Si mbaya kuwa kwenye mahusiano na mwanaume maana inapaswa iwe hivyo, lakini kwa wanawake tulio single tuwe makini sana.
Unapochagua kuishi pekee yako kwenye nyumba yako uliyopanga au uliyojenga usithubutu kamwe kumkaribisha mwanaume nyumbani kwako, hasa mpenzi wako. Bora uwe unaenda kwake kuliko yeye kuja kwako.
Na pia usikubali akupangishie ni kosa kubwa sana na hilo bora upange mwenyewe ila kama ni kumuomba hela ya pango uwe unamuomba kwa njia nyingine ila usimwambie ni pango itakuwa kero hapo nyumbani kwako.
Yafuatayo yanaweza kukupata kama utaruhusu kinyume chake hapo juu
1. Mwanaume ni lambalamba. Leo utamkaribisha kwako kesho amekuacha; ni aibu iliyoje hicho kitanda kulaliwa na wanaume tofauti tofauti kila mara, bora yeye awe anabadilisha wanawake kwake kuliko wewe mwanamke.
2. Ni marufuku mwanaume yeyote kuja kukusalimia kwako hata kama hampo naye kwenye mahusiano, akikukuta na mwanaume mwingine ndani utakuwa ugomvi wa hatari, na wanaweza akakuumiza akihisi aliye kukuta naye ni mpenzi.
3. Mwanaume atadhani amekuoa,yaani hapo kwako itakuwa kwake,atakutawala balaa,na atakuwa anawaleta marafiki zake hapo kwako, kazi yako ni kupikia mashem
4. Na kama ni mume wa mtu, dunia haina siri,unaweza ukakamatwa ugoni ikawa shida
5. Kama umemchoka mwanaume na unataka uachane naye inakuwa ngumu kumuacha maana kila dakika atakuja kwako, utakuwa unamkuta kitandani kwako amelala hata unune kiasi gani hawezi akaondoka, ugomvi ugomvi ambao utakuwa unaumia wewe.
6. Wanaume walivyo wajinga ukishamkaribisha kwako anawatangazia wanaume wengine ubabe wa kuonekana kwangu, na hujionyesha kwa majirani kuwa yeye ndo baba mwenye nyumba.
7. Wengine mkikosana atataka akunyang'anye vyombo au assets ambazo umenunua mwenyewe au alikununulia na kukuebisha.
Wanawake tushituke, tusifanye makosa.
Kama hujawa wa kuolewa ila unataka kuwa na mpenzi,mkutane huko hotel au kwake kama na yeye yupo single lakini kwako usije ukathubutu, utaumia na utakwama sana.
Sent using
Jamii Forums mobile app