Wanawake ndoa ni utii, acheni kujaza ujinga wadogo zenu

Wanawake ndoa ni utii, acheni kujaza ujinga wadogo zenu

Ahsañte mama umemaliza Kila kitu ,kupenda na kuhudumiwa tuwachie wao sisi tufanye yetu tunayopaswa kufanya
Unajua Mungu alitugawia haya majukumu ya upendo na utii Ili tukamilishane, Mwanaume ndiye anatakiwa Kupenda, upendo huvumilia, so yeye ataweza kuvumilia mood swings zetu wanawake (ambazo ni natural), upendo huprovide....hapa automatically mume atatunza mke na familia.
Kwa mwanamke tumeagizwa kutii...means utamtunza na kumuheshimu mumeo na kumsikiliza....haya mambo yakikutana automatically nyumba itakuwa na Amani ambayo ndio lengo la ndoa (Ili mpate utulivu).....ndo ukaona zamani wazee wetu walichaguliwa wake/waume na ndoa zilidumu, kila mtu alijua jukumu lake kwenye ndoa.

Leo haki sawa, wanawake na Sisi tunapenda, unamvumilia mwanaume miaka 8 uchumba sugu, hakuhudumii, anakudharau upo kisa unampenda.....hapo hapo una mdomo mchafu humuheshimu.....au mwanaume unaoa mwanamke Hana adabu, hakusikilizi Ila kigezo chako ni ana tako kubwa....halafu utegemee upate utulivu kwenye hiyo ndoa.
 
Sahihi kabisa
 
Assalamualaikum nnawatakia mifungo mema.

Dear girl child kama una malengo ya kuolewa ukae ukijua mwanaume ni kiongozi wa familia aliumbwa yeye ikapita miaka 40 ndo ukatolewa ubavu wake akaumbwa mwanamke. Mungu fundi hakuna sababu ya kuumba sote wawili mmoja ametokana na mwenziwee awe msaidizi wake, hizi feminists activities zinazoendelea ni kuharibu mpango wa Mungu.

Hakuna usawa kati ya mke na Mume isipokua katika kuutafuta ufalme wa mbinguni au kujua lengo la kuumbwa na namna ya kulifikia. Nyie mastrong sijui super woman msituharibie watoto wetu wa kike, asili ya mke ni heshima, mwanaume ni kiongozi wa mwanamke.

Tena siye waislam tunaambiwa kabisa Pepo yako iko kwa mumeo, kumtii mumeo ndo lango la wewe kuiona falme ya Mungu, haijalishi ni kibe10, kizee kikongwe whatever huyo Mume alivo mradi tu anawajaibika kama Mume na anabeba majukumu yake ya kiunaume.

Kuna Wanawake wakiwa nje wanapondea ndoa ila wakiwa Kwa waume zao wanatulia tulii wanafanya majukumu yao mpaka baasi ukiwasikiliza unapotea. Za kuambiwa changanya na zako, ewe mtoto wa kike
Kwenye ndoa hakuna kutoa taarifa kuna kuomba ruhusa Kwa mume, kwenye ndoa hakuna mashindani kuna maelewano.

Sijui lengo la wanaharakati wa ndoa ni lipi. Binti kama anapigiwa, anadhalilka na kufanyiwa unyama hapa hata akiresist ni sawa na ni bora talaka kuliko kuuana.

Wanaharakati wamezalisha kizazi cha wanawake wachepukaji, tusio walezi wazuri, waongo na unaafiki mwingi tunajifanya tunashinda kwenye nyumba za Ibada ila tuna machafu kibao. Ingawa Toka zamani uchepukaji ulikuwepo kwa jinsia ke ila Sasa imezidi tena sio Siri tena.

Kwa Sasa jamii zina macho lakini hazioani, zina masikio lakini hazisikii. Ifike mahala wanawake tujitambue na ktk kujitambua sio kudharau ndoa yako, hiyo ni dhambi kubwa sana tunafanya. Shida iliyopo wanaume wengi siku hizi wanakimbia majukumu yao ya ubaba na ulezi ni sperm donors tu, ila hiyo haifanyi sababu ya mwanamke awe juu.

Ukiona umeshindwa toka, Kaa pembeni lea watoto wako vizuri kabisaa kuliko kuishi na mtu asiyejitambua
Ila kama umepata mwenza muungwana mstaarabu mheshimu, mpende na jengeni familia yenu vizuri, achaneni na wanaharakati uchwara wenye stress na maisha yao.

Ndoa ni kitu kizuri na baraka Kwa wenye akili na uelewa tu.
[emoji91] [emoji91] [emoji91]
 
Back
Top Bottom