Wanawake mnaojenga nyumba kwa siri bila mwenza kujua huwa mnamaanisha nini?

Wanawake mnaojenga nyumba kwa siri bila mwenza kujua huwa mnamaanisha nini?

wanamaanishi kwamba
Nataka kujua ndio ujanja,umaarufu,ukisasa, usomi,kiburi,majigambo,majivuno,dharau,umwamba au!!?

Na tena wakati unafanya hivyo upo kwako na mlishajenga pa kuishi,na mwenza anakushirikisha Kila jambo la kifamilia analofanya!

MSAADA TAFADHALI,sio kwamba natumika baadae nitangulizwe baada ya mpangokazi wake wa ukwasi kukamilika!

Maoni yenu nitayazingatia!

Kataa ndoa mje pole pole!!

Na wale waume wenza mliopo humu mje pole pole nawajua!
wanamaanisha kwamba "CHAKE CHAKE,CHAKO CHAKE"
 
Kulipa Alimony au huduma za watoto siyo gender specific, yule mwenye kipato kikubwa au mali zaidi hua anamlipa mwenzake.

Kama kweli unazungumzia uhalisia, hizi ni case tatu kati ya nyingi za marekani ambazo wanawake waliamriwa kuwalipa Alimony wanaume.
  • Britney Spears - Aliamriwa kumlipa $20,000 kwa mwezi kwa ajili ya matunzo ya watoto kwa mume wake wa zamani, Kevin Federline, baada ya talaka yao mnamo 2007.
  • Mary J. Blige - 2018, aliamriwa kumlipa aliyekuwa mume wake, Kendu Isaacs, $30,000 kwa mwezi kama alimony baada ya talaka yao. Huyo mumewe alikua ameomba alipwe $100,000 kwa mwezi mahakama ikakataa.
  • Halle Berry - alilamriwa kumlipa aliyekua mpenzi wake Gabriel Aubry $16,000 kwa mwezi kwa ajili ya matunzo ya mtoto wake. Huyu hakuwa mume bali mpenzi waliyezaa pamoja.

    Kwenye swali lako la pili, ni kosa kisheria kwa mwanamke (au mwanaume) kuficha mali na kung'ang'ania kugawana mali za mwenzake tu, ikigundulika unachukuliwa hatua za kisheria. Huko Marekani, divorce lawyers huwa wanatafuta forensic accountants au financial experts kwa ajili ya kuchunguza mali kabla ya mgawanyo.
By 2013 ni asilimia 3 tu ya wanaume US ndio walikuwa wana receive Allomony na unaweza ukakuta hata sasa haijafi 5,ila zaidi ya asilimia tisini ya Allomony US wanapokea wanawake na kama hujui ,US wanaharakati wanao ongoza kupigania uonevu zidi ya wanaume ni wanawake ambao wengi wao ni wanasheria wa talaka au mafenist ambao mitizamo yao imebadilika baada ya kupata watoto au wajukuu wa kiume? Ushajiuliza ni kwa nini,wanawake wenzenu ndio wanao pambania haki za wanaume?
 
Na ndio maana tukiachana tunataka tugawane mali zenu nusu kwa nusu.

Sababu mwanaume akipata 30,000 nyumbani analeta 20,000 nyingine anampa mchepuko.
Mwanamke akipata 30,000 yote anaitumia kwake na watoto.
Watoto??? :AYOOO: :AYOOO:
 
Jamaa yangu inno wa moshi aliishi na mke wake kwa furaha, wakafanikiwa kufungua kampuni ya Utalii , mke akaanza usiri kwenye mambo yake akaanzisha biashara ya kuuza bidhaa nje ya nchi, zile bidhaa akawa anazitangaza export hub , globy (B2B) , ikawa Siri kweli baadae biashara ya Utalii ikayumba mke kajikausha , baadae inno akagundua mke alikua kwenye biashara , nzuri Tu na haukusema na mke alipobanwa ndio akatoboa Siri lakini biashara yake ikiwa imeyumba tayari, inno akajifunza ubinafsi mkubwa wa wanawake hadi Leo hawezi kuweka wazi mambo yake kwa mwanamke.
Hii muhimu, mwanamke sio wa kumuambia kila kitu
 
By 2013 ni asilimia 3 tu ya wanaume US ndio walikuwa wana receive Allomony na unaweza ukakuta hata sasa haijafi 5,ila zaidi ya asilimia tisini ya Allomony US wanapokea wanawake na kama hujui ,US wanaharakati wanao ongoza kupigania uonevu zidi ya wanaume ni wanawake ambao wengi wao ni wanasheria wa talaka au mafenist ambao mitizamo yao imebadilika baada ya kupata watoto au wajukuu wa kiume? Ushajiuliza ni kwa nini,wanawake wenzenu ndio wanao pambania haki za wanaume?
Tafadhali ambatanisha na takwimu za asilimia ngapi ya wanawake waliotalikiana mpaka mwaka 2013 walikua na kipato cha juu kuzidi wanaume. Asante!
 
Nataka kujua ndio ujanja,umaarufu,ukisasa, usomi,kiburi,majigambo,majivuno,dharau,umwamba au!!?

Na tena wakati unafanya hivyo upo kwako na mlishajenga pa kuishi,na mwenza anakushirikisha Kila jambo la kifamilia analofanya!

MSAADA TAFADHALI,sio kwamba natumika baadae nitangulizwe baada ya mpangokazi wake wa ukwasi kukamilika!

Maoni yenu nitayazingatia!

Kataa ndoa mje pole pole!!

Na wale waume wenza mliopo humu mje pole pole nawajua!
Aisee inasikitisha...
 
Kama akili zenyewe ndio hizi acheni tu vijana wa siku hizi wawe wagumu kuoa.Sasa mtu yupo kwenye ndoa anatelekeza vipi mtoto? Ila cha ajabu siku wakija kuachana zinagawanywa na mwanaume ila mali a mwanamke haziguswi,halafu kesho mnalamika mnataka 50/50 ,haki sawa ila vya kwenu hamtaki usawa.

Kama bado unaroho ya UBINAFSI ndoa haikufai achana nayo, endelea kukaa mwenyewe ujenge nyimba zako ,ufungue biashara zako uendelea na maisha yako binafsi.
Nyinyi wanaume ndiyo mnasababisha wanawake wawe hivyo.
 
Hivi ni kweli hamna uelewa wa haya mambo ya migogoro ya kifamilia na kadhia za talaka au kutengana.

Wanaume wangapi wanaendelea kuhudumia watoto ipasavyo baada ya ndoa kuvunjika na bila kushurutishwa na ustawi wa jamii au mahakama? Wapo ila ni wachache, wengi wanaamini mkiachana jukumu la watoto ni la mama.

Ndoa ikivunjika, taratibu za kutafuta mpaka kupata talaka inaweza kuchukua miaka. Hicho kipindi chote hao watoto uliomwachia mkeo wanaishije? Kama mke hajasimama kiuchumi ni either watoto watateseka au atarudi kwao kusaidiwa kulea na ndugu zake.
Naona kama majadiliano mengine tunalazimisha tutoke nje ya maisha yetu ya kiuhalisia kwenye jamii.

Kuna shida kubwa sana ya malezi ya watoto na mwanamke kwa kiwango kikibwa ndiye anayeathirika ndoa ikivunjika. Sheria za mgawanyo zimewekwa ili kulinda maslahi wa wanandoa wote na watoto. Kisheria, ni kosa kuidanganya mahakama na kuficha mali iwe amefanya mwanamke au mwanaume.
Uko sahihi kabisa.....Ngoja nikuuulize swali jepesi umefanya utafiti kwa kiwango gani kutambua kwamba wanaume weeng japo sio wote wakitelekeza familia linakuwa jukumu la mama kulea ...

Mahakamani ukitokea mtafaruko WA kugawana Mali inakuwaga 50/50 ...Ila mgawanyo huegemea upande WA mwanaume Sana Sana na huduma juu bado atoe Huoni kama kuna upendeleo fulani ambao huwapa kiburi wanawake?

Ubinafsi tunaugongelea pia katika malezi mkiachana lazima mama Ampandikize Sumu mtoto huo ni ubinafsi bado kwasababu matumizi Yao baadhi wanapata kwa mzazi WA kiume
 
Nataka kujua ndio ujanja,umaarufu,ukisasa, usomi,kiburi,majigambo,majivuno,dharau,umwamba au!!?

Na tena wakati unafanya hivyo upo kwako na mlishajenga pa kuishi,na mwenza anakushirikisha Kila jambo la kifamilia analofanya!

MSAADA TAFADHALI,sio kwamba natumika baadae nitangulizwe baada ya mpangokazi wake wa ukwasi kukamilika!

Maoni yenu nitayazingatia!

Kataa ndoa mje pole pole!!

Na wale waume wenza mliopo humu mje pole pole nawajua!
Hili wanalo hasa wanawake wa kiswahili. Uswahilini huwa wanawake wanaambiana mume anaweza kukuacha muda wowote hivyo ni lazima ujiandae. Ila ni tabia ya hovyo sana na ukiona mwanamke kafanya hivyo basi ujue hakuamini wewe na anajindaa kuvunja ndoa siku yoyote mambo yake yakikaa sawa. Tena wanawake wa aina hii wanakuwa jeuri sana wanapokuwa wamemamaliza nyumba.
 
Mimi mama yangu kajenga mikoa tofauti na hadi mshua anaenda kaburini hajui lolote. Wakati wa uhai wake kampiga sana matukio hataki afanye kazi na hataki awe na maendeleo yoyote eti mke wa mtu na alimkuta kasoma na ana kazi tayari. Mtu hawazi ya mbele na ukoo wake ni ule wanaamini cha ndugu yoyote ni cha ukoo mzima. Akaona isiwe kesi katafuta mahala pengine kimya kimya. Na mzee alipofariki tu fujo zikaanza haya niambie kama hakua kajiongeza mapema hali ingekuaje.
Sasa mfano Kelsea hayo umeyashuhudia Mama yako akifanyiwa na Baba yako. Kesho unakutana na mwanaume anakuoa anakwambia uache kazi utakubali?
 
Tafadhali ambatanisha na takwimu za asilimia ngapi ya wanawake waliotalikiana mpaka mwaka 2013 walikua na kipato cha juu kuzidi wanaume. Asante!
Women are still the primary alimony recipients, but the number of men who receive alimony from their former spouses is increasing. According to the 2000 census, 0.5 percent of alimony recipients in the United States were male. By 2010, 3 percent of the 400,000 alimony recipients in the country were male.

Correction ni 2010 na si 2013.
 
Back
Top Bottom