Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Baadhi ya wanawake katika vijiji vitatu vya Samanga, Kirongo juu na Sangasa, wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro wameeleza tishio la nyani wilayani humo linavyowaogopesha kutembea peke yao bila waume zao wakihofia kudhuriwa na nyani hao.
Wamesema nyani hao ambao hutembea makundi kwa makundi nyakati za asubuhi na jioni, wamekuwa ni tishio kwao na kwamba wanapovamia maeneo yao na kuwafukuza huwakonyeza na wakati mwingine huwazunguka na kuwaweka kati hali ambayo ni hatari kwa usalama wao.
Pamoja na hofu hiyo, wamesema kwa zaidi ya miaka saba wameshindwa kuendeleza shughuli za kilimo kutokana na uharibifu unaofanywa na nyani hao ambao wamekuwa wakila mazao yao mashambani.
Wakizungumza na Mwananchi Digital kwa nyakati tofauti, wananchi hao wameiomba Serikali kuangalia namna ya kuwaondoa nyani hao na kwamba kwa mara kadhaa wamekuwa wakiahidiwa na serikali kuwaondoa nyani hao jambo ambalo halijazaa matunda.
Mmoja wa wanachi wa Kijiji cha Samanga, Prediganda Shayo amesema nyani hao wamekuwa kero kubwa na kwamba wanapoingia kwenye makazi yao na kuwafukuza hawaondoki na badala yake nyani hao huwaita kwa kuwakonyeza.
Pia, Soma: Rombo wanaume walalamika madume ya nyani kushika shika wake zao