Nafasi za kisiasa kushikwa na wanaume ni uboya hizi ni kazi za wanawake, unakuta mbunge kama Msukuma eti anaonekana jembe kuliko mwanamke engineer na daktari, huu ni upuuzi mkubwa na kuna ubunge wa kuteuliwa rais ana viti kumi vya kumpa amatake na kuna wanaume wamepewa nao ni dhaifu?
Tatizo P letu hapa ni utamaduni tu. Wanawake bado hawana haki sawa haswa kwenye uongozi. Angalieni mfano mdogo tu watoto wa miaka 15 wawili wafanye mapenzi na msichana akapata mimba utamaduni wetu na mila nyingi tuta mtenga msichana kumfukuza shule lakini mtoto wa kiume ataendelea. Hata watoto bado hawana akili vizuri wote wamefanya makosa lakini utamaduni wetu ndiyo tatizo. Hao uliowaweka hebu angalia huko kwao kama wameshafukuza mtoto wa kike shule kwasababu ya mimba ya kumwacha mtoto wa kiume shule na ujue hawa ndiyo wale tunaosema wana utamaduni mbaya!.
Hata kwenye jamii zetu angalia Mama na Baba nani anafanya kazi zaidi. Wazee wengi ni ubosi tu hawapiki, hawafanyi usafi, wengine hata kulima hawalimi na isitoshe wengine wanakuja nyumbani jioni baada ya kupitia vilabuni wakiwa walevi. Huku nyumbani hajaacha hata pesa anataka akute chakula, nyumba safi , watoto wameangaliwa n.k. Haya yote ni utamaduni mbovu na wa kizamani. Wenzetu ni team work wote wanasaidiana kwenye shughuli za maendeleo Mama na Baba na nguvu za wawili ndizo zinasadia maendeleo.
Tukiona wabunge na viongozi wa kike wachache tujiulize sababu ni zipi maana si kweli kwamba wanaume wana akili zaidi, si kweli kwamba wanaume ni wachapakazi zaidi na si kweli kwamba wanaume ni wengi zaidi. Lakini kingine kwasababu ya utamaduni hata wanawake wakifanikiwa hatujui mfano wafanya biashara wengi Arusha ni wanawake lakini watu hawajui hilo maana tulishajenga picha fulani kwenye akili zetu. Na hata nchi zilizoendelea bado wanawake wanakuwa wananyanyaswa hivyo itachukua generation nyingine kurekebishika
Ni wanawake wachache sana wenye uwezo wa kusimama mbele za watu na kuhutubia , kuvumilia matusi na vijembe, wenye ujasiri huo wengi wao ni ma "tomboy" (wana tabia za kidume dume)
Uhuni huo huwa unaisha kwa wakati jinsi wanawake wanavyoongezeka katika siasa. Hii movement iliyoanza huko Marekani #MeToo* imeleta balaa kwa miamba wa kujiamini, wanasiasa na matajiri wamepukutika imepelekea hata wengine kujinyonga wakiwa mahabusu. Hivyo ndivyo jamii hustaarabika.
Spika mstaafu wa bunge mama Makinda amesema wakati umefika wa kuweka ukomo wa mbunge wa viti maalum kuhudumu kwa upendeleo huo.
Makinda amedai utaratibu wa viti maalum ulianzishwa ili kuwaandaa wanawake waweze kwenda kugombea majimboni lakini sasa mbunge anakaa zaidi ya miaka 10 katika viti maalum hii si sawa. Hawa ving'ang'anizi wanawanyima fursa wanawake wengine walio wengi.
Marekani wanawake walianza kupiga kura zaidi ya miaka 200 tokea uhuru wao.
Miaka 100 tena baadae ndipo Hillary Clinton akapitishwa kupeperusha bendera na kama sio Russian intrusion bila shaka leo she could be madam President.
It won't be easy.
Mama Makindaa awaache dada zetu, mama zetu wainjoy viti maalum. Kuogombea kutoka jimboni sio jambo jepesi.
Wewe mwenyewe kwenye bandiko lako uchaguzi wa Busanda ilionesha wazi kuwa Lolensia Bukwimba bila msaada wa JPM akiwa waziri, alikuwa ashashidwa kwenye uchaguzi mdogo.
Nimeiangalia hii picha ya wanawake hawa wa wenzetu, na age zao, nikajiuliza sana kuhusu sisi Tanzania na wanawake wetu katika nafasi za uongozi wa kisiasa, tatizo ni nini?.
Jee wanawake wetu Tanzania ni duni au dhaifu Kiongozi wa siasa?. Kama wanawake wetu si duni na si dhaifu na wana uwezo wa uongozi sawa na wanaume, hizi nafasi za Viti Maalum ni za nini?, je Tanzania tumefika mahali nafasi hizi za Viti Maalum zifutwe?.
Hivi hawa baadhi ya wanawake wetu wenye nafasi za juu za uongozi wa kisiasa, wamepata nafasi hizo by deserving au kwa kubebwa na affirmative action?.
Kama watu wawili mna uwezo sawa, kwa nini mmoja afanyiwe upendeleo wa kijinsia kwasababu tuu ya jinsia yake?.
Wanawake ni mama zetu, shangazi zetu, wake zetu, wapenzi wetu, dada zetu, watoto wetu, ni wenzetu na tunawapenda sana, lakini huu upendeleo kwa wanawake lengo lake ni nini haswa, jee hapa tulipofika, bado wanawake wetu wanahitaji upendeleo?.
Paskali
Wanabodi, Nimeona mijadala mbalimbali kumlaumu rais wetu mpendwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli, kwa kuteua wabunge wanaume 6 na Wanawake 2, kati nafasi zake 10 za uteuzi. Naomba kukiri nimehamasika kupandisha uzi huu kufuatia bandiko la mwana JF huyu Mkuu Learned brother Petro Mselewa. Kwanza...
Wanabodi, Leo ni Siku ya Wanawake Duniani, katika safari ya kuelekea usawa wa kijinsia, kuna wanawake wengi wenye sifa na uwezo, lakini wamenyimwa fursa za kushika nafasi za juu kisiasa kutokana na nyingi ya nafasi hizo, kuhodhiwa na wanaume, katika kitu kinachoitwa "mfumo dume!" Swali ni je...
Wanabodi, Leo ni Siku ya Wanawake Duniani, katika safari ya kuelekea usawa wa kijinsia, kuna wanawake wengi wenye uwezo, lakini wamenyimwa fursa za kushika nafasi za juu katika taasisi mbalimbali kutokana na nyingi ya nafasi hizo, kuhodhiwa na mfumo dume, hivyo kushikwa na wanaume!. Swali ni...
Norway kupitia mfumo wao wa bunge toka 1945 mpaka uchaguzi wa mwisho unafanyika 2017 walikuwa hawajatoboa 50/50.
Mama Makinda pia ajuzwe kunaga ubaga, kwenye Uspika kama sio JK kusema safari hii ni zamu wa mwanamke wakasimama na mzee wa Standard and Speed alikuwa hatoboi.
Marekani wanawake walianza kupiga kura zaidi ya miaka 200 tokea uhuru wao.
Miaka 100 tena baadae ndipo Hillary Clinton akapitishwa kupeperusha bendera na kama sio Russian intrusion bila shaka leo she could be madam President.
It won't be easy.
Mama Makindaa awaache dada zetu, mama zetu wainjoy viti maalum. Kuogombea kutoka jimboni sio jambo jepesi.
Wewe mwenyewe kwenye bandiko lako uchaguzi wa Busanda ilionesha wazi kuwa Lolensia Bukwimba bila msaada wa JPM akiwa waziri, alikuwa ashashidwa kwenye uchaguzi mdogo.
Mkuu Freddie Matuja, kwanza nimefurahi kwa reference yako ya Mhe. Lolensia Bukwimba, ni kweli mwanzo kwenye ule uchaguzi mdogo alitoboa kwa kubebwa na JPM, tena kampeni ziliendeshwa kwa lugha ya Kisukuma mwanzo mwisho, bila hivyo asinge toboa haswa kwa kuzingatia Wasukuma ni moja ya makabila yenye male chauvinism na kudharau wanawake. Lakini baada ya kuingia Bungeni, akajenga uwezo, 2010 na 2015 akasimama mwenyewe na akatoboa.
Hivyo Mama Makinda ana hoja ya msingi sana, lengo la viti Maalum liwe ni kujenga tuu uwezo kwa a single term, kisha waende jimboni na sio kubebwa na kuendelea kubebwa tuu!.
P
Usiwe na haraka, hii process inaitwa affirmative action ili kupromote makundi ya watu ambo waliachwa nyuma na mfumo. Imetokea sehemu nyingi sana duniai - hata huko Norway unakotoa mfano huo, na inapofikia makundi yote yako level ground ndipo inafutwa. Kwa Tanzania wanawake wengi waliachwa nyuma kielimu, wengi wao wakiwa wanatayalirishwa kuolewa na kuzaa tu, kwa hiyo waliofuata hawakuwa na role models kielimu na kimadaraka. Sasa hivi tumepiga hatua kidogo lakini bado, tunahitaji kama miaka 15 hivi ili tuwe level ground; Magufuli alifanya jambo zuri sana kumteua mwanamke kuwa Makamo wa rais ili kuharakisha mwendo huo; angalia siku hizi akina Ummy Mwalimu wanavyochachafya kiutendaji.
Nimeiangalia hii picha ya wanawake hawa wa wenzetu, na age zao, nikajiuliza sana kuhusu sisi Tanzania na wanawake wetu katika nafasi za uongozi wa kisiasa, tatizo ni nini?.
Jee wanawake wetu Tanzania ni duni au dhaifu Kiongozi wa siasa?. Kama wanawake wetu si duni na si dhaifu na wana uwezo wa uongozi sawa na wanaume, hizi nafasi za Viti Maalum ni za nini?, je Tanzania tumefika mahali nafasi hizi za Viti Maalum zifutwe?
Hivi hawa baadhi ya wanawake wetu wenye nafasi za juu za uongozi wa kisiasa, wamepata nafasi hizo by deserving au kwa kubebwa na affirmative action?.
Kama watu wawili mna uwezo sawa, kwa nini mmoja afanyiwe upendeleo wa kijinsia kwasababu tuu ya jinsia yake?.
Wanawake ni mama zetu, shangazi zetu, wake zetu, wapenzi wetu, dada zetu, watoto wetu, ni wenzetu na tunawapenda sana, lakini huu upendeleo kwa wanawake lengo lake ni nini haswa, jee hapa tulipofika, bado wanawake wetu wanahitaji upendeleo?.
Paskali
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.