Ertugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 14,705
- 30,041
Sifa ya Ego ni ya mwanaume na si ya mwanamke, mwanaume ndio mwenye ego ya mamlaka na uongozi kwenye ndoa
Hivyo basi mwanamke anapotaka kuchukua nafasi ya mwanaume na kuleta zile habar za 50/50 hapo anakuwa amevuka mstari mwekundu na kutikisa himaya ya mwanaume
Ndio maana ndoa yoyote ambayo mwanamke anajaribu kuchezea sharubu za mwanaume lazima ndoa hiyo itakuwa na mushkeli tu unless huyo mume aamue kumeza ego yake na kujifanya kama hakuna kitu chochote kinachotokea.
Ladies just know that ego is for men and not women.
Mnaweza kuwa na ego katika biashara au kwenye makumpuni,huko ndio mnapoweza kuwa na ego ya mamlaka na uongozi na 50/50 lakini sio kwenye ndoa zenu
Ukitaka kuwa na ndoa nzuri kama walizo kuwa nazo baba na mama zetu kuwa mke msikivu na muheshimu mumeo hiyo ndio njia pekee na uamuzi bora wa kuufanya
Ni hayo tu!