Wanawake hujifanya wana mood swings na kuitumia kutesa na kupelekesha wanaume mabwege

Wanawake hujifanya wana mood swings na kuitumia kutesa na kupelekesha wanaume mabwege

WANAWAKE HUJIFANYA WANA MOOD SWINGS NA KUITUMIA KUTESA NA KUPELEKESHA WANAUME MABWEGE.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Usikubali mwanamke akupelekeshe kwa kisingizio cha mood swings. Usikubali!

Kuna wanawake Wana tabia ya kupelekesha wanaume wakijifanya ati Wana mood swings.

Mood swings ni hali ya hisia kutokuwa stable yaani kubadilikabadilika kwa Muda mfupi. Mara anakuwa kanuna, Mara anakuwa anahasirahasira, mara anasusa, mara hivi mara vile.

Wanawake wengi hata kama hajakasirika huweza kuigiza amekasirika na kuifanya hiyo kama mood swings yake ya Muda huo.

Wanaume wengi wamejikuta katika mateso hasa wale wanaoendekeza ujingaujinga wa mood swings za wanawake Zao.

Umetoka kazini umechoka, umerudi nyumbani mwanamke muda wote alikuwa na furaha, lakini aliposikia Geti au mlango unabisha anabadilika upesiupesi na kujinunisha, wakati siku nzima alikuwa anacheka.

Ukimuuliza atakuambia ameshinda vibaya, au asikujibu.
Sasa wanawake wa aina hii Sisi tunajua namna ya kudili nao.

Kwanza Kabisa tukishajua mwanamke ni wale wakujifanya Mood swinger's na Sisi tunakuwa mood swinger's zaidi Yao.

Yaani umerudi amenuna wewe unaingia zako ndani ukiwa unaimba haujali Wala nini wala humuulizi chochote. Unaenda bafuni unaoga, unaenda kupakua chakula kidogo Sana, kisha unatoka zako unarudi kitaa.
Ukirudi saa nne sa tano hiyo usiku unarudi umenuna zako unafokafoka mwenyewe vitu havieleweki. Lakini usimshirikishe. Kisha panda kitandani Lala!

Lakini kama utakuwa kama huna Muda na mambo hayo ya kuigizaigiza na michezo ya kaole kama siye. Na kama utakuwa busy Sana na maisha yaani unayachukulia maisha serious saaana! Basi mwambie huyo mwanamke, Tabia za mood swings na wewe ni mbinu na ardhi.
Anamachaguo mawili aache ujinga wake au kila mtu apite Njia yake.

Wanawake wengine hujifanya Hamnazo ndio hao mood swinger's sio ajabu akakutukana au akakupiga Kofi au kukufanyia jambo lolote la aibu alafu utamsikia
Akisema;
" Oooh! Muda ule nilikuwa vibaya, oooh! Mimi nikiwaga na hasira nakuwaga vile. Ooh! Mimi nikikerekaga nakuwaga na mambo ya ajabu"
Usikubali hayo maelezo yake. Piga chini.

Mimi binafsi niliwahi kuwaga na vidada virembo vya aina hiyo ambavyo kwenye mahusiano yao vilikuwa mood swinger's lakini vilipokuwa havikuonyesha hizo Tabia za kijingajinga.

Ni Sawa mtu akuambie demu Fulani anapenda pesa wakati kuna watu wanamla bure tena anatoa kwa ushirikiano wote.

Alafu haohao mood swinger's ndio haohao watakuambia Mimi siwezi kuwa na mwanaume asiye na pesa. N kuna vijana wanahangaika kufa kupona kuhudumia hao viumbe wakati huohuo mwanamke huyohuyo kuna vijana wanampata bila hata mia mbovu.

Mwanamke kama hakutaki mwambie aondoke. Utapata mwingine.
Sio utumie nguvu kubwa na mapesa Mengi kwaajili ya kutuliza mood swings za Mwanamke. Hazitatulia. Unapoteza Muda wako na unajitesa bure.

Narudia, huyo anayejifanya kwako anakisirani, mara kanuna mara kakunyima akienda kwa mtu mwingine anakuwa anaakili timamu. Sasa hizo kama sio dharau kwako ni kitu gani.?

WANAWAKE wanakipaji cha kusoma akili ya Mwanaume. Akishakuweka kwenye kumi na nane zake. Yaani akikubadilisha ukiingia kwenye mfumo wake umekwisha.

Be a man! Usikubali kuwa kama bendera ya mwanamke. Mwanamke Akiwa hivi unafuata. Akiwa hivi unafuata kama bwege!

Hata kama unahela sio kisingizio cha mwanamke kuzitumia kwa ubadhirifu. Hizo pia kwako ni dharau.

Mbona pesa Zao hawazitumii kidharaudharau.

Elewa, mwanamke hawezi kuitumia vibaya pesa ya Mwanaume anayempenda. Weka akilini hiyo.
Lakini ukiona mwanamke Hana huruma na pesa zako ujue anakuona bwege nazi. Danga lake.

Elewa, mwanamke hawezi kuwa na mood swings kwa mwanaume anayempenda na kumhitaji ambaye hataki ampoteze.

Mwanamke huanza kukuchezesha shere akiona Hana chakupoteza, akiona wewe ndiye unampapatikia, akiona wewe ndiye unabahati kuwa naye.

Mwanamke hawezi mchezea chezea na kumletea mahisia mshenzi mwanaume wa ndoto zake. Never ever!

Wanawake wengi huanza kuwa na mood swings wakipoteza hisia na wewe au wakianza ku-cheat.

Mwanamke lazima ajue kuwa wewe ni mwanaume mwenye maamuzi kamili ambaye huna unayemsikiliza na utakayemsikiliza pindi yeye mwanamke akizingua.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Ni mood swings kweli😂😂😂Kuna wakati unakua unajskia kugombana tu mwanaume wako umnunie 😆Yan unakua unatafuta ugomvi makusudi mgombane afu akubembeleze😅😅
 
Wanawake kujinunisha nafikiri ndio asili yao,mi wife tunaweza tusiongee hata week, ila sasa siku nikihamua kumpelekea moto kuanzia asubui na usiku mechi inarudiwa,siku ya pili yake akihamka atatoa nguo zangu zote hata ambazo sivaagi atazifua zote,atasafisha nyumba nzima nje,kwenye kuta, na siku iyo kwa kuwa anajua napenda sana pilau,atalipika la nyama nyingi hata kwa hela yake,



Ila baadae tuliachana ,alinishinda akianza kupayuka mtaa mzima watajua,simu zangu ashavunja nyingi sana
🤣🤣
 
Mi nna pepo la kupenda nadhani au moyo dhaifu, nilihamua kuwa mtu wa ku-hit and run nimechemka, nimenasa kwa mtoto wa kizigua, week iliyopita tumezinguana, akasema kama vipi tuachane, mi nikamuambia poa, kiukweli nilitokwa na jasho baadae, nikimpigia simu hapokei tena, msg hajibu, nikakodi boda hadi kwao kimara usiku wa saa nne, kufika kumuona ndio presha ikashuka baada mzee kuhamua kuwa mpole,


MOyo dhaifu ni hatari sana kwenye mapenzi,, yule mzigua ashagundua udhaifu wangu sasaivi ataniendesha sana, nataka nimuwai kwa sheikh fulani anipe kombe nimsahau nirudi kwenye mfumo wa kula na kusepa(hit &run),
Ha ha ha.....pole Sana mkuu😁
 
Mmm
Wanahitaji maturity kudhibiti hisia zao zisikere watu wengine.

Mbona Sisi tunaishi na hao wanawake hawana hizo mood swings.

Nisikilize,
Mwanamke wakati wa mabadiliko ya homoni yanayotokana aidha kwa desturi ya hedhi au Mimba hudhihirisha hisia zake juu yako.

Yaani kile mwanamke anachoonyesha wakati anapokuwa na hormone changes ndicho Halisi ambacho alikuwa anakuficha wakati Akiwa kawaida.
Mmh kwani wewe ni mwanamke hadi ujue kwamba anadhihirisha? Hiyo atakuwa ni mwanamke wako usituchoshe
 
Mimi bwana ndo Nna hizo mood swing kuna siku naamka sielewi kabisa utafikiri nimekula bhange mama mtu anajibebisha ila muhuni full ndita utamsikia "Wa......... wamekutembeleA"Hapo ametaja kabila langu.
Aisee sipendi mwanaume anayejinunishaa
 
Back
Top Bottom