Wanawake wa JF mbona huwa mnafunga PM zenu?

Wanawake wa JF mbona huwa mnafunga PM zenu?

Habari za saa hizi wapendwa?
Natumaini hamjambo na ni wazima kabisa kama mimi nilivyo mzima.

Waungwana kuna jambo ningependa kufafanuliwa kwanini wanawake wa humu wanapenda kufunga PM zao?

Maana nimeliona Mara nyingi sana hili suala la wanaume kupiga magoti na kujishusha wakiomba kufunguliwa PM ili waweze kuongea Yale mambo ambayo huwa hayaongelewi public.

Ningependa kupata ufafanuzi wa kina na upembuzi yakinifu kuhusiana na hili suala.
Mkuu hili tangazo lako lina leseni??
 
Sijawahi kusema pale penye ninaishi aiseeeee.....
Zaidi napita sana hapo Dom, nakuwepo sana Dar, naonaekana sana Tabora, ingawa ninaishi Ushirombo... tehteehhh
Au ni jirani yake Ndugai salasala?
Nakumbuka ulizungumzia ujirani na kisa cha huyu mtu
 
Au ni jirani yake Ndugai salasala?
Nakumbuka ulizungumzia ujirani na kisa cha huyu mtu
Alichomfanyia Kaka Jo.. wa pale jirani na Reef-1..... Haki Mungu anamuona huyo bosi kubwa wa nguzo nzito ya 3 Tanganyika... tehteehhh
 
Mimi nilifunga ya kwangu kulingana na usumbufu wa (vivulana), yaani mtu anaingia halafu anaongea ujinga. Imagine mtu anakwambia naomba picha yako ukiwa mtupu!!!🙁🙁🙁
Mwingine anakazania kuomba umpe namba ya simu utadhani anataka kurekebisha muamala kumbe pumba tupu
 
Hahaaaa. Hivi wale niliowaachia mlango wazi na wewe si mmoja wapo rafiki.

Nikalala mapema kama kawaida yangu rafiki.
Hahah!...

Yani ratiba yako ya kulala huwa inanifurahisha sana ujue...
 
Back
Top Bottom