Wanawake jifunzeni kuwatunza na kuwaheshimu wafanyakazi wenu wa ndani yasije kuwatokea haya anayopitia mzazi mwenzangu

Wanawake jifunzeni kuwatunza na kuwaheshimu wafanyakazi wenu wa ndani yasije kuwatokea haya anayopitia mzazi mwenzangu

Ni dhahiri kuna baadhi ya watu hata ukiwastili vipi au kuwaheshimu vipi au kuwasaidia vp ipo siku watukufanyia ubaya tu bila sababu ya msingi. Lakini hilo lisiwe ndio chachu ya kuwatendea wengine mabaya, ni bora uwe neutral (mtu wa haki sio mtu wa favors) kuliko kuwa negative.

Hii ni kwa wanawake / wake zetu, msiwatese hawa mabinti wa kazi kwa kisingizio kwamba hawanaga shukrani, nenda nao kwa haki kama ukishindwa kuwapa favors, kwa haki namaanisha akizingua mzingue(in mama Samia voice), lakini asipozingua hamna haja ya kumuwekea wakati mgumu.

Kipindi nimemaliza kujenga huyu mwanamke ndo alikua amenizalia mtoto wa kwanza, nimuite tu mke wangu japo hatujafunga ndoa na sina mpango huo ila namjali kwa kila kitu na huwa ikitokea event wakataka double basi namchukua yeye.

Sasa huyu mama bwana alikua anamtesa kweli mfanyakazi wetu enzi hizo, yeye alikua mama wa nyumbani, yule binti alikua kamaliza form 4 kapata div 3 ila kwao wakashindwa kumsomesha, mimi nafahamiana na mjomba wake hivo ikabidi binti aje nyumbani pale awe anamsaidia kazi mke wangu.

Binti alikua mzuri na mwelewa sana, lkn mke wangu alikua anamuwekea visirani balaa. Huwa nna kanuni mambo ya nyumbani siingilii kabisa, namuachia yeye, hivo akawa anatumia huo mwanya kumtesa sana dogo.

Siku za sikukuu hata hapewi hela extra akanunue nguo, nyumba nzima nakuta wamependeza lakini binti kavaa matambara tu, **** sikukuu moja nilipata hasira nikamchukua yule binti baada ya kula nikaenda kumfanyia shopping ya nguvu. Mke wangu alikua na mdogo wake hapo nyumbani niliporudi wakawa na aibu tu wako kimya. Kumbe nilikosea sana, nilivyorudi dsm kikazi yule binti aliteswa pale hadi siku moja akanipigia simu kwa kuazima akiwa analia kweli.

Mimi nikaona isiwe kesi sababu nilikua nishamuonya mke wangu amchukulie huyo binti kama ndugu yetu ila hasikii, nikaona nitatue kiakili bila kuharibu uhusiano wangu na ndugu za huyo binti hasahasa mjomba wake,l.

Sasa nikaongea na mjomba wake kiakili tu kwamba huyo binti hawezi kuwa housegirl kwa muda mref wakati amesoma, hivo nikamtafutia kazi kwa marafiki hapa dar. Nlipoipata ile kazi nikaongea na mke wangu kwamba huyo binti wamruhusu mjomba wake anamtaka arudi kwao, lkn kumbe nishamwambia mjomba wake amchukue amlete dar aanze kazi. Nilifanya hivo ili upuuzi wa mke wangu usiharibu mahusiano yangu nae pale nyumbani na pia usiharibu mahusiani yangu na ndugu wa yule binti. Na nilichompendea yule binti nadhan hakuwahi kuwaambia ndugu zake mateso alokua anafanyiwa na mke wangu, ndo maana huyu binti namsifu ni mwelewa sana, hata kumtafutia kazi nilikua nna uhakika hatofanya ujinga ujinga.

Binti bwana baada ya kupata kazi kakomaa, sijui ikawaje huko akapata zari la mentali(in prof J's voice) kafungua kijihoteli, baadae akaongezea na duka la nguo. Ninavyoongea hivi huyu binti anajenga sasa hivi nyumba yake kubwa tu huko mwanza na ni mtaa mmoja na mimi nilipojenga, binti ana Murano yake ya brown.

Sasa mke wangu alipojua mjengo ule ni wa huyo binti akaanza kutafuta umbea akajua binti ana gari basi imekuwa kesi, mwezi wa pili huu ananililia nimnunulie gari na bila aibu anasema eti "Hadi aliekua mfanyakazi wetu ana gari ila mimi hutaki kuninunulia"

Wanawake zetu, haya maisha usije ukamdharau mtu, hasa housegirl alio na kielimu kiasi, wanapinduaga meza hawa, mateso mnayowapa ndio fuel ya wao kuhangaika, wakushikwa mkono kdg tu wanatoboa.

Na huyu binti atafika mbali sana sababu ni mwelewa na ana moyo mpana sana, huwa natamani hata ningemuoa lkn haiwezekani(NB sijawahi hata kumla kumasikhara kama wengi mnavyoweza kudhani, kwangu mm ni kama ndugu kabisa). Yan nikifika hotelini kwake huwa nakula bure, dukani kwake tukipishana lazima anipe nguo za watoto bure namtumia mke wangu mwanza na sijawah mwambia mke wangu zinapotoka.

Alamsiki
Mwanamke akipata power kidogo,huwa ni waovu kupitiliza,the best version ya mwanamke huwa inakuja akiwa mama yako otherwise ni shida
 
Hata hao dada wa kazi wakiolewa nao huwa ni watesaji wakubwa sana wa dada wa kazi.
 
Hio inatokea hasa mwanamke akulie kwenye maisha ya kawaida alafu aolewe sehemu ambayo kila kitu kipo ni anapokea tu, majivuno, uchoyo na dharau huwa ndo vinamuongoza
 
Kwani unashindwaje kumfanya kama ndugu yako,ni kitu gani anapunguza hapo nyumbani
Mie kwangu ni msaidizi wa kazi ambazo siwezi kufanya au nikiwa nimechoka but yule humchukulia kama msaidizi tu

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Hio inatokea hasa mwanamke akulie kwenye maisha ya kawaida alafu aolewe sehemu ambayo kila kitu kipo ni anapokea tu, majivuno, uchoyo na dharau huwa ndo vinamuongoza
Kweli kabisa, wengi wa hivyo huwa ni shida. Alokulia kwenye hela mara chache sana kukuta ana visirani na watu wengine ila wewe mpenzi wake ndo utaisoma namba, hizo deko na wivu jiandae aisee
 
Wanawake hawajuagi hata Masuala ya kiusalama wa Familia yako Dada wa kazi ana Access kubwa mno ya kufanya chochote hata akiamua kuwawekewa Sumu kwenye msosi Familia nzima mnalala mazima Safari kwa Muumba msiwatese hao watu kumbukeni ndio wameshikilia uhai wa watoto wenu muwapo nyie Makazini huko...!
 
Kweli kabisa, wengi wa hivyo huwa ni shida. Alokulia kwenye hela mara chache sana kukuta ana visirani na watu wengine ila wewe mpenzi wake ndo utaisoma namba, hizo deko na wivu jiandae aisee
Hao waliokulia kwenye hela sijawah kuwaona boss 😀 nakutana na hawa middle class ingawa sio mbaya [emoji4]
 
Hao waliokulia kwenye hela sijawah kuwaona boss 😀 nakutana na hawa middle class ingawa sio mbaya [emoji4]
madem walokulia kwenye hela wako tofauti sana, especially ukute sio muhuni, utafanya upuuzi wote, showoffs zote ila anakushangaa tu, hv unajua umaskini ndo chanzo cha chuki na visasi, na chuki na visasi ndo vinatengeneza roho mbaya. Sasa hawa hawajui hata umasikini ni nini, wanausikiaga tu
 
Mateso na roho mbaya za watu huwafanya watu wa chini wawe na nidhamu katika utafutaji

Na ndivyo ilivyo watoto/watu waliotoka katika hali ya chini asilimia kubwa huwa na nidhamu sio tu matumizi hata kimaongezi pia they are ethical, tofauti na watu waliozaliwa wakutane na mali na wanaishi kwenye hizo mali ni wachache ambao wana adabu (good ethics)
 
Roho mbaya tu ya mke wa bamkubwa nilikuwa naaminika na kupendeka kwa mshua, basi nilipata tabu ya kutosha ila nowdays anavyojifanya kunijali sasa😂😂
Wala hakujali bali ni mnafiki tu tena akiona maokoto yapo ndio kabisa anakuwa mnafiki wa kiwango Cha first class
 
Back
Top Bottom