendi hiyo kitu kwasababu ni waoga sana wa maisha na wanataka wakute umeshaandaa 80% ya Maisha wao waje kuishi tu. So komaa na life plan yako inayokuhusu ili mwanamke atayevutiwa atakuja, tena watakuja wengi kwa mafungu.


Jikaze kijana acha uzembe na kulainika kama mchuzi wa mlenda wanawake hawapendi hizo habari.
 
Mama Yangu Juzi Kati Hapo Nlimnunulia Ist Kaka...!! Kama ni Baraka (Bless) za Wazee Nnazo Nyingi Tu
Sasa kama unaweza mnunulia mama yako IST ina maana una uwezo wa kufanya Maisha, unafeli wapi? Yaani unashindwa mbinu hata na madogo wanaoendesha bodaboda na bajaji wanapiga pisi kali balaa.
 
Huwezi ukapima baraka au mkosi kwa kukataliwa na wanawake au kupendwa na wanawake.
 
Kaka Kwa Story Nazopewa na Washkaji Zangu Kupendwa na Kudekezwa Inaonekana Dhahiri ni Raha Sana ila Robot Haliwezi Kufanya Hivyo...!! Hii Mada sio Kwamba Nakosa Kudinya ila Love Kama Nayoona kwa Washkaji Hio Mie Sijawai Kuipata Tokea Nizaliwe
Kuna maswali nitakuuliza ukinijibu mimi nitajua chanzo cha tatizo lako.
1.Utanashati wako ukoje kiujumla je ni mtu unajipenda sana kwenye kuvaa au ni mtu wa potelea mbali hata ukivaa kandambili au usiponyoa/kuchana nywele wewe ni sawa tu?
2.Wewe wakati uko mwanafunzi ulisoma katika shule za bweni?
3.Lifestyle yako ukiwa kijana mdogo ilikuwa vipi je ni mtu serious sana?bize sana na mambo yako au ulikuwa ni mtu wa kujichanganya na watu?
4.Je katika maisha yako ya nyuma au ukiwa shuleni ulikuwa unapendelea sana kujihusisha na kujichua/punyeto?
5.Je usiku ukiwa usingizini unaotaga ndoto za kujamiiana mara kwa mara?
6.Na je hao wanawake unaodate nao huwa unawapata kwenye mazingira gani yaani mitaani unakoishi?sehemu za ibada?sehemu za starehe?masokoni?
Kaka Kwa Story Nazopewa na Washkaji Zangu Kupendwa na Kudekezwa Inaonekana Dhahiri ni Raha Sana ila Robot Haliwezi Kufanya Hivyo...!! Hii Mada sio Kwamba Nakosa Kudinya ila Love Kama Nayoona kwa Washkaji Hio Mie Sijawai Kuipata Tokea Nizaliwe
 
Wanawake hawapatani na mtu abaejifanya kidume sana na kujiona eti una ubora kuliko wao.

Pia hawapendi mtu anaejisifu "mimi hivi, mimi vile". Kua "humble".

Wacha mwanamke aamini kua yeye ndio boss na wewe inapaswa uamini kua mwanamke ndie boss, sio wewe.
Hii pia ni kweli wanawake hawapatani na mtu ambaye anaweka nao ligi au kushindana nao kwenye kila jambo ukiwa hivyo wanakutangaza yule kaka anajiona sana,ana mfumo dume,ana gubu na wote wanakukataa hata kama uko na pesa,sanasana wakija wanakula pesa yako siku chache wanapotea.
 
Mwamba kuwa na utulivu ,usijifungie sana ndani.Toka nje ukakutane na watu wazuri.Amini kuna kiumbe kimoja kitakupenda kwa jinsi ulivyo na wala sio hayo matakataka mengine.Niamini.
 
Koo za simba hatuna matatizo hayo.

Tatizo lako umetokea kwenye koo isio-jitambua.
We jamaa una maneno makali sana, na yenye kuchomo moyo wa mtu. Unajua nini mkuu, ulichokiandika ni sawa na kujisifia una mali na zote ni za uruthi. Kama shida ni koo yake, hakuna haja ya kumkebehi wala wewe kujisifia kwa sababu hakuomba kuzaliwa kwenye koo hio nawewe hukuomba kuzaliwa kwenye koo yako. Ni sawa na mtu kuzaliwa kwenye utajiri na mweingine kwenye umaskini. Hakuna aliyeomba azaliwe wapi, tulijikuta tu.

Alichokiomba mtoa mada ni ushari, kama wewe umebaini tatizo ni ukoo basi ungemshauri tu mkuu ili vizazi vyake viepukane na haya. Kila kitu kina mwanzo na yy anaweza kuwa mwanzo mpya
 
Huu uzi ni Chai aisee, hivi inawezekana vipi mwanaume mzima unakataliwa na hawa viumbe in anyway? Eidha utakuwa ni mlugaluga au mtu pori kupitiliza au ni mlemavu.

No way huyu jamaa sio troll.
 
Back
Top Bottom