Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 14,762
- 32,386
Wanawake wa Kiislamu nchini wamemuomba Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan awape ufadhili wanawake wenye hali duni kwenda Hija na Umrah kila mwaka ili kufanikisha wajibu wao wa kidini.
Akizungumza jijini Dar es salaam leo Machi 26,2025 kwenye kongamano lililowakutanisha wanawake zaidi ya 1,000 mwanzilishi na Mwenyekiti wa Ladies In Islam, Salha Aziz amesema “Wanawake wa Kiislamu tunakabiliwa na changamoto ya fursa chache za kwenda Hija na Umrah , wengi wanakosa fursa ya kutimiza nguzo hii ya Uislamu kwa sababu ya hali ngumu ya maisha na kipato duni.”
“Tunamuomba Rais afadhili wanawake wa Kiislamu wenye hali duni kwenda Hija na Umrah kila mwaka, kulingana na idadi atakayoturidhia, hili litawapa fursa ambao hawawezi kumudu gharama za ibada hii muhimu kufanikisha wajibu wao wa kidini”
“Tunakuomba kwa moyo mkunjufu upokee maombi yetu na utusaidie kuyafikisha kwa Rais ili tuweze kufanikisha lengo hili kwa baraka za Mwenyezi Mungu, tunaamini kuwa kwa msaada wake, ‘Ladies in Islam’ itaendelea kuwa chachu ya maendeleo kwa wanawake wa Kiislamu na jamii kwa ujumla. “Tunamuomba Rais Samia atusaidie pia kupata eneo la kudumu kwa ajili ya ofisi yetu ili tuweze kutekeleza shughuli zetu kwa ufanisi zaidi”
Mgeni rasmi wa tukio hilo la leo ni Katibu Mkuu Kiongozi wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Zena Said Ahmed ambaye amemwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan.
My take
Sijui ni nani huwa anatuhujumu Hii Dini yetu. Siyo Bure tunahujumiwa. Mara ya pili hii tunaongea hivi