Wanawake mnaojenga nyumba kwa siri bila mwenza kujua huwa mnamaanisha nini?

Wanawake mnaojenga nyumba kwa siri bila mwenza kujua huwa mnamaanisha nini?

Jamaa yangu inno wa moshi aliishi na mke wake kwa furaha, wakafanikiwa kufungua kampuni ya Utalii , mke akaanza usiri kwenye mambo yake akaanzisha biashara ya kuuza bidhaa nje ya nchi, zile bidhaa akawa anazitangaza export hub , globy (B2B) , ikawa Siri kweli baadae biashara ya Utalii ikayumba mke kajikausha , baadae inno akagundua mke alikua kwenye biashara , nzuri Tu na haukusema na mke alipobanwa ndio akatoboa Siri lakini biashara yake ikiwa imeyumba tayari, inno akajifunza ubinafsi mkubwa wa wanawake hadi Leo hawezi kuweka wazi mambo yake kwa mwanamke.
 
Sina jibu la moja kwa moja ya swali hili.
Kwa upande wangu siwezi kumfanyia hivi mtu niliyenaye kwasababu hela zake nazitumia nitakavyo halafu sio mchoyo.
Hela zangu tutazitumia wote hata nikipata kazi akitaka na mshahara wangu nitampa kila mwezi.
Huwezi,utaanza mwanzoni wakati mmekodi nyumba mkishajenga tu ubinafsi unaanza baada ya security!
 
Kuna jamaa yangu alimshtukia mkewe ana kibanda cha room 3 na kajenga kimya kimya. Kilichomfanya aanze kufanya uchunguzi ni mke kuanza kuwa jeuri kupitiliza. Alitafuta wahuni wakakivunja usiku, dada wa watu alitumia wiki kama mbili anaongea kwa ukwali huku akitema mate kama cobra bila kueleza kipi kimemkuta.
Huyo mwamba ni gaidi 😂
 
Sina jibu la moja kwa moja ya swali hili.
Kwa upande wangu siwezi kumfanyia hivi mtu niliyenaye kwasababu hela zake nazitumia nitakavyo halafu sio mchoyo.
Hela zangu tutazitumia wote hata nikipata kazi akitaka na mshahara wangu nitampa kila mwezi.
una uhakika? mshahara utauweka mezani? au haya ni maneno kabla haujaolewa?
 
Back
Top Bottom