Wanawake pindi mnapokuwa na miaka 17-25 kwanini huwa hamshauriki mkasikia?

Wanawake pindi mnapokuwa na miaka 17-25 kwanini huwa hamshauriki mkasikia?

Joined
Sep 6, 2024
Posts
69
Reaction score
136
Kwa uzoefu wangu Hawa mabinti kuanzia umri wa balehe Hadi miaka25 au zaidi kidogo Huwa huwaambi kitu wakakusikia.

Haijarishi wewe ni mzazi wake au kaka yake vyovyote vile hata kama wewe ni kiongozi wa Dini au Dr huwezi kumpa ushauri akakusikiliza na then akaelewa.

Unapomshauri muda huo atajifanya anakusikiliza mno Tena Kwa u pole wote lakini akiondoka hapo sana sana atakuona wewe ni adui yake.

Lakini Kwa yule anaye mshauri mambo ya ovyo basi atamuona wa maana kabisa na atampa muda wake wa kutosha hata kama sio ndg yake nk.

Baada ya umri huo kupita ukimshauri hata kuuza ubuyu atakusilikiza na ataanza kuuza ubuyu au kuchoma vitumbua

Wakati hizohizo kazi aliapa hata kuja azifanye maishani mwake.
Mbaya zaidi awe na mtoto tiyari na aliye mzalisha haeleweki yaani Hana mbele Wala nyuma.

Atafanya kazi yoyote Ile..........Hii Huwa inani sikitisha sana.

Jambo hili ni tofauti Kwa wanaume mwanaume mwenye miaka hiyo aliyelelewa vyema husimama kama mwanaume na wengi mitazamo Yao kama sio kusoma basi atajipanga aoe.

Ni wachache sana Ambae unaweza kaa nae ukamshauri habari za maisha asisikie.

Wengi humaliza masomo na kujikita kutafuta maisha Kwa kazi halali. Hii Kwa wanawake ni kinyume utashauri Hadi koo likauke unywe maji lakini amini kazi Yako ni Bure unapoteza muda.

Swali langu kwenu ninyi wanawake watu wazima mliopitia huo umri huwa Kuna changamoto Gani inayowafanya msisikie la mkuu?
 
Inatokana na mabadiliko mbalimbali anayopitia mtu kulingana na umri.
(Stages mbalimbali za mabadiliko)

Kwa umri huo mtu yupo kwenye peak yake ya ulimwengu wake, anaishi ndoto zake zinazowezekana na zisizowezekana, kwahiyo ushauri wako hapo ni kazi bure

Na pia kuwatupia lawama watu wa stage hiyo ni kuwaonea tu maana yake wanahitaji guidance na counselling ya kutosha yani, sio siku moja au mbili udhani mtu anaelewa no!!!

Ni kama kumlaumu mtu ambae yupo katika stage ya balehe kwa tabia mbaya mbaya alizonazo wakati unajua kabisa ni mabadiliko ya kawaida katika umri huo anahitaji kusaidiwa na sio kulaumiwa wala kuachwa
Vivyo hivo kwa mabinti wa umri huo.

(psychological point of view)
 
Inatokana na mabadiliko mbalimbali anayopitia mtu kulingana na umri.
(Stages mbalimbali za mabadiliko)

Kwa umri huo mtu yupo kwenye peak yake ya ulimwengu wake, anaishi ndoto zake zinazowezekana na zisizowezekana, kwahiyo ushauri wako hapo ni kazi bure

Na pia kuwatupia lawama watu wa stage hiyo ni kuwaonea tu maana yake wanahitaji guidance na counselling ya kutosha yani, sio siku moja au mbili udhani mtu anaelewa no!!!
(psychological point of view)
Kwanini ni kuwaonea? Je ni kosa kumuelekeza mtoto wako/ dada yko kwenye njia impasayo.

Huoni akiharibikiwa sisi ndo Huwa tunaona aibu zaidi?
 
Hiyo age huwashauliki na wakibugi kidogo wanazalishwa na kuachwa. Unaweza ukampa mifano yote theory na practical ila still anakuja kutoa boko, sababu ya tamaa au kuendekeza nyege.
Wana shida kubwa sana Kuna mtoto wa ba mkubwa hapa mzee kashafariki. Baada ya kumkanya aache upumbavu wake hakusikia Mimi kaka yake niliyekuwa natoka matumizi ya shule nk nikaamua ni mrambe viboko vya maana hapo yupo form two tu na baada ya kumchapa si akaacha shule Kisha akatoroka nyumbani kaenda huko kazalishwa mbaya zaidi ana HIV Kwa umri wa miaka17 tu Kwa Sasa. Mama Hana uwezo wowote .

Nimeshindwa hata la kumwambia Kwa Sasa.
 
Duh masikini, pole zake..... Bado mdogo kabisa
 
Sio wote mkuu
Wengine tulijua mapema kuwa maisha hayataki lelemama
usipojituma utatumika
Na Bado wapo wengine had Wana 30 plus lkn hwaelew Cha kufanya inasikitisha sana

Kutokushaurika nafikir ni stages tu hata wanaume kunakipind Huwa ni ngumu kuwashauri
 
Wana shida kubwa sana Kuna mtoto wa ba mkubwa hapa mzee kashafariki. Baada ya kumkanya aache upumbavu wake hakusikia Mimi kaka yake niliyekuwa natoka matumizi ya shule nk nikaamua ni mrambe viboko vya maana hapo yupo form two tu na baada ya kumchapa si akaacha shule Kisha akatoroka nyumbani kaenda huko kazalishwa mbaya zaidi ana HIV Kwa umri wa miaka17 tu Kwa Sasa. Mama Hana uwezo wowote .

Nimeshindwa hata la kumwambia Kwa Sasa.
🥲Aisee poleni sana
 
Sio wote mkuu
Wengine tulijua mapema kuwa maisha hayataki lelemama
usipojituma utatumika
Na Bado wapo wengine had Wana 30 plus lkn hwaelew Cha kufanya inasikitisha sana

Kutokushaurika nafikir ni stages tu hata wanaume kunakipind Huwa ni ngumu kuwashauri
Hatma ya mtoto wa kiume na wakike huwaga tofauti kabisa kwa binti wa kike hatma yao inakuwaga mbaya sana.
 
Namuonea huruma sana heri hata angefeli shule sawa kidogo umri ungeenda je Kwa Sasa una msaidiaje?

Kwanza kashatengeneza uadui kwangu eti sikumpenda
Inakuaga hivyo ukimkanya kumrudisha katika njia sahihi unakua ni adui, kudeal na umri huo sio rahisi kwakweli.....

Labda, labda nawe ujifanye kama rika lake ndo walau anaweza elewa.

Pole kwa changamoto unazopitia mkuu
 
Sio wote mkuu
Wengine tulijua mapema kuwa maisha hayataki lelemama
usipojituma utatumika
Na Bado wapo wengine had Wana 30 plus lkn hwaelew Cha kufanya inasikitisha sana

Kutokushaurika nafikir ni stages tu hata wanaume kunakipind Huwa ni ngumu kuwashauri
Nikweli lakini Kuna uafadhari Kwa wanaume kiasi chake.Lakini Kwa wanawake kati ya watano unaweza usipate hata mmoja amini haya....wengi wao ni Bahati Huwa inawaangukia wanakoswakoswa na kupigwa mimba au wanaanza kuyatumia majira mapema zaidi.

Ukitaka kulitambua hili nenda kaulizie wauza madawa (pharmacy) watakuambia Hali ilivyo.
 
Inakuaga hivyo ukimkanya kumrudisha katika njia sahihi unakua ni adui, kudeal na umri huo sio rahisi kwakweli.....

Labda, labda nawe ujifanye kama rika lake ndo walau anaweza elewa.

Pole kwa changamoto unazopitia mkuu
Ahsantee sana hili litapita lakini Sasa hata sisi tunao Watoto wa kike wanaelekea huko ndo najiuliza sana nikwanini hawasikii hivi
 
Kwa upande wangu nadhani haya mambo yanaanzia upande WA malezi na Jamii wanayokutana nayo vijana ..Mfano Mtoto anaweza lelewa Maisha ya kichungaji haoneshwi upande WA pili ni kubanwa Tu kutoka primary Mpaka chuo....

Akifika chuo ni kama fungulia mbwa😁,nikimaanisha Yale yote aliyokuwa akifichwa atataka ajaribu(Ingawa si kwa wote)

Ukija kwenye Jamii tujaribu kuwajenga vijana kuwa marafiki WA wazazi,Jamii sio maadui hii itasaidia Sana kwa maana Mtoto atakuwa muwazi kwa Yale yanayomsibu ...Mfano kijana pindi ana baleghe kuna vitabia vya ukuaji anapitia sasa badala ya kushauriwa hapa tunafanya hivi na hivi, maneno yanaaza"Ooh watoto WA kizazi hiki WA hovyo,mara utakuwa Malaya n.k ".Haya Maneno hayajengi badala Yake yanabomoa mahusiano mazuri hivyo vijana kuwa na tabia za hovyo wanapokuwa
 
Nakumbuka tukiwa wadogo mzee alitumia mbinu nyingi sana za kutuonya, kutushauri, kutufundisha, kutuelekeza katika makuzi yetu. Alikuwa hadi anatupeleka wanapojiuza dada poa anatuambia mnaona wenzenu? Mnavyowaona hivyo wengine wameathirika hapo ni muda haujafika wa kupandisha makenchi na kuteleza nywele ( by then ARV hazijashika hatam) yaan kama mtu ana ukimwi anajulikana tu. Sasa usipoyashika yale na kukaza buti kwenye kitabu utajua mwenyewe anakwambia na mama yenu sitaki ajihusishe na ujinga ulioufanya ukiukwaa tunakutengea chumba chako dah tena anacheka, hapo lazima akili ikukae hakutumia bakora kabisa ila mafundisho yake nayaishi
 
Back
Top Bottom