ephen_
JF-Expert Member
- Oct 28, 2022
- 14,949
- 54,485
Tena wanaume wengi akijitahidi sanaa kuhudumia mtoto basi atamlipia ada tu, kuhusu kula, mavazi, afya jukumu anaachiwa mwanamke.Hivi ni kweli hamna uelewa wa haya mambo ya migogoro ya kifamilia na kadhia za talaka au kutengana.
Wanaume wangapi wanaendelea kuhudumia watoto ipasavyo baada ya ndoa kuvunjika na bila kushurutishwa na ustawi wa jamii au mahakama? Wapo ila ni wachache, wengi wanaamini mkiachana jukumu la watoto ni la mama.
Ndoa ikivunjika, taratibu za kutafuta mpaka kupata talaka inaweza kuchukua miaka. Hicho kipindi chote hao watoto uliomwachia mkeo wanaishije? Kama mke hajasimama kiuchumi ni either watoto watateseka au atarudi kwao kusaidiwa kulea na ndugu zake.
Naona kama majadiliano mengine tunalazimisha tutoke nje ya maisha yetu ya kiuhalisia kwenye jamii.
Kuna shida kubwa sana ya malezi ya watoto na mwanamke kwa kiwango kikibwa ndiye anayeathirika ndoa ikivunjika. Sheria za mgawanyo zimewekwa ili kulinda maslahi wa wanandoa wote na watoto. Kisheria, ni kosa kuidanganya mahakama na kuficha mali iwe amefanya mwanamke au mwanaume.
