Wanawake tuwe waelewa tukiwa kwenye ndoa jamani

Wanawake tuwe waelewa tukiwa kwenye ndoa jamani

Halafu tukisema humu mwanamke aliyesoma ni LIABILITY kwenye ndoa tunaonekana wapuuzi, mara ohoo.. hatujiamini..blah blah blah!

Labda tuwekane sawa kwenye kitu kimoja na wote mnaojiandaa kuoa wanawake wasomi/wenye kazi muipate hii.

-Kadri mwanamke anavyozidi kusoma umuhimu wake kwa mwanaume unapungua. Na hata akiangia kwenye ndoa ni kwa ajili ya kupandisha social status tu.

-Mwanamke aliyeelimika hasa aliyefika ngazi za juu ana ndoto binafsi nyingi sana za kutimiza na huwa hazifi hivi hivi tu. Anaweza akazitelekeza kwa muda lakini siku akipata fursa ya kuzitimiza ndoto zake lazima aitumie fursa hiyo hata kama tayari yumo ndoani na hajari kama itaathiri ndoa.

-Mwanamke hata awe na uchumi mkubwa kiasi gani lakini ile natural instinct ya utegemezi haiwezi kumtoka, sana sana akijitahidi atakupunguzia mzigo tu kama mmezaa nae yeye atajigharamia mwenyewe huku watoto akikuachia wewe.

-Kadri mwanamke anavyozidi kuishi na wewe kwenye ndoa ndivyo anavyozidi kukuchoka hasa kama anajiweza kiuchumi na haoni hatari kuvunja ndoa maana hana cha kupoteza.

Kiufupi tu ni kwamba wanawake wasomi ni watu wenye matatizo mengi sana ndoani.

To a woman more education more problems in marriage-wise.
Ni liability kwako sio kwa kila mtu.
Wewe kama unaona Ni liability wenzio wengine wanaona Ni asset.
Ulitaka tuwe wajinga tusisome???
 
Kuna wadada huwa wanadhani mwanaume Ana hela Muda wote,yaani hata ile huruma kumhurumia kidogo haipo..wadada sisi tuna roho ngumu jamani,Mwanaume nae Ni binadamu Kama sisi.
Tunapaswa kuwashika mkono hata Kama Ni kidogo.i(la hapa si kila mwanaume wa kufanyiwa hivyo.,wengine hii huruma hawastahili.)
Wanaume nao akili zao sijui zipo wapi,unakuta nae anatoa tu hovyo..watazidi kuwanyoosha
Empathy ni muhimu sana kwenye mahusiano.

Mwanamke akikosa Empathy hata Endurance itampa shida. Ndoa itaenda kaput.
 
Huwezi kujua kwa sababu kuna ndoa inakuwa imevurugika hasahasa kama mme anachepuka na mke anajua, na labda kabla ya hapo alikuwa anachangia matumizi bila shida lakini leo mme anahonga nyumba ndogo hivi mke ataendelea kutoa hela kwa moyo jamani

Acheni kutwisha Lawama wanawake kwa kisingizio kuwa wao ni wabaya na wanaweza kukosa kuolewa, niwaambie tu kadiri umri unavyoyoyoma mwanaume ndio anahitaji zaidi kuwa na mke.

Mleta mada atakuwa ni nyumba ndogo ya jamaa ndo maana kaijua story nzima wakati ni mambo ya ndani, kusimuliwa na Mchepuko wake... Shame on you
Kwa hii case nahisi chanzo Ni mchepuko.
Kamwe siwezi msaidia mwanaume msaliti.
 
Kwajinsi ulivyo elezea, nimejikuta mawazo yangu yanaamini kwamba wewe ni mchepuko wa huyo unae muita kwa jina la kaka mmoja....
Kwa connection tu sikuwezi![emoji1316][emoji1316][emoji1316]
 
Bado nina hasira ntaandika neno moja moja.Women are so selfish!Huwa wanajenga kwao,najiuliza je na mamaake na bibi yake wengejenga kwao ingekuwaje?
 
Anataka tuwe vilaza watuburuze vizuri
Ukiingia kwenye ndoa hakuna mimi kuna SISI,Wakristo si huwa mnasema mwili mmoja?unakuwaje mwili mmoja nusu inafuraha na nusu inahuzuni?Wewe huna mume and with that attitude you wont have a husband,utazalia nyumbani!
 
The same woman, mwanaume akikomaa akapata hela akaanza umalaya na dharau mwanamke atasema wanaume hawana maana.

Wanawake muwe makini sana kuwasimang'a wanaume zenu kipindi hawana hela maana akipata hela atalipiza tuu, hii ni akili ya wanaume wengi maskini.unamvumilia sababu hana kitu na unaendelea nae huku unamsimang'a,sawa sina hana kitu,sasa akizipata ndo utajua uvumilivu una kikomo...
 
Jukumu la kutunza familia ni la mwanaume, imeandikwa katika vitabu vyote vya dini. Sitaishi kwa kumtegemea mwanamke hata awe kiongozi mkubwa na mwenye mshahara mkubwa mara 10 yangu.

Nitaishi kadri ya uwezo wangu na cha mke wangu itakuwa ni ziada tu ila daima sitamtegegemea haswa katika yafuatayo 1. Kulisha familia, 2. Ujenzi wa nyumba, 3. Ada za watoto, 4. Malipo ya maji, umeme, TV, nguo za wanafamilia, malipo ya wafanyakazi (house girl, house boy, mlinzi) n.k.

Mwanamke anachopata kitakuwa nyongeza tu. Ndio kanuni ilivyo hata kama analipwa mara tano Zaidi yako usimtegemee utakuja kulia kilio cha mbwa koko mdomo juu
 
Sasa kama jamaa anachepuka mimi nikioa kuna shida gani,kizuri kula na mwenzio mkuu
Hakuna shida mkuu... Oa tu, lakini usijidanganye kuwa huyu anayemsema mwenzake haachi hela nyumbani kwamba yeye ndo atakuwa anatoa hela ya matumizi...
 
Ingekua mie akifika tu kwao namuambia ukirudi ukatafute pa kuishi hapa hapakufai
Mwanamke umebahatika kupata mwanaume wako wa ndoa,mnaishi vizuri tu,lakini kwa nini sisi wanawake tunakuwa tunawategea wanaume na huku unajua fika hali ya mmeo? Na huku tuna ingiza vipato vyetu wenyewe

Kuna mkaka nimemuonea hadi huruma

Huyu kaka ni mfanyakazi wa serikali na mke wake pia

Siku za hivi karibuni amemaliza chuo,ila gharama za chuo alikuwa anajigharamikia kwa kiasi kikubwa na kulingana na maisha ya chuo na gharama ,aliweza kukopa kwenye Benki moja hivyo kwa wastani kwa makato ya mshahara wake ,mshahara ukawa mdogo sana,na ulivyotoka wa mwezi uliopita alilipa kodi ya nyumba na nyingine kwenye shughuli za kilimo,akawa hana kitu

Na bahati nzuri mke wake anajua hali yake ya uchumi na kila kitu

Sasa leo mke wake kasafiri kwenda nyumbani kwao,na kwa vile mke wake anajua hali ya mme wake,mwanaume akafikiri mwanamke angefanya shopping ya mahitaji ya ndani kabla hajaondoka ili watoto wao watatu na mmewe wasipate shida

Lakini mwanamke hakununua mahitaji ya ndani ameondoka kwenda kwao akisema wazazi wake wamemuita kwa dharura

Mwanaume alivyojaribu kumuuliza "Mbona umetuacha bila kitu ndani?

Majibu ya mwanamke" Hivi wewe si ndo mwanaume, yaani unadiriki kuniambia jambo kama hilo,kwani mimi ndo mwanaume wa familia,wewe fanya mpango mle na wanao lakini sio kuniambia mambo ya ajabu"

Loh! Kaka wa watu mpaka nimemhurumia,

Jamani na sisi wanawake tuwe na utu,familia ni ya wote, na kama mwanaume hali si nzuri,ajibika asilimia 100,lakini si kwa roho mbaya hiyo
 
Ila huyo kaka ana moyo nae kumuuliza mwanamke "Mbona umetuacha bila kitu ndani?

Kaka zangu tafuteni hela tafuteni hela mbebe majukumu yenu wenyewe
mbona wanaume wengi hawasem lakini hayo maneno maneno ya kukatisha tamaa wengi wanaambiwa, ila hilo la mbona umetuacha bila kitu ndani,mmh wanaume wa chache wanauwezo wa kuuliza wengi wanakufa na tai shingoni mtu anaona bora akope kwa riba a solve tatizo
 
🤣🤣🤣🤣🤣 nakubali baharia, hawa watu wanatufanya mabaharia watu wa hovyo hovyo tu huko ndoani!!!

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom