Wanawake muelewe hili, wanaume wana maumivu pia, tena yenye huzuni karibu ya kifo

Wanawake muelewe hili, wanaume wana maumivu pia, tena yenye huzuni karibu ya kifo

Wanaume tuna maumivu kweli ila kulialia sio mchongo.

Mwanaume wa kiafrika lazima uuvae ubandidu. Sisemi wasizungumze na wenza/familia zao mambo yanayo wasibu la hasha ila usijilegeze sana, hata ukilia kama mtoto maisha ni magumu and it's gets even tougher kila siku.

Hizi kampeni za siku hizi za kutaka wanaume wajilize na kutema nyongo zao kama wanawake on regular is feminization of a black man na mimi nasimama nayo kinyume.

Carleen eti laazizi nianze kulia lia?
Bufa laazizi usilie lie ila kulia mara moja inapunguza machungu, na si wajua sintokufuta machozi bali nitalia nawe.??
 
Matatizo mengi mnayasababisha wanaume Kwa kukosa uaminifu na kuchepuka.

Mwanamke mwingine akishapoteza imani Kwa mumewe hawezi kumuamini tena mume wake, sasa hapo patakuwa na penzi tena ?

Ishini na wake zenu kwa akili na sio hisia wala maombi
 
Sasa hayo yanatoka wapi wakati nyie mnaonaga ni wajanja kwenye ndoa kwa kuchepuka?

Si mnashaurianaga Eti mfanye mkeo awe nyumba kubwa mpandishe cheo,

Huko kwa hawara zenu mnakochepuka si mkapate furaha huko ?

Au haitoshi?
 
Ndio maana kama wanandoa mnaona upendo umekwisha afadhali kuachana,

Ingawa inamchukiza Mungu,

Lakini hajakataza kuachana,

Kwanini muishi maisha ya sonona na kuvumiliana?

Kama umeona you have been honest hujawahi ku-cheat isipokuwa mke ni Mkorofi tu umeongea naye hataki kubadilika umeongea na wazazi wake ukute nao wanamuogopa kumuambia ukweli,

Kaitafute furaha yako lakini baada ya kuachana rasmi.

Provided umekuwa honest kwa kipindi chote.
 
Because for the matter of facts kuna wanawake wakorofi by nature pia,

Hata kwao walikotoka waliposikia mtoto/ndugu yao anataka kuolewa walijisemea bora vikaonekane mbele ya safari.

Sasa unategemea nini?!
 
Tena hawa walozaliwa miaka ya 2,000 ndio worse kabisa.

Hawajui kitu kuwa humbled,

Kanuni ya msingi ya mke ni utii Kwa mumewe Kwa kila jambo kwa mujibu wa Maandiko Matakatifu,

Sasa binti/mwanamke wakati yuko kuji-defend zidi ya kila mume anachomuelekeza,

Hajafundishwa jinsi ya kuishi na mume.

Hajui ku-admit makosa.

Unategemea nini.
 
Ndoa nyingi watu wanaishi kimkanda mkanda tu!

Lakini mkiona hupati furaha Kwanini uishe kwa ku-pretend?!
 
Wengine wanazani wanafuraha sababu one part is not well informed of what is going on to the other side!

Na kwa bahati nzuri Duniani hakunaga Siri ni swala la muda tu.

Kwa hiyo jiandae kwa matokeo!
 
Hayo nitayaelewa Kwa Mwanaume ambaye yuko honest Kwa mkewe tu lakini Kwa Mwanaume bandidu mchepukaji wala!
 
Weeee! watoto wanililie!! ....... na zee zima!! lenye mindevu kila mahala nalo lini lilie!!! mweee! ntakupiga mitama ukalilie huko mbele vizuri!!....tafuta pesa nile na watoto Nyambaf!!! nacho fanya mie nikukuombea tuuu!!

km huwezi kwanini uliwowaa?? au laa acha niache nisepe zangu uone km ntakufa !!...mnajifanya kuwowa kuumbe hamana kitu!! kaa ivovivo!!
Sema we mwanamke una mdomo sana

Ila cha ajabu nakuwa turned on na Maneno yako machafu

Is that weird ?
 
Sema we mwanamke una mdomo sana

Ila cha ajabu nakuwa turned on na Maneno yako machafu

Is that weird ?
Jamani!! kuwakumbusha wajibu wenu siyo maneno machafu! niombe samahani!! aliye sema ''mtakula kwa jasho lenu'' .... siyo mie!.. mnamjua fika!!.....kosa langu mie nini?? hadi unihukumu ivo?? usijitoe ufahamu???...na bado..

kazi yangu mie ni kuzaa kwa udhuungu!! baasi!! mbona hunihurumii?? mkuu usikwepe, Beba zigo lako babu!! hata usemeje hkn unafuuu!! ndo unajirogaaa!...jitahidi uwezavyo upende kazi hata za hovyo weye fanya tu! ili mradi dumekazi.

kwanza! dume Hutaki fanya kaziiii '' Rhuksa kwa sirikali olewa!! saabu mnamatumizi mbili Front side na Back side? ni me' wengi tuu walioshindwa kazi wanageuzwa!! lengo ni ili upewe Km mie navopatiwa!! km unaona wivu navopewa!!!

Onyo tu! nisijue kuwa kunguru wa manzese anashikishwa!...nikijua utayamba kifukuto!
 
Tabia yetu wanaume ya kuficha maumivu kwenye mahusiano kama unaficha begi lenye nyara za taifa (meno ya tembo) ndio inafanya tunakufa mapema.
Mimi my wangu akiniumiza nalia kabisa kwa kurusha rusha miguu. Ile kimasta[emoji854]

Unalia na kugalagala sio? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
As a hustler with no secured financial source am scared of failing my family. I will be shown bills and kids' school fees and I will just say "I'll work on it"

The burden gets heavier everyday.

But I have never cried. But getting scared? That happens all the damn time, like "What if there will be no food tomorrow?" "What if rent comes right now?"

Crying is an option but I've never used it yet.

Sure
 
WANAUME WANA MAUMIVU PIA

Mwanamke mmoja aliniambia, 'Ilinichukua miaka kujua kwamba wanaume pia hulia. Nilimchukulia mume wangu kama binadamu bora. Ninamwona akitoka nyumbani kila siku na kurudi akitupa mahitaji yetu. Siku moja nikiwa nimetoka nyumbani na yeye alikuwa nyumbani, nilikumbuka kwamba nilihitaji kuchukua kitu nilikuwa nimekisahau nyumbani, niligeuka na kuelekea nyumbani. Nilipofika nyumbani, nilijaribu kupitia mlango wa nyuma ambao ulikuwa karibu na dirisha la chumba chetu. Nilimsikia mume wangu akilia kama mtoto mchanga akimwomba Mungu anisaidie nipate kazi ili nimsaidie kutunza familia. Hajawahi kunilalamikia hapo awali lakini siku hiyo, nilitokwa na machozi nikigundua kuwa mume wangu ameshikilia maumivu makali yake peke yake"

Binti msichana aliyeolewa muda si mrefu sana, aliwahi kwenda kulalamika kwa mama yake kwamba mume wake amekuwa hamtimizii mahitaji yake, basi yule mama kwa busara kubwa akamuuliza binti yake, ‘Umenunua vitu vingapi kati ya hivyo?” binti akakaa kimya na kusema, ‘Lakini huyo ni mume wangu si ana wajibu wa kunihudumia? Mama akamjibu, 'Je, umewahi kujua vitu ambavyo mumeo anataka umnunulie?".

Wanaume daima hujaribu kuficha maumivu yao.

Wanaume wanaweza kuwa kwenye msoto na wakati mgumu kifedha lakini wanaweza kufake kujifanya kuwa wana kila kitu.

Wanaume wengi wameoa lakini wana maisha ya upweke kupita maelezo.
Wewe mwanamke wakati mwingine jaribu kuongea na mume wako kwa utaratibu na utulivu utapata kitu kikubwa sana kutoka kwa wanaume, Wanaume huwa sio kwamba wako busy kila wakati kama wanawake wanavyofikiria.

Unapaswa kuelewa kwamba mume wako ana maumivu na ana mahitaji pia. Usimhukumu kwa mambo unayotaka kutoka kwake tu, Wakati mwingine mume wako hana mambo unayotaka wewe.

Wanaume pia wana mahitaji na matatizo ya kihisia. Wanaume bado wanalia kwa mapenzi na wanahitaji upendo wa mwanamke ...
Upo sahihi kabisa mkuu

Sent from my M2101K6G using JamiiForums mobile app
 
Hayo nitayaelewa Kwa Mwanaume ambaye yuko honest Kwa mkewe tu lakini Kwa Mwanaume bandidu mchepukaji wala!

Mkuu unaonekana una stress sana Juu ya wanaume kuchepuka hehehee,,,, Comment zako ziko opposite sana na maada husika...

Vipi nini kimekupata Bidada..??? Kijana mwenzetu amekuacha kwenye mataaa au.....

Nimeuliza tu.
 
Hakika umenena vyema mno. Unastahili pongezi japo umejifunza kwa njia ngumu kidogo. Mimi huwa ni muwazi sana lakini najigundua bado siwezi kuwa muwazi wa kiasi hicho. Mwanaume ni kiongozi tangu asili, kwa mke na kwa watoto pia. Kinachotakiwa ni level fulani hv ya uelewa kwa huyu kiumbe maana hawezi onyesha madhaifu wazi. Anaweza katisha tamaa anaowaongoza. Mwanaume ni alama ya nguvu na uthabiti. Ni kielelezo cha uimara.
 
Tabia yetu wanaume ya kuficha maumivu kwenye mahusiano kama unaficha begi lenye nyara za taifa (meno ya tembo) ndio inafanya tunakufa mapema.
Mimi my wangu akiniumiza nalia kabisa kwa kurusha rusha miguu. Ile kimasta[emoji854]
Kaka ukiweza kutoka hapo pia unstahili hongera ila hii ni asili kabisa ya mwanaume na tumelelewa hivyo. Tangu utoto unaambiwa na baba na mama ila haswa baba na kaka wakubwa usilie ww mwanaume, jikaze. Basi inajengwa hvyo tangu asili. Sis wengine tukiwa wenyw ni walaini mno, tunalia hata kwa scene za simanzi tukiwatch movies.
#mara ya kwanza nacomment JF kwa kile alichoandika dada angu kwny Uzi huu.
 
Back
Top Bottom