Naweza nikawa nimefanya mengi katika maisha yangu, lakini hata siku moja sitakuwa sehemu ya wanao endekeza udini kwa namna yoyote ile.
Kwa muktadha huo, ningependa ndugu yangu usinituhumu kwa jambo ambalo mbali tu na kulifanya sijawahi kuwa mfuasi wake (huo udini).
Ningependa tujadili hoja kwa kuzingatia kile tunachokiona badala ya kuendeshwa na hisia pamoja na dhana; tujikite kujadili hoja kwa kuepuke kutoa tuhuma ambazo hazina tija kwa wachangiaji ili kuzuia kuhamisha mjadala na kupoteza lengo.
Tujifunze ustaarabu, hata kama imetokea wazazi wetu hawajatufunza, basi tuige.