Wanawake ni wazuri wakiwa kazini

Wanawake ni wazuri wakiwa kazini

Dame wangu hapaki make up na alishazikataa. Hapaki kucha rangi. She is humble, she cares.

Siyo ombaomba unlike other girls niliodate nao. Anajua maisha nini. Japo hela huwa nampa.

Above all ni mrembo.

She has my repect.

Mapema mwakani namvuta ndani.
Huyo ndio mwanamke halisi, sio unakuta kitu imejipodoa imekua kama kinyago cha mpapule.
 
Chief nauomba basi huo moyo tukapige fweza chap!

Seriously mwanamke akiwa yuko natural huwa napenda sana.
Huwa nikikutana na mwanamke mwenzangu yuko na short hair/ziwe ndefu za asilia,awe na rangi nyeusi flani hivi,asiweke makorokoro mengi uso,amemevaa vizuri halafu ananukia..Jesus huwa nasimamaga tumtazama aiseh sikubaligi apite sijamwangalia.haiwezekani
Inabidi nikuje DM tujue namna ya kukabidhiana moyo na kufanya uwekezaji ulio bora wenye manufaa pande zote mbili .....hahaha
 
Duh mwana kawaza sana mpaka kaleta huu uzi hatari sana ,kweli kazini wanapendeza au sio ndugu zangu
 
Huu uzi ni muhimu sana kwa wanawake wote ndani ya ndoa ambao wakiwa majumbani mwao wanajisahau sana kwa kisingizio cha kupika, kusafisha nyumba etc. Ni ukweli usiofichika huwezi kujiremba wakati unafanya kazi hizo lakini ukimaliza kaoge ujirembe weka nywele zako vizuri kama zile za kuendea kazini 😜😜😜 piga gauni lako zuri hata kama siyo lile la kuendea kazini 😜 ili hata mwenzio ajisifu hapa nilioa banaaa mke wangu mzuri kweli siyo uko nyuku nyuku utadhani ni house girl na kama una house girl yeye anaonekana kajiweka vizuri kuliko mama mwenye nyumba 😜😜😜😂😂😂😂
Habari za Jumapili.

Nikiwa nimetulia ndani jioni namuona mamsap akirudi toka kwenye mishe. Pia alipitia saluni. Katengeneza nywele zake vizuri anavutia kumtazama

Sasa ujinga ni kuwa kufika tu kachukua kilemba kafungia nywele humo kazibania vizuri hata isionekane hata moja! Hapo tayari kuanza mishe za nyumbani. Ule mvuto aliokuja nao ukatoweka.

Ikifika asubuhi anajikwatua tena na kuziachia vizuri tayari kwenda kazini. Huko anakutana na wenzake. Mabosi, vijana, wababa, wapita njia, n.k. Wote kwa nyakati tofauti wanavutiwa nae kwa muonekano ambao alipokuwa nyumbani aliuficha.

Jioni inafika tena anafika nyumbani na kujitupia tambara lake kichwani. Tena anaweza kutafuta na nguo nguo huko akajitupia kisha akaendelea na mishe za nyumbani.

Kwa hali hii hamasa itakuwepo? Hakika yatabakia mazoea tu
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kweli kabisa vitu vipate hewa jamani. Halafu hivyo videra vilivyopauka vinanoga kweli kushindia nyumbani.

Sasa hadi uje utulie ujipare saa ngapi jamani na majukumu kibaao yanakusubiri[emoji2297][emoji2297]
Kawaida ya dera jipya haya yetu ya bei rahisi yanakuwa na fabric ngumu kama karatasi, likifuliwa fuliwa likaanza kupauka linalegea na kuwa laini basi ukilitupia bila kyupi ni burudani sana. 😀

Wanaume msitufananishe na wanawake wa kizungu wanaovaa leggings top na hills ndani. Sisi tuna namna yetu ya kupendeza ndani, kikubwa mtu awe msafi na achane nywele zikae vizuri kama hazijasukwa.
 
Samaki anavuliwa mara moja tuu, labda saiv nawe umekuwa samaki!
Mabaharia wanakwambia kwanini uendelee na kampeni wakati umeshapata jimbo? 😀😀😀😀

Anyways ni somo zuri sana hili, mimi niliumwa kipindi fulani nilivyopona nikajiachia sababu nilikuwa likizo, ilibidi nikumbushwe kwa utani kuwa umejichoka sana, (nakumbuka nilikuwa na wiki kadhaa hata kwapa sijashave, naona hata aibu kuhadithia) Baada ya ujumbe kunifikia Nilipata purpose ya maisha again nikarudi kwenye game.

Mapenzi raha sana kama una mtu anakupenda na mnaelewana.
 
Back
Top Bottom