joseph1989
JF-Expert Member
- May 4, 2014
- 17,420
- 35,765
Mhhh mwanamke anaweza akadai hela ya matibabu aliyo mtibia mtoto wake na hapo utakuta jamaa kasafiri labda kwa wiki kamwachia laki mbili na nusu ,moja na nusu ni matumizi,moja ni ya ziada .Ila mtoto akiumwa ukakuta labda matibabu yake alitumia elfu 30,siku mumewe akirudi atadai elfu 30 akisahu kuwa lipewa laki moja ya ziada.Na ndio maana tukiachana tunataka tugawane mali zenu nusu kwa nusu.
Sababu mwanaume akipata 30,000 nyumbani analeta 20,000 nyingine anampa mchepuko.
Mwanamke akipata 30,000 yote anaitumia kwake na watoto.
Nina mfano huo hata sijasimuliwa jamaa yangu dereva wa bajaj,kakesha usiku ila usiku huo biashara ilikuwa sio nzuri karudi night kali,anahelaya kula tu yy na familia yake. Asubuhi mkewe anamuamsha anataa hela ya pampas jamaa akamwambia jela ana,ila amfunge mtoto na vikanga mchana akiingia road atamtumia,demu akawa analalamika mara kanga sijui style za kizamani ila akakubali kwa shingo upande. Sasa akatoka kwenda kunua vitafunio na jamaa mda huo kaamka anaanza kutafuta simu yake,katafufuta weee,baadae akaanza kupekua kabatini kaanza upande wake wapi hakuiona,akasema labda atizame upande wa mkewe kupekua pekua anakutana na 1.2m,jamaa alichoka. Mkewe kurudi home anamuuliza hii 1.2m umeipata wapi, akadai alipewa na baba 1.5m baada ya mzee kuuza kiwanja chake, laki tatu alitumia (matumizi yenyewe hayaeleweki) ndio ikabaki hiyo 1.2m,sasa pata picha kwenye 1.2m anashindwa kutoa mia tano ya pampas kwa ajili ya mtoto.
Shukuruni tu wanaume kiasili sio waongeaji kabisa, mengi tunamezea tu.