Wanawake jifunzeni kuwatunza na kuwaheshimu wafanyakazi wenu wa ndani yasije kuwatokea haya anayopitia mzazi mwenzangu

Wanawake jifunzeni kuwatunza na kuwaheshimu wafanyakazi wenu wa ndani yasije kuwatokea haya anayopitia mzazi mwenzangu

Wanawake wengi nimeona hawakai na wadada wa kazi kwa mda mrefu. Mimi binafsi nimekaa na mabinti wawili tu, wa kwanza alienda olewa wa sasa ninae hana hata mpango wa kuondoka na ni jembe kweli kweli. Mtu akija kwangu hawezi baini mapema yupi ni housemaid na yupi siye. Yuko responsible naishi nae km binti yangu kabisa na madogo wasipomuona kwa 20min lazima ugombane nao.

Nilichojifunza: ukiona binti yuko vizuri mpe outonomy ya kufanya shughuli zake, akikosea usilalaame muelekeze maisha yaendelee.

Sikatai kuna wengine ni vichomi ila ukimpata walau mzuri mtengeneze unavyotaka mjali muamini.
Hawawezi upo sahihi. Kuna tension fulani ya kuonesha umaza house ambayo sio ya lazima
 
Kabisa.

Kuna baadhi ni majembe.

Mimi huyu hadi kuchukua risk ya kumtafutia kazi kwa watu nnaoheshimiana nao nilijua kabisa hatoniangusha sababu kwa siku chache nilizokua nakaa pale nyumbani nilimuona tu, kastaarabika na anajielewa, atakae muoa aisee kaula
Nipe namba yake PM mkuu
 
Unamtesa mtoto wa watu, mara fimbo mara makofi mwishowe afe afu ufie jela kisa ujinga tu. Alafu bado huyohuyo unaemtesa unamuachia akuangalizie vifaranga vyako ukienda kutafuta mia mia zako. Hivi hizi akili huwa zikoje jamanii???

Tangia udogo wangu mbaka utu uzima sijawahi ona msaidizi wa kazi akipigwa. Nimeona juzi kwa macho yangu. Alooo nilifuraaaa, nikasimama katikati. Unajua mbaka mwili unauma kwa zile hasira mana kumuonea mtu kisa yupo kwako na unaona hana msaada basi kwako faida etiii!!!

Kama wapo wamama wa staili hizi waache huu ujinga. Sio sawa hata kidogo. Mtoto wako nawewe anakua hujui kesho atakaa kwa nani. Vipi uone anapigwa kama wewe unavofanya kwa watoto wa wenzio???

Ni kweli wapo wengine hawana adabu na vijitabia vya hovyo. Mrudishe alipotoka uendelee na mambo yako. Ila ujinga wa kutesa watoto wa watu sio sawa kabisaa.

Ova
 
Kwa kweli madada wanapaswa wapewe maua yao. Wazazi wengi tunafeli kuwanyanyasa madada wa kazi lkn hatuoni umuhimu wao.

Binafsi ninaishi na mdada ki ukweli namlea kama binti yangu. Licha ya mshahara namnunulia mahitaji yote ya mtoto wa kike. Na ikitokea familia yake inachangamoto basi natoa msaada.
Na mwezi uliopita nilijikusanya nikamnunulia simu ya laki mbili na nusu. Sifanya haya kwa sababu nina kipato kikuba la hasha natambua thamani yake ya kunilelea mwanangu wakati mimi sipo.

Kuna siku nilisafiri kikazi kufika usiku wa manane dogo kaanza kutapika,,,akachukua kadi ya mtoto akampeleka hospitali hapo kanipigia simu sijapokea nami simu nilikuwa nimeweka chaji. Kulipokucha ndo nikampigia akanipa taarifa hizo.

Japo si wadada wote wanajielewa lakin kama alivyosema mtoa mada tuishi nao kwa haki kwa sababu nao ni binadamu.

Mungu awabiriki wote wanaowatendea vizuri wadada na kuwachukulia kama sehemu ya familia yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kweli madada wanapaswa wapewe maua yao. Wazazi wengi tunafeli kuwanyanyasa madada wa kazi lkn hatuoni umuhimu wao.

Binafsi ninaishi na mdada ki ukweli namlea kama binti yangu. Licha ya mshahara namnunulia mahitaji yote ya mtoto wa kike. Na ikitokea familia yake inachangamoto basi natoa msaada.
Na mwezi uliopita nilijikusanya nikamnunulia simu ya laki mbili na nusu. Sifanya haya kwa sababu nina kipato kikuba la hasha natambua thamani yake ya kunilelea mwanangu wakati mimi sipo.

Kuna siku nilisafiri kikazi kufika usiku wa manane dogo kaanza kutapika,,,akachukua kadi ya mtoto akampeleka hospitali hapo kanipigia simu sijapokea nami simu nilikuwa nimeweka chaji. Kulipokucha ndo nikampigia akanipa taarifa hizo.

ok ok ok, kuna huyu anakaa kwa bi mkubwa, simpendi simpendi, kazi kufokea wajukuu na kuwatumatuma tu, yaani analipwa ila hata kitunguu ni mjukuu akate yeye kakalisha makalio tu, mpaka wajukuu huwa hawaentoy likizo zao kwa bibi
 
Back
Top Bottom